Msaada wa kisheria - kuchukua sheria mkononi

Kilele9

JF-Expert Member
Jun 1, 2017
1,452
1,091
Wasomi /wakuu habari za siku,
Mimi ninatatizwa na usemi hapo juu maarufu "kujichukulia sheria mkononi"
Hivi karibuni kumetokea baadhi ya wananchi kufanya maamuzi kinyume na sheria
(nionavyo mimi) na hapa ndipo ninaomba ufafanuzi/ kufahamishwa.
Mifano ni mingi ila kwa sasa ninanukuu huu hapa:

"Dar es Salaam.
Watu watano wanaodaiwa kuwa ni wahalifu wameuawa katika eneo la Toangoma jijini Dar es Salaam, katika majibizano ya risasi na Polisi yaliyotokea usiku wa kuamkia leo Ijumaa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke, Emmanuel Lukula amesema walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna njama za uhalifu zimepangwa kufanyika maeneo hayo usiku wa jana, hivyo wakajipanga kwa ajili ya kudhibiti.

Amesema ilipofika muda walioambiwa kweli wahalifu hao ambao idadi yao haikuweza kupatikana, lakini walikuwa wengi, wakafika eneo la tukio na kupambana na polisi.

“Majibizano ya silaha yalikuwa makubwa kwa sababu walikuwa na silaha nzito, lakini Jeshi la Polisi lilijipanga imara kuwadhibiti na kufanikiwa kuua watano na wengine wakatokomea kusikojulikana,” amesema."

Kama hiyo hapo juu ni kweli watuhumiwa watano wameshahukumiwa kabla ya kufika
mahakamani na hakukamatwa hata mmoja wa kuendesha kesi .

Swali langu:
  • Je hivi ndivyo utawala wa sheria unavyotaka !?
  • Je wananchi mmoja mmoja au kikundi wakifanya hivyo jeshi letu na mahakama zetu zitaamuaje?
 
Ndugu;
Ni rahisi saana kuwalaumu polisi wetu wanapoifanya kazi yao kwa weledi. Hebu fikiri; Ingelikuwa ni weye, umetumwa kulikamata jambazi lenye silaha nzito nzito.

Uliambie toka nje mungu akuone; wadhani huwa linatoka na mikono mfukoni?? Sasa Kamanda kasema, yale majambazi yalijibu kwa moto. Ulitegemea kama polisi wangelikimbia na kwenda kujificha ni nini kingelitokea?? Ni neno gani ungelisema hapa?

Jamani, tusiwalaumu polisi bali tuwaelekeze majambazi kuacha hiyo ofisi. Hailipi chochote.
 
Ndugu;
Ni rahisi saana kuwalaumu polisi wetu wanapoifanya kazi yao kwa weledi. Hebu fikiri; Ingelikuwa ni weye, umetumwa kulikamata jambazi lenye silaha nzito nzito. Uliambie toka nje mungu akuone; wadhani huwa linatoka na mikono mfukoni?? Sasa Kamanda kasema, yale majambazi yalijibu kwa moto. Ulitegemea kama polisi wangelikimbia na kwenda kujificha ni nini kingelitokea?? Ni neno gani ungelisema hapa?

Nia ya bandiko hili si kuwalaumu
askari wetu wa usalama (polisi) au mtu yeyote yule
bali ni kuweka mazingira sawa. Tunaweza kurekebisha katiba na sheria ila sheria moja isiwe inatumika visivyo
Aidha askari wapewe mafunzo na vifaa bora zaidi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao n.k
 
Asant mkuu
 
kwa maelezo yako polisi walikuwa wanafanya self defence/kujilindana mashambulizi ya majambazi itakuwaje kujichukulia sheria mkononi.
 
Nia ya bandiko hili si kuwalaumu
askari wetu wa usalama (polisi) au mtu yeyote yule
bali ni kuweka mazingira sawa. Tunaweza kurekebisha katiba na sheria ila sheria moja isiwe inatumika visivyo
Aidha askari wapewe mafunzo na vifaa bora zaidi kwa ajili ya kutekeleza majukumu yao n.k

Swali ni kwamba; Je, hao majambazi wataenda likizo au? Ili kuwe na fair play hapo kusikwe na upande unao wagandamiza wengine hapo? Jambazi haliji kwako kucheza drafti bali ni uhai wako na au malizako. Umewahi vamiwa na jambazi??

Chukulia mfano; Umevamiwa nyumbani kwako, mbele ya mkeo na watoto. Kama kuna msichana kati yenu, abakwe mbele yako halafu wambake mkeo, halafu wakulazimishe uwape hela ulizouza mahindi siku hiyo.

Hapo wewe waona kuwa kuna haki ya kuishi?? Imetokea wala sio hadithi. Nadhani kama ungesha patwa na msiba ka huu, wala usingeli kuja hapa JF na kusema, polisi wasiwauwe hao majambazi.

Hivi wajua kwamba kuna wakati hao hao majambazi huhonga wakaachiwa?? Nasema, kwa kuwa majambazi hujibu kwa moto, nao wapelekewe moto huko huko. Hongereni polisi kwa kazi njema
 
Asant mkuu

Nashukuru mkuu kwa kunielewa. Kuna watu humu JF kazi yao ni kupinga kila kitu tu. Nadhani hawajawahi kufikwa na mkasa wa kuvamiwa na majambazi. Waliowahi kufikwa au kuona live kisa cha majambazi wenye silaha, hawaogopi kuiomba serekali kibali cha kuwatoa ngozi live majambazi angalao wasikie hao majambazi tu wakipiga yowe ya kuomba msaada
 
Hao ni tundu lisu
 
Nadhani maishani mwako hujawahi kusikia neno kusingiziwa . Wapo pia watu waliwahi kufananishwa kwa bahati mbaya kimakosa (mistaken identity) hujawahi kuwasikia?
Watu kama hao serikali yao ipo wapi?
 
Mkuu;
Nadhani hiyo yako ni thread nyingine tofauti na huu mjadala. Kufananishwa kimakosa na kujibizana isasi na polisi wapi na wapi??

Kwamba mtu anakuwa katoka buchami na panga halafu polisi wakampiga risasi au?? Yaani unamaana polisi wampige risasi mtu aliyekuwa njiani? Kila mara likitokea hilo, huwa marehemu analipwa. Peleka vielelezo vyako mahakamani utalipwa.

Tunazungumzia majambazi yenye silaha kuuliwa na polisi baada ya kukataa kutiii sio waliopigwa risasi kwa false identity.
 
Mkuu, kujihami ni ruksa. Kwa mfano, jambazi likivamia kwenu, kama una uwezo wa kumwua, ua tu, na hakuna atakayekulaumu.

Tofautisha kat ya kujihami na kuchukua sheria mkonon
 
Habari za siku mbaya...pangilia hoja vizuri, kichwa cha habari hakiendani na kilicomo ndani
Umeelewa??Ana hoja ya msingi sana sasa kama hatuwezi kujibu swali lake basi tukae kimya then watakaoweza watajibu ila kupangilia vzr sio kila mtu anaweza kufanya hivyo by the way haujampeleka shule.
 
Swali ni kwamba; Je, hao majambazi wataenda likizo au? Ili kuwe na fair play hapo kusikwe na upande unao wagandamiza wengine hapo? Jambazi haliji kwako kucheza drafti bali ni uhai wako na au malizako. Umewahi vamiwa na jambazi??
Chukulia mfano; Umevamiwa nyumbani kwako, mbele ya mkeo na watoto. Kama kuna msichana kati yenu, abakwe mbele yako halafu wambake mkeo, halafu wakulazimishe uwape hela ulizouza mahindi siku hiyo.
Hapo wewe waona kuwa kuna haki ya kuishi?? Imetokea wala sio hadithi. Nadhani kama ungesha patwa na msiba ka huu, wala usingeli kuja hapa JF na kusema, polisi wasiwauwe hao majambazi.
Hivi wajua kwamba kuna wakati hao hao majambazi huhonga wakaachiwa?? Nasema, kwa kuwa majambazi hujibu kwa moto, nao wapelekewe moto huko huko. Hongereni polisi kwa kazi njema

Kwa maelezo yako (wino mwekundu) hata hao wahalifu waliotuhumiwa wasingejibizana na polisi kwa risasi wangeuwawa tu?
 
Wala sina haja ya kukujibu kwa sababu tiyari ulisha amua kuwa polisi ni wauaji. Nikuulize swali; Je, inamaana hakuna majambazi yanayofikishwa mahakamani?? Kama wapo, Je, ni wote hufungwa?? Nawajua waliokwenda mahakamani na wakashinda kesi ya wazi kabisa na baada ya kutoka yakaiba wiki ile ile silaha. Tuseme tatizo liko wapi hapo??
 
Nakupongeza kwa jitihada yako kujitahidi kujibu/kunielewesha hadi hapa ila tuweke kumbukumbu sawa sikusema wala sikuwa na nia ya kumaanisha haya hapa chini:

"Wala sina haja ya kukujibu kwa sababu tiyari ulisha amua kuwa polisi ni wauaji."
 
Umeelewa??Ana hoja ya msingi sana sasa kama hatuwezi kujibu swali lake basi tukae kimya then watakaoweza watajibu ila kupangilia vzr sio kila mtu anaweza kufanya hivyo by the way haujampeleka shule.
Mbona kama unakurupuka mkuu..unajua mwanzo alikuwa ameandika nini?? baada ya kumwambia hivyo ndio akajirekebisha akaandika vyema upya sasa we unakuja kunishushia mapovu yako hapa!! Pole sana
 
Back
Top Bottom