mwenye mwembe kafanya trespass, ushauri tu, mwenye nyumba kajilipa fidia kwa kula maembe ya mwenzake na mwenye mwembe anapaswa kutoa mwembe wake huko kwa jiran, hakuna wa kumlipa mwenzake
Nashukuru wote mliochangia, tulilimaliza shauri kwa kukubaliana hivi:
1) Mwenye mwembe, utaendelea kuwa mwembe wake na tachuma maembe ya uoande wake.
2) Maembe yanayoning'inia upanda wa jirani, jirani atayachuma na kuyafaidi bila kuomba idhini wakati wote ambao mwembe utakuwa hai.
3) Mwenye mwembe na Jirani wasimsahau (kaimu mjumbe wa nyumba kumi (mimi)) kila watapochuma maembe.
Kwa hiyo katika kesi yako hii kuna masuala mawili. Kwanza ni hilo la huo mwembe kuingia kwa jirani na pili jirani kuvuna au kuokota matunda ya mwembe ambao sio wake.Jamani mtaani kwangu hakuna mjumbe wa Nyumba kumi aliye "official" lakini mara nyingi huwa kesi ndogo ndogo naletewa mimi kuzipatia ufumbuzi kutokana na umri wangu.
Kuna hii nimeletewa jana na nimeshindwa kuamua hapo kwa hapo na nimeomba nipewe muda kuipatia ufumbuzi, naomba msaada wa kisheria au kisharia kwenye hili:
Kuna mtu ana mwembe uwani kwake, ule mwembe uko karibu na ukuta wa uwa wa nyumbani kwake lakini kwa juu matawi yametokeza mpaka upande wa pili wa uwa ambako ni kwa jirani yake. Jirani anachuma maembe yanayoning'inia upande wake na anasema hiyo ni halali yake na mwenye mwembe anadai alipwe, jirani nae anasema basi kuanzia leo kama unataka nikulipe, na wewe uje kufagia majani na taka zingine za mwembe zinazodondokea uwani kwangu. Wakaamuwa waje niwatatulie hili kasheshe, nikawaomba wanipe siku tatu, sina ufumbuzi wa haraka.
Jumatano Jioni watakuja kwangu kupata ufumbuzi, naomba mwenye kuijuwa hukumu ya hili iwe kisheria au kisharia anisaidie.
Kwa hiyo katika kesi yako hii kuna masuala mawili. Kwanza ni hilo la huo mwembe kuingia kwa jirani na pili jirani kuvuna au kuokota matunda ya mwembe ambao sio wake.
Hilo la kwanza. Mimi naamini kisheria, hupaswi kupanda au kujenga vitu ambayo vitaingia kwenye property ya mtu mwingine (sio matawi hata mizizi) - isipokuwa kama kuna makubaliano. So huyo mwenye mwembe alitakiwa kuhakikisha matawi ya mwembe wake hayawi kero kwa jirani yake either kwa uchafu (shedding) au uwezekano wa kuharibu nyumba ya jirani kama matawi (au hata mizizi) yataanguka au kujongea na kusukuma nyumba au sehemu ya nyumba. Ndio maana tunapopanda miti tunashauriwa kwanza kufahamu tabia za miti hiyo ili kuweza kupanda sehemu muafaka katika eneo lako.
Hilo la pili, linaanzia kwenye hilo la kwanza. Huyo jirani hana haki ya kuvuna au kuokota matunda kutoka kwenye mti ambao sio wake. Lakini anaweza kudai fidia (ambayo inaweza kuwa kubwa kuliko hata hayo thamani ya hayo matunda) kwa usumbufu/uharibifu ambao mwembe huo unamletea. Anaweza pia kumtaka huyo jirani kuondoa matawi yote ambayo yanaingia upande wake.
Btw, hao watu ni kabila gani?:lol::lol::lol:
Hivi huyo ambaye matawi yanaangukia kwake, ikitokea siku moja tawi likavunja kioo au likaumiza mtu atakubali yaishe kwa kuwa nae anafaidi maembe? Nafikiri ushauri mzuri na wa kudumu ni kukata hayo matawi, labda kama mjumbe unapenda kuneemeka na mgawo wa hizo embe. Mfano wa mkahawa (Omumwani) sikuuelewa vizuri maana mimi nakumbuka kule kwetu tawi likizidi kwenda kwa jirani huwa tunalifunga na kamba ili lielekee nyumbani.