Msaada wa kisheria; Juu ya utamaduni wa wananchi kujichukulia Sheria mkononi

kilanio

JF-Expert Member
May 30, 2015
221
69
Habarin Wakuu,Naomba kwanza kulaani dhidi ya baaadh ya jamii ya watanzania ambao tumezidi kua na tabia ya kuchukua sheria mikononi na kuua watu tukiwatuhumu kua ni majambazi,wezi,wagoni n.k...
Sielewi huu utamaduni tuliutoa wapi na kwanini watu wa kizazi cha miaka ya hivi karibuni tumekosa hofu ya Mungu na kugeuka kama wanyama kwa kuua binadamu wenzetu,na mifano mikuu miwili ambayo tulipoteza watanzania wenzetu(kifo cha marehem bondia thomas mashalli r.I.p aliepigiwa kelele za mwizi na kuuawa na mwananchi kule kimara-Dsm na vifo vya wale watafiti waliouawa na wananchi kule Dodoma kwa madai kua walituhumiwa kua ni wanyonya damu r.I.p, Hii ni mifano midogo sana ambayo tumepoteza watanzania wengi ambao hawana hatia ) nb na hata kama wangekua na hatia bado sheria haijaruhusu kuua hadharani...

INASIKITISHA SANA....

SWALI LANGU KWA WANATAALUMA WA SHERIA
.

, JE INAPOTOKEA WATU WAMEMTUHUM MTU ALIKUA ANA attempt KUIBA NA WANANCHI WAKACHUKUA SHERIA MKONONI NA KUMPIGA HADI KUTAKA KUMUUA ILA AKAPONA,NAFASI YA SHERIA IKOJE HUYU MTUHUMIWA ATAKUA NA HAKI YA KUWASHITAK WANANCHI AMA WANANCHI AMBAO WALICHUKUA SHERIA MKONONI WATAKUA NA HAKI YA KWENDA KUMSHITAK HUYO MTUHUMIWA MAHAKAMANI..? AHSANTENI..

"SAY NO TO MOBB JUSTICE."
 
Pole mara 3. Moja kama hujawahi ibiwa na hawa watu wanaosadikiwa ni wezi
Pole ya pili ni kama hujawahi kabwa tapeliwa na kuporwa vitu vya muhimu hadi wengine wanafikia kubaka dada au mam zetu.
Pole ya tatu kama hujaanza kujitegemea na hujajua uchungu wa kupotelewa na vitu wakati wa ukata wa kulimia meno. Kingine serikali kama imezidiwa kesi kwani unaenda shitaki kituo cha polisi anakuja ndugu anamtoa mtoto anakuja kuwaibia tena, au unajisikiaje mtoto wako anatoka shule anabakwa na jamaa ambalo lipo kijiweni limepora pesa,simu na kununua bando na kuangalia pono na kuja kubaka au mlawiti kijana wako.
Sheria na haki ya kweli utaipata ukiwekwa kwenye jumba la milele
 
Mkuu nimekupata shukrani,ila mi nimejikita zaid kwenye mifano ambayo hutokea MTU kusingiziwa kua mwiz bila kua na hatia hyo na kupigwa hadi kufa ama kupata majeraha makali,unakumbuka Kifo cha Bondia Thomas Mashalli mwaka Jana,? Ama wale watafiti waliouawa Dodoma ?
 
Thomas Mashali alienda kwenye ugomvi kuitiwa mwizi ni kutokana na aliyekuwa anakabiliana nae kumshindwa mashali ni mkorofi ndio mana alikuwa haivi hata na baba yake mzazi.ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga.
 
Pole mara 3. Moja kama hujawahi ibiwa na hawa watu wanaosadikiwa ni wezi
Pole ya pili ni kama hujawahi kabwa tapeliwa na kuporwa vitu vya muhimu hadi wengine wanafikia kubaka dada au mam zetu.
Pole ya tatu kama hujaanza kujitegemea na hujajua uchungu wa kupotelewa na vitu wakati wa ukata wa kulimia meno. Kingine serikali kama imezidiwa kesi kwani unaenda shitaki kituo cha polisi anakuja ndugu anamtoa mtoto anakuja kuwaibia tena, au unajisikiaje mtoto wako anatoka shule anabakwa na jamaa ambalo lipo kijiweni limepora pesa,simu na kununua bando na kuangalia pono na kuja kubaka au mlawiti kijana wako.
Sheria na haki ya kweli utaipata ukiwekwa kwenye jumba la milele

Uchukuaji wa sheria mikononi umetokana na serilali yenyewe kutengeneza mazingira ya uchukuaji sheria mikononi.

Mifano:=

(1). Mhalifu anakuvamia kwako, unapeleka report police, police wanajivuuta kwenda kumkabili mhalifu..
Mwisho unaona huyo mhalifu na police ni kitu kimoja tu.
(2). Wewe ni mkulima umelima mazao yako shambani na yamekubali sana. Anakuja mfugaji anaingiza ng'ombe zake kwenye shamba, wanaharibu mpaka inakua total loss. Unamlalamikia mfugaji, anakwambia kuwa "unataka nauli ili uwahi kufika police??"....
Unapeleka report police, ukifika tu wewe mkulima ndio unawekwa ndani kwa 'kosa' la 'kumuonea' mfugaji...!!!
Ukienda mahakamani, hakimu anageuka kuwa ni 'wakili' wa utetezi wa mfugaji aliyeharibu mazao yako.
(3). Unapeleka kesi yako ofisi za serikali (kata, tarafa au wilaya) yako dhidi ya wafugaji wakorofi, unajibiwa kuwa wameshamuonya mfugaji huyo na kumwambia kuwa awe muungwana na wewe na mfugaji mnatakiwa kuishi kwa amani. Hivyo swala lako 'limeshashughulikiwa' na limekwisha...!!

Mifano hii mitatu tu, ungekua wewe ungefanyaje...????
 
Thomas Mashali alienda kwenye ugomvi kuitiwa mwizi ni kutokana na aliyekuwa anakabiliana nae kumshindwa mashali ni mkorofi ndio mana alikuwa haivi hata na baba yake mzazi.ukiishi kwa upanga utakufa kwa upanga.
Sawa tuachane na yote hayo,Je Sheria ipi ime justify kuua katika Sheria za Nchi yetu ama sheria ipi ambayo Mungu alitupa mamlaka kuua?bado ni tatizo katika jamii yetu ya kitanzania.
 
Kwa Mfano jitu ni lijizi na linajulikana ni lijizi police likipelekwa wanaliombea msamaha likitoka linaiba tena jitu kama hili lifanyajwe? Kama sheria zilizowekwa zifatwe zinapindishwa?
Pia myb niulize tu ushawahi kuona watu wameuwa mwizi kisha polic wakaja kukamata waliouwa mwizi?
pili mara ngapi jeshi la police linakama watu hai lakini wanakulakibano au wanafia mikononi mwao unajifunza nini endapo jeahi lenyewe halina usawa?
mkimkamata mwizi mkapiga mkiita difenda wanauliza kwanini hamjammaliza kabisa?
 
Sawa tuachane na yote hayo,Je Sheria ipi ime justify kuua katika Sheria za Nchi yetu ama sheria ipi ambayo Mungu alitupa mamlaka kuua?bado ni tatizo katika jamii yetu ya kitanzania.

Yaani wewe hauko tofauti sana na police na viongozi wa serikali.
Katika mifano hiyo mitatu, ni nani aliyeanza kuchukua sheria mikononi...?? Wewe uliyeshambuliwa, au wahalifu waliokushambulia...??
Hivi sheria za Tanzania zinaruhusu mwizi kukuibia, mfugaji kukuhujumu mazao yako, n.k...?? Mbona hujawahi kuuliza hilo...??
Kwa maana hiyo wewe uliyeshambuliwa na wahalifu, ukijitetea tu basi wewe ndio 'mhalifu'...
Yaani unachosema ni kuwa ukishambuliwa na wahalifu inabidi uwe mpole tu ili usionekane mhalifu mbele ya police na mbele ya serikali...!!!!
Haki ingekuwa inatendela sawa sawa, hakuna hata mtu mmoja angechukua sheria mikononi....
Ni baada tu ya kukwama kwenye kupata haki zao, ndio watu wanaamua kujichukulia sheria mikononi.
 
Habarin Wakuu,Naomba kwanza kulaani dhidi ya baaadh ya jamii ya watanzania ambao tumezidi kua na tabia ya kuchukua sheria mikononi na kuua watu tukiwatuhumu kua ni majambazi,wezi,wagoni n.k...
Sielewi huu utamaduni tuliutoa wapi na kwanini watu wa kizazi cha miaka ya hivi karibuni tumekosa hofu ya Mungu na kugeuka kama wanyama kwa kuua binadamu wenzetu,na mifano mikuu miwili ambayo tulipoteza watanzania wenzetu(kifo cha marehem bondia thomas mashalli r.I.p aliepigiwa kelele za mwizi na kuuawa na mwananchi kule kimara-Dsm na vifo vya wale watafiti waliouawa na wananchi kule Dodoma kwa madai kua walituhumiwa kua ni wanyonya damu r.I.p, Hii ni mifano midogo sana ambayo tumepoteza watanzania wengi ambao hawana hatia ) nb na hata kama wangekua na hatia bado sheria haijaruhusu kuua hadharani...

INASIKITISHA SANA....

SWALI LANGU KWA WANATAALUMA WA SHERIA
.

, JE INAPOTOKEA WATU WAMEMTUHUM MTU ALIKUA ANA attempt KUIBA NA WANANCHI WAKACHUKUA SHERIA MKONONI NA KUMPIGA HADI KUTAKA KUMUUA ILA AKAPONA,NAFASI YA SHERIA IKOJE HUYU MTUHUMIWA ATAKUA NA HAKI YA KUWASHITAK WANANCHI AMA WANANCHI AMBAO WALICHUKUA SHERIA MKONONI WATAKUA NA HAKI YA KWENDA KUMSHITAK HUYO MTUHUMIWA MAHAKAMANI..? AHSANTENI..

"SAY NO TO MOBB JUSTICE."
Kama unaona wanaonewa pita jipendekeze upite kwenye anga zao utatuletea maamuzi mazuri hapa JF
 
Yaani wewe hauko tofauti sana na police na viongozi wa serikali.
Katika mifano hiyo mitatu, ni nani aliyeanza kuchukua sheria mikononi...?? Wewe uliyeshambuliwa, au wahalifu waliokushambulia...??
Hivi sheria za Tanzania zinaruhusu mwizi kukuibia, mfugaji kukuhujumu mazao yako, n.k...?? Mbona hujawahi kuuliza hilo...??
Kwa maana hiyo wewe uliyeshambuliwa na wahalifu, ukijitetea tu basi wewe ndio 'mhalifu'...
Yaani unachosema ni kuwa ukishambuliwa na wahalifu inabidi uwe mpole tu ili usionekane mhalifu mbele ya police na mbele ya serikali...!!!!
Haki ingekuwa inatendela sawa sawa, hakuna hata mtu mmoja angechukua sheria mikononi....
Ni baada tu ya kukwama kwenye kupata haki zao, ndio watu wanaamua kujichukulia sheria mikononi.
Mkuu nadhani tumepishana kidogo,maana yangu ni kwamba Huu uchukuaji sheria mikononi una athari mbaya katika jamii kwa maana kuna wengine hu uawa si kwasabab ni wezi bali chuki,maana sasa imefikia mtu mkipisha kauli kidogo tu,mtu akikuitia mwizi basi ujue mwisho wako ni hapo MFANO mzuri alivyouawa Marehem bondia thomas Mashalli je yeye alikua ni mwizi?si chuki tu za watu,hii ni HAKI?kipindi nasoma chuo kikuu flani nimeshuhudia vifo vya watu zaidi ya 3 wakiuawa na wanachi baada tu ya wapenzi wao wa kike kuwaitia "Mwizi", je hii ni Sawa,tunauhakika gani asilimia 100 wanaouwawa mitaani ni wezi?
 
Serikali isingetengeneza mazingira niliyoyaandika hapo juu... hata uite mtu mwizi... kusingekua na raia yeyote anayechukua sheria mikononi.
Sasa, serikali na vyombo vyake vya dola, vimetengeneza mazingira hayo, halafu wanalaumiwa raia...!!!
Kama kawaida ya nchi yetu hii, raia mwema ndio 'mhalifu'...!!!!
 
Halafu hujajibu swali langu nililouliza kuwa raia mwema na wahalifu, kwa maoni yako wewee, ni nani anayeanza kuchukua sheria mikononi?
Mfano, jambazi anakuvamia nyumbani kwako usiku, je jambazi huyo yuko sahihi kisheria za Tanzania??
Na kama amevunja sheria, kwa nini vyombo husika havianzi na yeye huyo jambazi, badala yake vyombo hivyo vinakushambulia wewe raia mwema unayejitetea??
Jibu hapa.....
 
Ni kweli Mkuu Rushwa imeleta yote haya.so Sad
 
Hakuna Sheria inayoruhusu jambazi kufanya uhalifu na kwa MFANO wako huo RAIA nitakua sahihi maana katika mfano huu,nitakua natumia kanuni ya self defence maana bila hvyo majambazi wanaweza kukudhuru,hop nimejibu Mkuu
 
Ni kweli Mkuu Rushwa imeleta yote haya.so Sad

Serikali itoe haki, na almost instantly, hakutakuwa na raia wema wanaochukua sheria mikononi.
Lakini kama kawaida, serikali imefumba macho...... raia wema wananyanyaswa kama vile ni wakimbizi kwenye nchi yao.
 
Back
Top Bottom