Kwanza pole, ili ukweli huu ukuingie.
.
Mwanamke mpaka akuache lazima kuna sehemu ulianza kutetereka na akakuvumilia mpaka sasa we unaona ghafla lakini kamwe sio ghafla. Ulipoanza story na kusema 'kwangu alikua rafiki, mshkaji na kama ndugu' nikajua tu umeachika. Sababu mwanamke yoyote hawezi kuwa na mahusiano au kudumu na mtu amchukuliaye kama rafiki, mshkaji na ndugu na akiwa basi hayatakua mahusiano matamu.
.
Okay, limeshatokea nini cha kufanya?
Cha kwanza futa namba yake, kata mawasiliano naye, USIMTAFUTE kutaka kujua chanzo cha break up au amekula nini leo, mwache hata huyo aliyenae saivi akitetereka atakutafuta tu wewe. Pata muda wa kupoza moyo. Ila jitahidi hayo maumivu yasikuendeshe au watu (hasa huyo mdada) kuona kuna kitu kinakutatiza. Usitafute demu wa kulipizia kuachwa ila tafuta mwanamke kwa lengo lako..
.
Seriously, mpotezee futa kila kitu chake, hata kama ni ngumu vipi mana tayari amekuonesha alivyo, je ungependa uende naye kwenye ndoa baada ya kukuonesha alivyo?