Msaada wa Kisheria: Kaachishwa kazi bila taratibu na sheria za kazi kufuatwa

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Wadau naomba tusaidiane katika ili,nina shangazi yangu mdogo tu 24 ameachishwa kazi bila kufanyiwa haya na mwajiri wake kama taratibu na sheria za kazi . Shangazi ni mwalimu katika shule ya private,jana ameachishwa kazi na meneja wa shule bila mwajiri kufanya yafuatayo.
Barua ya onyo
Kumlipa stahiki zake mfano mshahara wa mwezi na likizo
Kumpa barua au cheti cha kuachishwa kazi
Sababu za kuvunja au kustishwa ajira
Hela za usafiri wa kurudi kwao Iringa na vitu vyake na mtoto wake
Malipo yake ya NSSF mpaka leo yalikua bado hayajapelekwa
Sasa wadau naombeni msaada ni nini lakufanya hapa
 
Aende kwenye baraza la usuluhishi
 
Mkuu ni shule gani hiyo weka mambo wazi maana waajiri wamashule wamezidi kuwanyanyasa walimu wa kike. Tupia jina la shule
 
Afike CMA (commission for mediation and arbitration) iliyo karibu yake, pale atapewa CMA form no 7 then atajaza na pale kwenye course of action aweke tick kwenye "unfair termination".
Kuhusu maombi aweke:
Compansation of 18 months salary,
Severance pay
Fare-3txdistancex2000
Leave (kama hakuchukua)
Certificate of service

Na mkazo zaidi amuone mwanasheria aliye karibu yake.
 
Maswali yangu ni haya kabla sijakushauri...

Huyo shangazi yako alipoajiriwa alifata taratibu zote za kisheria za kuajiriwa kama ku-sign mikataba na kadhalika au alichukuliwa kama kibarua?
Sababu halisi iliyopelekea kuachishwa kazi ni ipi kwani ni vigumu mtu kukuachisha kazi bila sababu ya msingi..!
 
amefuata taratibu zote na kuachishwa kazi wamemwambia eti wamepata walimu wengine
 
Back
Top Bottom