Msaada wa haraka please, mke wa mtu anakufa hukuu

Kwanza wewe mwanamke ni pepo kabisa.. umeolewa na bado unamfanyia mumeo hiv...?
Achwa yakukute tu... acha yakukute.. wanawake kama nyie hamfai kabisa
 
Duh..!
Aliyeelewa atachangia.,mimi hiyo lugha hata sijaielewa labda sababu mimi bado mgeni humu jukwaani
Hahaha

Huyo mjasiriamali inabidi amwone shigongo si haba anaweza kupata Mawazo mazuri sana ya kuimarisha biashara yake na pia atapata suluhu ya mkasa wake
Kha! Alafu nimeskia shigongo ananitafuta kiru! AJE!

Anataka msaada wa nini wakati aliyataka mwenyewe?

BTW uongo hujitenga na ukweli ma mficha maradhi kifo humuumbua, the best way ni kumuambia ukweli mumewe ili asije kuumia huko mbeleni
Aya Street Pastor

haaa!!! yaan hii yote nisome mimi..!!!!
hapana bora niitwe bashite ila sio kusoma kitabu kizima..!!!!
Sawa bashite

Tuanzie kwenye vyeti kwanza kama ni vyake au vya....
Vyeti vipi labda ahahaha

kila ninavyojitahidi kusoma na usingizi ndio unazidi nimeipotezea.

wanawake watauelewa zaidi huu uzi.

naona tu KICHWA PANZI, BISIBISI, MSUMENO, KISODA nilijitahidi kusoma nikajua nitakutana na BASHITE
Stori zangu na za Lara mnasoma page 25 lakini hapa mnaona nyota
Basi sawaaa Mungu anawaonaa

Sasa mki-copy na kupaste basi fanyaneni editing. Unaacha bold text, font size 20 sijui? Inachosha kusoma.
Jaman wengine wanapenda ivyo hawaini maandishi madogo jamaa

Huyo mnunulie conc. Hydrochloric acid 20ml anywe itamsaidia
He unataka afe au?! Shindrwaaaa

Huyu aliforce kuolewa, bado
Hatarious baab!

Basis tena b money mi nalala
Za asbh mpendwaaa

Kwan mkasa unahusu nini
Unamhusu dadako soma vzuri utamwona
 
Nina shogangu kidawa tunamwitaga KICHWA PANZI. Amekwama anataka kujimaliza bila sababu nikamwambia hii kesi ya nyuki pelekea malkia kama sisi kwanini ujiue labda unawahi Mbinguni kufanyaje kuimba kwaya au?! Na mechi za kila siku unamwachia nani labda?!

Basi kichwa panzi akafunguka

KICHWA PANZI:
Money Penny we wangu tu wala sikufichi
Hii michezo ya Yondo sister tuwaachiwe Mama zetu na Mama wakubwa na wadogo akina sisi tuliozaliwa miaka ya 79-82 ni wa akina JLo.

Mume bwana akasafiri kimasomo China kwa miaka miwili kila mwaka anakuja Tz me nipo na watoto

Basi nikaskia shogangu KISODA anajigamba, me nina mume lakini bado ofa za nje nachukuaaaaa tena mume akisafiri ndio kakoseaaaaa

KISODA akajigamba wee nikamwambia basi tumwita Money Penny atuvushe akakataaa. Nikamwambia nipe ubuyu dadalake mama la mama, Lemutus hana shida na wewe anashida na Mange Kimambi tuuu, ila wewe ndo wewe, nikamsifia pale akajaa kichwa

Akanipa maujanja akaniambia kwanza kuna MSUMENO unatafuta pa kuhemea, sumeno la kikenya, kuna BISIBISI ya Kibongooo, kuna PLUG ya kibongooo wote wapo wanatafuta pa kuhemea

Nikamwambia niingize mama niingize front, KISODA akani connect na ma Sponsor hao dadeki, sponsor wana hela safiii afu nyingiii

Nikaonana na MSUMENO tukaongea wee tukapendana wee tukapanga na siku ya ku do. After 2 weeks tuka do na kinga, akanipa laki 3 nikaondoka nikajua nimemaliza cheee! Msumeno sijui alinogewa basi kila siku simu simu kama customer service, oh nataka kukuona and shit, nikaenda round ya pili tukanyooshana nikasepa akawa bado ananigandaa

Nikamuvuzisha majeshi kwa BISIBISI, aisee Mbongo Mbongo sijui Mangi yule maana ni shida anang'ang'ania Mkenya atasubiri miaka 1000
Nikajaribu kumkwepa wapi ila mchaga nomaaa, anatoa hela mpaka nikadhangaa mmachame gani anarusha hela kama DJ KHALID?! Basi nikawa napokea kwakweli kati ya MSUMENO na BISIBISI, anaeongoza kwa kutoa pesa BISIBISI no 1.

Huku mume anapiga simu anatumabhela za familia hizi za pembeni sasa kudadeki naziweka kwenye akaunt, si unanijua mtoto wa Kitanga, Tanga kunani paleee

Nikaenda kumcheki PLUG, kiru! Plug nomer sana, plug ana ma care hatarious, plug anakufungulia mlango wa gari, anakufungia, ukifika anakuchum, mechi usiseme si unajua Wanyakyusa tena, ila huyu mnyakyusa k/nyoko kitandani nikisalimu amri

Basi mume akarudi zake Tz likizo nikatupa namba ya simu ya madhambi yangu, aliporudi shule nikahamia Airtel kufungua simu nina sms za kutosha, Mpesa pending zimerudi, Kha nikaona sio bin sio nikawarukia hewani
Wakazirudisha pesa

Kashehe imenikutia hapa. Wakati mume yupo masomini buana, me nikaenda out na BISIBISI, mmachame masifa hatari, kufika dinner mara whuuuuuuu, goti chini will you marry me tobaaaaaaa! Watu ma selfie na makofi kibao, hapa hapa dar DVD imechezwa Chinese Dragon restauutant
Mh unakataaje kwanza, nikakubali kupunguza attention

Baada ya mwezi mmoja PLUG akaniomba tuonane, me kama kawaida chek noris navua gwanda pete za ndoa tupa kuleee, nikajisogeza tukaenda Tabata Green View Hotel, kula na nini tukazama kwenye mechi, kuamka asbh jamaa sijui ndo ulimbukeni au sielewi ka propose, mmh nikaona hapa sass ni balaa kea mauno gani mpaka niwe proposed in 2 month friendship ya kujiiba?!
Nikakubali with fake smile na mahaba kuridi home pete kwenye sanduku chiniii!

MSUMENO sikuwahi kumwona gadame, akaja akaibuka mwezi wa 6 wakati naendelea kuzipanga karata zangu sawa kati ya PLUG na BISIBISI, naona simu whuuuu! Cri cri cri cri nikapokea najua mume kumbe MSUMENO, tukaongeaa anasema alienda kwao Kenya visa iliisha ilikuwa ghafla na kamata kamata ya serikali akaona aende bila kuaga, appologies kibaaaao nikamwambia uskonde, uko wapi me niko posta njoo basi serena hapo nikiangalia watoto wote wapo shule nikaji stretch mpaka Serena Lunch nene nini, akachukua room, tukapiga uzinduzi mpaka saa 3 usiku nikarudi home
Kesho anataka tenaaaa nikampaaaa
Kila siku anatakaaa nikamwambia mkei usinipande me sio kichongeo cha kuchangamsha dyu dyu ichongeke nimechookaaa
Huku BISIBISI na PLUG nao wapo mwake kama nusu ya Eifl Tower Paris wanawaka sio kidogo oh baby nataka kukuona kwako oh baby nataka kulala kwako me nawadanganya baba mkubwa mkali kwanza hawaamini proposal za nje wanapenda protocals BISIBISI akaniambia niambie lini nilete wazee
PLUG nae wimbo ule ule wa ndoa ndoa ndoa!
Nilipoharibu ni hapa sass baada ya purukushani ya mwaka na miezi 3, KISODA yeye kakomaa kwenye hili game hata anitafuti,
Siku nipo zangu natoka Bank MSUMENO huyooo, eh baby nakuona umependeza mara BISIBISI huyooo, anashangaa mbona nashikwa shikwa kimahabaaa?!
Posta CRDB Azikiwe branch kwa nje nilipaona peusi ghafla, kila mtu anaulizana huyu nani huyu nani Mlinzi akaja akasema naomba mpishe maongezu mbele kwa mbeleee

Tukasogea mpaka parking ya Azikiwe kila mtu anataka explaination, pete niliovaa ya PLUG naulizwa hii pete ya nani, kufekisha nazikia siwezi, watu washaanza kujaaa, wale mabwana wametukakanana me nipo kimya kama dadabyao kumbe bibi yao, huyu anatukana kikenya huyu matusi ya kibongo mara gari hilook, PLUG ananiita we mrembo twende basi mbona umemalizana na bank haujaniambia twende bwana, tobaaaa! Nilihisi moyo umesimama!
Ile nanyanyua mguu niende kwa PLUG nikavutwaaa less wig langu unakwenda wapi we malaya, nikavutwa less wig la kubond likaanza kusogea pembeni noma, akapaki PLUG akaja kunitetea basi ni sheedah haelewi likaja bus la mwananyamala nikanyata wiiiiii mpaka keenye buss dereva ondoa gari plz nakufaaa dereva nashukuru Mungu alimtumia akaondoa gari wale majamaa kugeuka hamna demu sijui iliendeleaje lakini me namba ya simu niliitupa barabarani

Nikakaa miezi michache mbele mume akarudi for good hapa ndo niliona rangi zote duniani

Siku tumetoka zetu out tunarudisha penzi on date night mara PLUG huyooo, enheee nimekutafuta we dada
Mume: we unamtafuta mke wangu kama nani?!
plug: mke?! Kwani we dada umeolewa
Mimi: ndio me mke wa mtu we kaka vepee me sikujui au unataka nikuitie mwizi?!
Plug: we dada si nimelala na wewe akaanza kutaja mahoteli yoooote gadame, mume ananiangalia me nimekaza uso namwambia mume buana vichaa skuhizi ni wengi sana achana nae tuondoke uso mkavu kama hindi la kuchoma

Tukaondoka tumemwacha PLUG anatuangalia

Baada ya miezi 3 mbele tena OMG, kumbe wale mabwana walikutana wakakaaa wakaongeaaa wakawa na plate no ya gari ya mume, tobaa wakamsaka wakapata no yake wakamwita, ndio kumweleza kiiiila kitu Mume haelewi anaona kama movie ya Isidingo isioisha kiruuu, mtoto wa Kitanga nilipatikana nikamkumbuka kuwa Kisoda ni Kisoda hawezi fanana na Kichwa panzi
Mume kuja anauliza kila kitu me nakataaa pete zikowapi kumbe nilishayeyusha kwa sonara muuudaaaa hela zipo benk
Nikapigwaaaa weee me bado usi mkavu si hana prove ni maneno na kapicha kamoja tumepigwa na hotel manager ya proposal nikamwambia ah huyu kama nimesoma nae anapenda kunitania tania hapa aliniita tukaongee basi mume wangu sijafanya haya yote waliosema

Sasa katika pigwa pigwana vipondo visivyoisha toka kwa mume nikamponyokaaa ndio breki ya kwanza kwako Money Penny

Hii kesi ya Kenge lazima nilete kwa Mamba

Nafanyaje Dadangu?! Inawezekanaje mimi mke wa mtu kuposwa mara 2?!

Naomba m comment Msaada plz sio mipasho wala matusi, kama hauna msaada basi acha usi comment plz
unajua kuandika script!
nadhani kanumba angekuwepo ungeuza hii movie kali sana!
kumbe humu JF watu wanaweza sana kuandika Movie, kwa hakika mimi nimeisoma mwanzo mwisho, sikuiwekea maanani kama tukio la kweli, ila nimeiona kama simulizi nzuri sana!
 
Back
Top Bottom