Msaada wa kimawazo ndugu zangu.

Meridah Tough

Senior Member
Nov 27, 2017
136
363
Wakuu habari zenu?
Nakuja tena mbele yenu ndugu zangu, mara nyingi ninapopatwa na matatizo naona jf ndio mahala pa kuweza kuongea kwa uwazi na kupata ushauri hata ule mchungu ndugu zangu.

Niliwahi kuwa na mpenzi ambaye tulikutana kipindi tunasoma sekondari, kiukweli alinijali sana na kunipenda sana hata nikakutana na baadhi ya ndugu zake. Mara kadhaa alitaka kujitambulisha nyumbani lakini binafsi niliona muda bado. Kutokana na upendo wake kwangu hata mimi nilijikuta nikimpenda sana.
Tuliishi katika hali ya ugirlfriend na uboyfriend kwa miaka 3. Miaka miwili ikiwa ni furaha na amani lakini mwaka wa tatu niliumwa kwa mwaka mzima na sikupaswa kutembea kabisa lakini alikua nami bega kwa bega.
Baada ya miaka 3 mwenzangu alikwaruzana na kaka yangu ambaye naweza kusema alikua rafiki yake.
Baada ya ugomvi huo mahusiano yetu yalianza kutetereka. Alianza kunikwepa na hata simu zangu ilikua ngumu kupokea.
Nilichukua jukumu la kumuuliza mwenzangu tatizo liko wapi ili turekebishe lakini hakuwa tayari kuniambia chochote. Mwisho aliamua kuniacha. Sikua na jinsi.
Baada ya mwaka, huku bado nikiwa karibu na familia yake, kusalimiana na kusaidiana hapa na pale, nikakutana na ex wangu.
Tukarudisha tena mawasiliano kama marafiki wa kawaida. Aliniambia pia bado maisha yake ya mahusiano hayana dira. Bado ana wanawake anaodate nao for fun.
Baada ya siku kadhaa mwenzangu huyu akaamua kuniomba kurudiana nami kwa madai kuwa anaomba nami niwe katika list ya wanawake zake.
Jambo hilo nililifikiria kwa siku moja na siku ya pili nikamjibu kuwa siwezi kuishi kwenye mahusiano yasiyo na dira, kuna magonjwa, magomvi, kutoendelea kiuchumi nk hivyo ni kheri aendelee na hao watu wake ila mimi nibaki kuwa rafiki.
Sasa hapa ndipo vita ilipoanza. Amenichukia na hataki hata kunisikia. Najiuliza kosa langu liko wapi!
Nimepata mawazo sana na nasikitika sana. Ndugu zangu wenye busara, je swala hili napaswa kuhandle vipi?
 
Kukuchukia leo inakuumiza na akati hapo nyuma mlikuwa wapenzi mkaachana??? Na wewe unataka akusikie ili akupe nn ilihali ushamkatalia au hujui unataka nini ktk maisha yako
 
Mbona hujamalizia? Na yule uliekuwa nae kwa muda wa miaka hiyo mitatu vp?

"ᴬ ᵍᵒᵒᵈ ᵖˡᵃⁿ ᵛⁱᵒˡᵉⁿᵗˡʸ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵒʷ ⁱˢ ᵇᵉᵗᵗᵉʳ ᵗʰᵃⁿ ᵃ ᵖᵉʳᶠᵉᶜᵗ ᵖˡᵃⁿ ᵉˣᵉᶜᵘᵗᵉᵈ ⁿᵉˣᵗ ʷᵉᵉᵏ"
 
Kwanza hana adabu na ukikutana naye leo mwambie huna adabu kabisa.
Mwanaume anakuambia vip mrudiane akikuhakikishia kuwa wapo wenzako tena sio wake zake ila malaya zake?
Mwambie huna dira na mimi wewe na chapa lapa, kama alikuacha mara ya kwanza kwa mambo ya kijinga basi jipeleke tena ukaachwe tena kwa mambo yale yale ya kijinga kama alivyokuambia uwe naye wakati ana darasa zima la wanawake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi wanawake mnakumbukaga nini hasa kwamabwana wazamani waliowaacha? [KITOMBO MLICHOKUWA MNAPEWA AU HUWA MNAYATAMANI MAUMIVU MLIYOPEWA KWAHIYO MNAKUWA MNAYAHITAJI KWAMARA NYINGINE TENA?] Embu mtuambie basi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu habari zenu?
Nakuja tena mbele yenu ndugu zangu, mara nyingi ninapopatwa na matatizo naona jf ndio mahala pa kuweza kuongea kwa uwazi na kupata ushauri hata ule mchungu ndugu zangu.

Niliwahi kuwa na mpenzi ambaye tulikutana kipindi tunasoma sekondari, kiukweli alinijali sana na kunipenda sana hata nikakutana na baadhi ya ndugu zake. Mara kadhaa alitaka kujitambulisha nyumbani lakini binafsi niliona muda bado. Kutokana na upendo wake kwangu hata mimi nilijikuta nikimpenda sana.
Tuliishi katika hali ya ugirlfriend na uboyfriend kwa miaka 3. Miaka miwili ikiwa ni furaha na amani lakini mwaka wa tatu niliumwa kwa mwaka mzima na sikupaswa kutembea kabisa lakini alikua nami bega kwa bega.
Baada ya miaka 3 mwenzangu alikwaruzana na kaka yangu ambaye naweza kusema alikua rafiki yake.
Baada ya ugomvi huo mahusiano yetu yalianza kutetereka. Alianza kunikwepa na hata simu zangu ilikua ngumu kupokea.
Nilichukua jukumu la kumuuliza mwenzangu tatizo liko wapi ili turekebishe lakini hakuwa tayari kuniambia chochote. Mwisho aliamua kuniacha. Sikua na jinsi.
Baada ya mwaka, huku bado nikiwa karibu na familia yake, kusalimiana na kusaidiana hapa na pale, nikakutana na ex wangu.
Tukarudisha tena mawasiliano kama marafiki wa kawaida. Aliniambia pia bado maisha yake ya mahusiano hayana dira. Bado ana wanawake anaodate nao for fun.
Baada ya siku kadhaa mwenzangu huyu akaamua kuniomba kurudiana nami kwa madai kuwa anaomba nami niwe katika list ya wanawake zake.
Jambo hilo nililifikiria kwa siku moja na siku ya pili nikamjibu kuwa siwezi kuishi kwenye mahusiano yasiyo na dira, kuna magonjwa, magomvi, kutoendelea kiuchumi nk hivyo ni kheri aendelee na hao watu wake ila mimi nibaki kuwa rafiki.
Sasa hapa ndipo vita ilipoanza. Amenichukia na hataki hata kunisikia. Najiuliza kosa langu liko wapi!
Nimepata mawazo sana na nasikitika sana. Ndugu zangu wenye busara, je swala hili napaswa kuhandle vipi?
Pole mdada, Duuh! Huyo jamaa mpaka anakuchana live kwamba anao wengine. Na wewe anataka kukuongeza!

Mi ninachojua sisi Wanaume, hata kama tuna lundo la wanawake pembeni, lakini tutasema hatuna hata mmoja kwamba tupo Single.

Kukuambia live, ina maana hajali na hakujali, anakuona wa hivi hivi.

Achana naye huyo, asikuumize kichwa.

Nb: una Miaka mingapi?
Na Huyo jamaa ana Miaka mingapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza hana adabu na ukikutana naye leo mwambie huna adabu kabisa.
Mwanaume anakuambia vip mrudiane akikuhakikishia kuwa wapo wenzako tena sio wake zake ila malaya zake?
Mwambie huna dira na mimi wewe na chapa lapa, kama alikuacha mara ya kwanza kwa mambo ya kijinga basi jipeleke tena ukaachwe tena kwa mambo yale yale ya kijinga kama alivyokuambia uwe naye wakati ana darasa zima la wanawake

Sent using Jamii Forums mobile app
Bidada ndo hajielewi naona... anaumia eti jamaa hataki hata kumskia, kwan mtoa mada bado anamtaka jamaa???
 
Back
Top Bottom