msaada wa kisheria kuhusu madai | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada wa kisheria kuhusu madai

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mary Glory, May 23, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. M

  Mary Glory Senior Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wanajf ninaomba msaada wa kisheria kuhusu hili.namdai mtu shilingi milioni tano.hatukuandikishana popote nilipokuwa nampa hizo pesa.yeye anakiri kwamba namdai ila kulipa ndo anasumbua.nimejaribu kumuomba tukaandikishane anakataa.je nifanyeje ili niweze kupata pesa zangu?
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Unaweza au usiweze kuzipata hizo pesa. Hili litategemea kama kulikuwa na mkataba kati yenu. Mkataba sio lazima uwe kwa maandishi. Ila ukiwa wa maandishi ni rahisi kudhibitisha. Pia inategemea kama ulimpatia hizo pesa kama zawadi au mkopo. Tatizo linakuja kwenye ushahidi. Hakuna maandishi (promissory note) kudhibitisha kuwa ulimkopesha na aka-promise kukurudishia hizo pesa baada ya muda fulani. Ulimpaje hizo pesa? Kwa hundi or bank transfer? If so, unaweza kutumia hizo kama ushahidi. Lakini kama ulimpa cash itakuwa ngumu unless kama kuna watu walioshuhhudia ukimkabidhi hizo pesa kama mkopo. Kati ya hizo milioni 5, hajawahi kukurudishia hata kidogo? Kama amekurudishia kidogo unaweza kutumia hiyo kama ushahidi kuwa unamdai ndio maana amekurudishia kidogo. Still bado ni ngumu na itategemea alikurudishia kwa njia gani.

  Katika kukopeshana huko mlishawahi kuwasiliana kwa text messages or email? Kama kuna correspondences kama hizo unaweza kuzitumia kama ushahidi wa mazingira kujaribu kuonyesha kuwa ulimkopesha. Pia hizo pesa alienda kuzifanyia nini? Kwa mfano kama alizitumia kupata bail, then unaweza tumia hiyo bail kama ushahidi. Still hii bado ni ngumu. Kama huna ushahidi wowote kilichobaki labda yeye mwenyewe akubali kuwa unamdai. Otherwise, itakuwa vigumu sana kumshtaki na kushinda kesi. Anaweza akakataa au akasema tuu kuwa ulimpatia hizo pesa kama zawadi (gift). Hata kama una ushahidi wa kutosha, pia angalia kama huyo jamaa kama ana uwezo wa kulipa ukimpeleka mahakamani. Usije ukakuta unaingia gharama za bure na kupoteza muda wako.

  Lakini nafikiri hapa utakuwa umepata fundisho ili usirudie kosa kama hilo. Sina maana kuwa usimkopeshe mtu tena kwa sababu iko siku na wewe utahitaji kukopa. Huwezi jua. Cha kujifunza hapa ni kwamba, next time ukikopesha jaribu kutengeneza ushahidi in case akikataa kulipa. Badala ya kumlipa cash tumia njia nyingine kama hundi au bank transfer kutoka kwenye account yako kwenda yake. Tengeneza mazingira ili mtumie mawasiliano ya kimaandishi zaidi wakati anaomba mkopo. Kuandikiana mikataba inategmea na mahusiono yenu na kiasi cha mkopo. Kama mkopaji anasisitiza umkopeshe kwa cash badala ya hundi or bank transfer, au anakataa kutumia aina fulani ya mawasiliano, then think twice.
   
 3. M

  Mary Glory Senior Member

  #3
  May 24, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanx kwa ushauri.nilimpa hizo pesa kwa cash.nilizotoa kwenye account yangu then nikampa.hatukuandikishishana coz ni mume wangu.so ndo maana nilimpa bila maandishi..mbele ya ndugu zangu na ndugu zake anakiri kuwa nilimpa hizo pesa.but hasemi ni lini atarudisha na me natakiwa nilipe hizo pesa.nilishawahi kumpeleka kwa mchungaji wake na akakubali kuwa namdai na atalipa.je naweza kumtumia kama shahidi?nimejifunza ndugu yangu sitamkopesha yeyote bila maandishi.
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  May 26, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Duuh kumbe ulimkopesha mmeo na leo umekuja kumwandika hapa ..Hii ndoa ipo kweli?
   
 5. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #5
  May 26, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  pole sana mary glory kama alivyokushauri EMT sio rahisi kuzipata hzo pesa samehe alafu umesema ni mmeo je mna mtt nae? je aliichukua kufanyia nn? mpaka umeamua kumpeleka kwa ndugu na wachungaji na hapa jf lazima akuna mahusiano tena na kama nipo sahihi hizo pesa itakuwa mlipeana kimapenzi or ulimwonga ss amekubwaga/umembwaga mnaanza/unaanza kudaiana k2 ambacho sio kzuri na kama amekubali mbele ya ndugu zake/zako na kwa pasta wake/yako shida yako nn? ushauri wangu mvumilie mpata atakapo kulipa mana inaonyesha kabisa una hushaidi wowote ule ataukisema uchukue ndugu zako/wako na pasta bado sio ushahidi tosha alafu umesema ni mumeo sio vzuri kumfanyia mumeo hivyo mngemalizana chumbani kama mlivyopeana na sio kutangaziana hadharani kama ivyo kama umeshamwaibisha hivyo anaweza ata asikulipe kwa jinsi unavyomzalilisha kumdai kama ivi.
   
 6. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #6
  May 26, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  nina shaka kama hyo ndoa ipo tena FL kweli mke mpumbavu uivunja nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe ebu fikiria mmeo ajue umemwanika jf inakuwaje
   
 7. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #7
  May 26, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  umesema umempa mumeo madai ya nn? inaonyesha ulimpa kama zawadi na sio kibiashara mwisho wa cku mambo hayakwenda sawa ebu kuwa wazi zaidi upate msaada zaidi kwa ushahidi wa pasta bado uwezi kutumia kwani aliandika kwa maandishi mbele ya pasta? kama ni no anauwezo wa kuwakana ajasema ivyo amwezi kumlazimisha
   
 8. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #8
  May 26, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kama ni mume wako, then itakuwa ngumu zaidi. Kwenye sheria za mikataba kuna kitu kinaitwa "intention to create legal relations" kwa kiswahili "kusudio la kuunda mkataba wenye nguvu ya kisheria." Kusudio la kuwa na nguvu ya kisheria katika uundaji mkataba ni kipengele muhimu sana ambacho mahakama huangalia ili kuweza kuona kama kweli wahusika walikuwa na haja ya mapatano yao kuwa na nguvu ya kisheria. Kama wakati mnaingia kwenye huo mkataba hamkuwa na kusudio la mkataba kuwa na nguvu ya kisheria, hautaweza kushinda mahakami. Kwa maneno mengine ni kuwa ili uweze kumshtaki mume wako kwa kuvunja mkataba lazima muwe mlikusudia mwanzoni kabisa kuwa hayo makubaliano ya kukopeshana yatakuwa na nguvu ya kisheria.

  Sasa kuna presumption kwenye sheria kuwa mikataba kati ya wanafamilia (acha ile ya kibiashara) haina kusudio la kuwa na nguvu ya kisheria. Kama unaelewa Kingereza ni hivi: "Where an agreement is reached between family members or friends in a domestic context, then the presumption is that there is no intention to create legal relations." Lakini unaweza kupinga hili mahakani kama una ushahidi unaonyesha kuwa wakati mnaingia kwenye huo mkataba mlikusudia uwe na nguvu ya kisheria. Kwa maana nyingine yalikuwa ni makubaliono ya kibiashara zaidi kuliko ya kifamilia. Kwani uhusiano wenu wakati unamkopesha na sasa ukoje? Kama ni mzuri kesi itakuwa ngumu. Kama sio mzuri mfano wakati unamkopesha mlikuwa kwenye process ya kutengana, then unaweza kusema makubaliano hayakuwa ya kifamilia. Whatever, the case bado una kesi ngumu.
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ndoa imeingia bundi hiyo!
   
 10. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mchungaji kumbe hii kesi ilishafika mpaka kwako? Makubwa!

  Uko tayari kumtetea mahakamani kama shahidi? Otherwise you need to sort out this mess!
   
 11. M

  Mary Glory Senior Member

  #11
  May 26, 2011
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Thanx.kwa sasa naangalia navyoweza kurecover my money,hayo mambo mngine just wait
   
 12. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Lakini make sure unatumia njia halali ku-recover the money bila kuvunja sheria.
   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Wakuu heshima mbele jamani nisaidieni nifanyeje m2 anapokupakazia anakudai anapita kwa marafiki ndugu na wote wanaokujua ana kielelezo chochote akiambiwa mpeleke polic ataki mkikutana 2 anakwambia nitakuabisha mpaka ujute naitaji kukomesha hii hali mana utani utani imeanzakuwa kero
   
 14. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Huyo mtu wako yupo hapa

  na anasema anachotaka yeye ni pesa zake umrudishie

  kwa nini usimrudishie hizo pesa yaishe?????????????????
   
 15. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  sio lazima ujibu kila post kujaza idadi kama una jibu unasoma unapotezea
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye red nachukulia hakudai. Then, anachokifanya inaweza kuwa slander (malicious, false, and defamatory spoken statement with the intention to damage your reputation). Kusanya ushahidi wa anayokutendea if possible record kwenye diary. Akizidi mpe formal warning aache. Asipoacha chukua hatua za kisheria.
   
 17. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mkuu ushahidi upo wa kutosha kabisa nimemrecord nina sms zaidi ya 600 na rb ninazo zamatukio mbalimbali nimempa warning ackii nipo kwenye proces ya kumwona lawyer ili nidai compasation kwa kunichafulia jina langu
   
 18. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu mnaishi eneo moja. Ingekuwa vizuri ukamshirikisha mkuu wa kitongoji pia kujaribu kusuluhisha.

  Otherwise, Mkuu mwandikie formal letter. Ziko sample letters kwenye Google kibao kama hii niliyomodify.

  Dear X

  Re: INTENTION TO TAKE LEGAL ACTION

  For long time [specify the period], you have been spreading disparaging remarks about about me. The remarks are [list them]. These remarks are untrue and malicious and constitute slander against my reputation and credibility. My credibility and good reputation are the fundamental to my personal character and I treat your attempt to damage my character with the utmost seriousness.

  This letter will constitute notice to you that unless you immediately cease and desist from making such remarks, I will notify my lawyer to institute legal proceedings against you claiming the full amount of the damages suffered by me.

  Kindly govern yourself accordingly.

  Sincerely,

  Drphone


  Hakikisha unapata udhibitisho wa kimaandishi kuwa amepokea hiyo barua. Huo ushahidi uifadhi utaihitaji pindi utakapoamua kumpeleka mahakani. Mkuu wakati wakati unafanya haya make hakikisha mikono yako ni misafi pia.
   
 19. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #19
  May 31, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu EMT ninavyoona hawa watu wanafahamiana na there is a personal issue between the two. Inawezekana pia kuwa kuna madai au hakuna madai na wanachafuliana. Maana kila anachojibu jamaa kuna mtu hapa anaitwa Mary Glory anamjibu kuwa anamdai na personal issues nyingine. Naona kwanza jamaa angekuwa wazi kuwa hadaiwi na hakuna issue between the two bdo utoe msaada kisheria maana naona kama unajitahidi kutoa msaada kisheria wakati it seems there is a hidden agenda
   
 20. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #20
  May 31, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Umenifumbua macho, naona haya ni majibu ya huyo niliyembold 7bu alikuja hapa jamvini na kulalamika kuna mtu amemkopa hela hataki kumrudishia.Hebu malizaneni bana
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...