Msaada wa kisaikolojia

Msaada wa kisaikolojia

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
360,527
Reaction score
830,085
Habari za siku mbili tatu na poleni kwa msiba wa Bw. Mbele na wapendwa wetu wengine, ni jambo la kuhuzunisha sana.

Nimesoma ujumbe wa Bush na kuona kwamba anahitaji faraja na msaada wa KISAIKOLOJIA, tukimwacha hivyo haitakuwa sawa.

Mtu anapopatwa na msiba au jambo kubwa la kushtua anapitia hatua kadhaa ikiwemo:
1. Mshtuko (shock) wengine wanaweza kuzirai hata kupoteza maisha;
2. Kukataa (denial), "Sio kweli, wamekosea, sio yeye, amelala tu ataamka)
3. Hasira (anga), why me? Km ni VVU hapa mtu huambukiza wengine kwa makusudi (tufe wengi)
4. Woga (nina VVU nitakufa, fulani nitaishije bila yy)
5. Kujitenga (kujinyanyapaa) (hataki kuchangamana akidhaini wanamesema au wanamcheka)
6. Kubembeleza (bargaining) (Mungu ukimrudisha au ukiniepusha na hilo nita...) Hapa wengi hukimbilia kwa watoa faraja kama za kiroho
7. Kukubali hali au kuishi kwa matumani. Hapa mhusika anakubali kwamba yamekuwa na hakuna jinsi zaidi ya kukubali na kuendelea na maisha.

Kauli za mdogo na rafiki yangu Bush, "Bora niache kazi" na nyinginezo zinaaahiria kwamba yupo kwenye hatua mojawapo kati ya hizo.

Kuwa kwenye hatua ya kwanza hadi ya tano kimaweza kuleta madhara kwa mfusika au mtu/watu wengine.

Jukumu la mtaalamu ni kumsaidia mhusika kuvuka kutoka hatua moja hadi nyingine mpaka kuishi kwa matumaini.

Japo nitaongea na Bush, nashauri nyie MAAFISA UTAWALA, wenye dhamana ya ustawi wa wale mnaotuongoza mwendelee na juhudi za kumsaidia mwenzetu na sote tunaohitaji msaada wa kitaalamu wa kuvuka katika vipindi vya "GREIFING" au majonzi.

Kwa yeyote atakayehitaji msaada tuwasiliane nomwongoze kuhusu upatikaji wa huduma hiyo.

Nipo mtaani nashangashangaa maisha.
 
Hizi nchi zetu zilizokaribiana na kuzimu hazitambui kabisa kwamba tiba ya kisaikolojia ni tiba muhimu kama tiba nyingine. Wagonjwa wa kisaikolojia hawatambuliwi kama wagonjwa na hata kunga za utawala na mahakama zetu hazitambui hayo. This is Africa my friend.
 
Kwasisi tunaoteseka na puli
You cannot solve a problem by the same method you used to create it in the first place. Notice: ^you created your own problem^ and you need a solution which is clearly beyond you 🙂
 
Mtaletewa barakoa nyingine ambazo ndizo zenye matatizo, Mimi ni Kiongozi wenu ninajua mengi, ukitaka kuvaa barakoa kavae zilizotengenezwa na Wizara ya Afya, DSM wanatengeneza barakoa, ukishindwa shona yako mwenyewe, kachukue likitambaa hata kama ni kanga likunje hata mara 5”- Bush.

Sasa hiyo mikunjo mara tano si inaweza kumnyima mtu pumzi.
 
Hizi nchi zetu zilizokaribiana na kuzimu hazitambui kabisa kwamba tiba ya kisaikolojia ni tiba muhimu kama tiba nyingine. Wagonjwa wa kisaikolojia hawatambuliwi kama wagonjwa na hata kunga za utawala na mahakama zetu hazitambui hayo. This is Africa my friend
Sasa mtu kama Bush anayejidai anajua kila kitu, utampa ushauri gani?
 
Mtaletewa barakoa nyingine ambazo ndizo zenye matatizo, Mimi ni Kiongozi wenu ninajua mengi, ukitaka kuvaa barakoa kavae zilizotengenezwa na Wizara ya Afya, DSM wanatengeneza barakoa, ukishindwa shona yako mwenyewe, kachukue likitambaa hata kama ni kanga likunje hata mara 5”- Bush.

Sasa hiyo mikunjo mara tano si inaweza kumnyima mtu pumzi.
 
Back
Top Bottom