Msaada Wa haraka kunusuru ndoa ya hawa watu

Msaada Wa haraka kunusuru ndoa ya hawa watu

Yale yale ya mkuu Yona Fares Maro,mie ushauri wangu ni naomba kaa karibu na jamaa maana anaweza kuchukua maamuzi mabaya ya kujiuwa.
 
Mwanamke anapitia kipindi kigumu sana.
 
Ww mtoa mada ushapatanisha ndoa ngapi?? Au ndo unataka ujaribu hapo kisa ni ndugu yako ili upate uzoefu.....
Utakula za uso Mzee nani fanya yako ama wapeleke kanisani wakapatanishwe..

Ndugu; sijawahi patanisha bali nimewahi kushauri ndoa kadhaa wakarudi kwenye hari yake ya kawaida

Hawa ndugu sio wakristo ni waislam. Katika kikao hicho mwanamme alikataa kukutana na shekhe kwa hiyo mazungumzo yakabaki kwangu na hao wanandoa.

Lakini pia baada ya mazungumzo nilijaribu kupata ushauri mzuri kutoka kwa shekhe na pia nilimwonesha copy ya taraka alopewa mwanamke na shekhe ndo alisema hii taraka ni batiri coz haina mashahidi
 
Waambie hivi, Watawatesa watoto wao, hayo ni mapito tu na yatapita, wasiuze vitu,ila waishi mbalimbali kwa kipindi fulani, baadae watarudiana tu hasira zikiisha
 
Hapo kila mmoja anatumaini lake la pembeni tayari hivyo huwezi kuwazuia kwa sasa. Badae mambo yakigeuka ndo wataelewana na kurudiana. Acha tu kwa sasa watengane. ILA mke ndo ana balaa zaidi maana usikute hilo Tumaini lake linamdanganya mwisho litamtupia virago Nje. Labda abahatike...
 
Vema watengane kwa kuwa mme tayari ametenda dhambi ya uzinzi hapo hamna ndoa
Vema watengane kwa kuwa mke hakuwa mvumilivu amelipa kisasi kwa kuzini mtu asiye mumewe ndoa hamna hapo
Kila mmoja wao anaye ambaye kampa nafsi yake
Ukilazimisha ndoa hiyo iwepo uwe tayari kupokea chochote hata kifo kwa wao wanawake ni wadhaifu anaweza weka sumu kwenye chakula wakala wote
Ndoa haipo vunja
 
Habari za mchana wana ndugu

Jana usiku nikiwa nimepimzika na mke wangu kipenzi; gafla nilipokea simu kutoka kwa mmoja Wa wanandoa akiniambia kuwa amemua kuachana na mwana ndoa mwezie; na kesho asubuhi (Leo asubuhi) kitakuwa na kikao cha kugawana mali na tunakuomba ufike ukiwa kama mwanafamilia.

Nilichukua muda kutafakari juu ya hili; asubuhi nikajihimu mapema kwa lengo LA kwenda nyumbani kWa wahusika japo tayari mmoja Wa wanandoa ameshaondoka yupo kwa ndugu zake. Kabla sijafanya hivyo ilibidi nimpigie mmoja Wa wanandoa (mwanaume) ili nipate nafasi ya kuonana nae mapema kabla ya kikao hicho nikiwa na lengo la kunusuru kutokuvunjika kwa ndoa hiyo. Nashukuru Mungu niliongea na mwanandoa huyo na akakubari kuonana nae kwa masharti ya kuwahi kufika Nyumbani kwake!

Nikifika eneo hilo; kwanza nikamsifia kwa ujenzi Wa nyumba nzuri na kujuliana habari za Maisha.

Then; tulianza mazungumzo ya kina juu ya matatizo hayo! Lakini ikumbukwe kwa muda wote huo tulikuwa wawili tu! Alinieleza mambo mengi sana yanayomuhusu mke wake. Ikiwemo mke kupishana kimaneno na mkwe wake, mwanamke kuwa na mawasiliano na mpenzi wake Wa zamani, tuhuma za uchawi, lakini kubwa zaidi ni mke kuchelewa kurudi nyumbani Mara kadhaa yeye mume akiwa amslesafiri kikazi na habari hizo kuzipata kwa majirani.

Wakati tukiwa katikati ya mazungumzo; mke akiingia na tukaungana ktk mazungumzo; baadae nilimpa nafasi mwaname kuongea ilionekana kuwa mwanaume ana mwanamke mwingine na amemjengea nyumba na anamezaa nje ya ndoa.

Pia mwanamke amelalamika kuwa anazaidi ya miezi Tisa hajakutana kimwili na Mme wake na kila akihitaji unyumba kutoka kwa Mme wake Mme hataki; wakati mke akiendelea kuongea mume alikuja juu akataka kumpiga mke kwa lengo la kutokutaka mwanamke asiendelee kuongea; bahati nzuri nikadhibiti hari hiyo!

Binafsi niliwasihi na hususani Mme nilimsihi ahairishe maamuzi yake ya kutaka kuuza nyumba na kugawana fedha na Mali zingine; nilimsihi hivyo coz ana watoto wawili ambao watahitaji kuendelea kuishi ktk hiyo nyumba.

Sikutaka kuingilia maamuzi ya Mme kubatilisha maamuzi ya taraka alompa mke wake!

Lakini Mme hataki kabisa mke wake arudi ktk nyumba hiyo hari kadharika mke hataki kuendelea na ndoa pia

Lakini niligundua pia; taraka ilotolewa ikikuwa batiri coz haina mashaidi na sahihi zake na wala haitaji tarehe ya kuachana na sababu za kuachana

Ninakuja kwenu kuomba msaada Wa mawazo nifanyeje kusaidia kuinusuru ndoa hii au kuwapa ushauri utakaowafaa.
Waache waachane la sivyo watauana.
 
Back
Top Bottom