Msaada wa kimawazo unahitajika

Singasinga

JF-Expert Member
Aug 27, 2011
2,649
3,162
Habari wakuu

Kuna mama mmoja hapa jirani ana kijana wake wa kiume wa miaka 18,lakini changamoto ni kuwa kijana hataki shule,kajiingiza kwenye makundi kila mara kesi zinaletwa nyumbani
Na ndo mtoto wa pekee wa kiume katika uzazi wake.

Kiukweli inamuuma sana na kibaya zaidi ni single mother
Je afanye nini ili huyu mtoto wake arudi kwenye standard

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angemhamisha eneo hilo ili aepukane na makini. Kama kuna bibi au uncle kijijini ni vizuri angepelekwa huko kwanza
 
Mara nyingi hawa mama zetu hujimwambafai na kujifanya wanaweza kulea na kukuza mtoto peke yake kwa vile ana vijisenti! Sasa acha aone umuhimu wa malezi ya baba!
 
Kijana ashatimiza miaka 18 ivo kesi sio jukumu la mzazi tena the man will be responsible for his actions

Makundi yana mda wake ni stage tu anapitia mtoto ivo ataacha baada ya mda

Mwambie Aweke tu akiba asipoteze pesa zake kwa sasa kijana kachagua peer group na always zina nguvu sana kushinda hata mzazi
 
Kwa hiyo amuache tu aishi maisha alochagua
Yeye awe ni kumpikia basi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wakuu

Kuna mama mmoja hapa jirani ana kijana wake wa kiume wa miaka 18,lakini changamoto ni kuwa kijana hataki shule,kajiingiza kwenye makundi kila mara kesi zinaletwa nyumbani
Na ndo mtoto wa pekee wa kiume katika uzazi wake.

Kiukweli inamuuma sana na kibaya zaidi ni single mother
Je afanye nini ili huyu mtoto wake arudi kwenye standard

Sent using Jamii Forums mobile app
1. Yaani mama alikua wapi mpaka anafika 18 ndio anashtuka?

2. Mtoto anahitaji ushauri nasihi

3. Mtoto abadilishiwe mazingira
 
Mara nyingi hawa mama zetu hujimwambafai na kujifanya wanaweza kulea na kukuza mtoto peke yake kwa vile ana vijisenti! Sasa acha aone umuhimu wa malezi ya baba!
Kwahiyo wanaolelewa na baba zao wote wamenyooka eti???

Landlord wangu ana mtoto wa miaka 12, anatukanana na baba yake as if ni mtu mzima mwenzie, anaiba, kumkuta nyumbani ni nadra, kazi yake kuzurura mtaa kwa mtaa, shule akitaka aende na asipotaka asiende, watoto anao-hangout nao ni wale wa mtaani kabisa. Ukikutana nae huwezi amini anatokea kwenye family background anayotokea, ni zaidi ya chokoraa.

Swala la mtoto kuwa mkorofi ni matokeo ya uzembe wa mzazi iwe baba au mama. Wazazi wengi huzani kumuendekeza mtoto ndo kumpenda na matokeo yake ndo kama hayo.

BACK TO MTOA MADA....
Waswahili waliposema "Samaki mkunje angali mbichi." hawakua wajinga. Mbona kachelewa sana kumuadabisha mwanae??Siku zote huyo mama alikuwa wapi mpaka mwanae afikie alipofikia??

Mtoto anafundishwa tabia nzuri akiwa mdogo sio akiwa 18 kipindi ambacho hata kisheria anahesabika kama mtu mzima.

Anyway, aanze kwa kuongea nae, ajaribu kuelewa kwanini mwanae anafanya anayofanya na yeye amueleweshe kwanini ha-approve. Pili asiendelee kumuendekeza, aangalie benefits zote huyo mtoto anazopata kwake na azisitishe ikiwa hatomsikiliza. Na kama inawezekana amhamishe mbali na mazingira/washkaji aliowazoea.
 
Back
Top Bottom