naomba msaada wana jamvini, sheria inawezaje kumhukumu mtu ambaye bila ya ruksa kaweka number ya msichana mmoja kwenye mitandao na kudai kwamba eti anatafuta mchumba, wakati siyo kweli... sasa usumbufu mkubwa wakupigiwa simu anaupata huyu dada naombeni msaada
Mosi,
huyo amevunja haki yako ya faragha.(Right to privacy)
Katiba ya Tanzania katika Ibara ya 16 (1) inasema"Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi"
Pili,
amejifanya ni mtu mwingine kwa kupitia kompyuta.(Impersonation)
Hili ni kosa la kimtandao na adhabu yake ni milioni tano au miaka saba.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.