Msaada Wa haraka kunusuru ndoa ya hawa watu

Msaada Wa haraka kunusuru ndoa ya hawa watu

Ngambako

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2013
Posts
315
Reaction score
264
Habari za mchana wana ndugu

Jana usiku nikiwa nimepimzika na mke wangu kipenzi; gafla nilipokea simu kutoka kwa mmoja Wa wanandoa akiniambia kuwa amemua kuachana na mwana ndoa mwezie; na kesho asubuhi (Leo asubuhi) kitakuwa na kikao cha kugawana mali na tunakuomba ufike ukiwa kama mwanafamilia.

Nilichukua muda kutafakari juu ya hili; asubuhi nikajihimu mapema kwa lengo LA kwenda nyumbani kWa wahusika japo tayari mmoja Wa wanandoa ameshaondoka yupo kwa ndugu zake. Kabla sijafanya hivyo ilibidi nimpigie mmoja Wa wanandoa (mwanaume) ili nipate nafasi ya kuonana nae mapema kabla ya kikao hicho nikiwa na lengo la kunusuru kutokuvunjika kwa ndoa hiyo. Nashukuru Mungu niliongea na mwanandoa huyo na akakubari kuonana nae kwa masharti ya kuwahi kufika Nyumbani kwake!

Nikifika eneo hilo; kwanza nikamsifia kwa ujenzi Wa nyumba nzuri na kujuliana habari za Maisha.

Then; tulianza mazungumzo ya kina juu ya matatizo hayo! Lakini ikumbukwe kwa muda wote huo tulikuwa wawili tu! Alinieleza mambo mengi sana yanayomuhusu mke wake. Ikiwemo mke kupishana kimaneno na mkwe wake, mwanamke kuwa na mawasiliano na mpenzi wake Wa zamani, tuhuma za uchawi, lakini kubwa zaidi ni mke kuchelewa kurudi nyumbani Mara kadhaa yeye mume akiwa amslesafiri kikazi na habari hizo kuzipata kwa majirani.

Wakati tukiwa katikati ya mazungumzo; mke akiingia na tukaungana ktk mazungumzo; baadae nilimpa nafasi mwaname kuongea ilionekana kuwa mwanaume ana mwanamke mwingine na amemjengea nyumba na anamezaa nje ya ndoa.

Pia mwanamke amelalamika kuwa anazaidi ya miezi Tisa hajakutana kimwili na Mme wake na kila akihitaji unyumba kutoka kwa Mme wake Mme hataki; wakati mke akiendelea kuongea mume alikuja juu akataka kumpiga mke kwa lengo la kutokutaka mwanamke asiendelee kuongea; bahati nzuri nikadhibiti hari hiyo!

Binafsi niliwasihi na hususani Mme nilimsihi ahairishe maamuzi yake ya kutaka kuuza nyumba na kugawana fedha na Mali zingine; nilimsihi hivyo coz ana watoto wawili ambao watahitaji kuendelea kuishi ktk hiyo nyumba.

Sikutaka kuingilia maamuzi ya Mme kubatilisha maamuzi ya taraka alompa mke wake!

Lakini Mme hataki kabisa mke wake arudi ktk nyumba hiyo hari kadharika mke hataki kuendelea na ndoa pia

Lakini niligundua pia; taraka ilotolewa ikikuwa batiri coz haina mashaidi na sahihi zake na wala haitaji tarehe ya kuachana na sababu za kuachana

Ninakuja kwenu kuomba msaada Wa mawazo nifanyeje kusaidia kuinusuru ndoa hii au kuwapa ushauri utakaowafaa.
 
"Ya Ngoswe, Mwachie Ngoswe! Edwin Semzaba"
"Muungano ni kama koti, kama linakubana, unalivua" Mzee K
 
Msaada wa kiukweli - kweli hapo utatoka ndani ya hiyo nyumba mkuu. Huyo mwanaume ni kama kashashikwa na mwanamke wa nje anamuona mkewe hafai tena na sasa anaona zaidi negatives kuliko mazuri ya mkewe na pia huyo mama nae pengine sababu ya mazonge ya jamaa nae kapata pumziko nje basi tabu tupu!

Ulijaribu kumuuliza jamaa kama ni kweli hajampa mama kibamia kwa miezi 9? Kama ni kweli anategemea mama aendelee kuwa royal tu? Pamoja na kunyimwa haki yake na pia kusikia jamaa ana mwanamke nje na hadi kazaa nae?

Sasa mwambie jamaa yako kama yeye ni mwanaume wa kweli asiuze nyumba. Mwambie abebe begi amwachie mama na watoto nyumba, hivyo ndio wanaume wa kweli hufanyaga maana huwezi jua anaweza kuja kuugulia na kuzikiwa hapo uzeeni. By the way si ameshamjengea kimada nje, abebe begi akaishi kwenye nyumba yake mpya
 
Mhhhh Mbona bado ndiyo kwanza Mwezi wa Kwanza wa 2018 na bado ni mwaka wa Tatu katika utawala wa Awamo ya Tano???
 
washachokana hao.ndo maana wazungu wenzetu ndoa zao za mikataba.waache walivyoamua hivyo hivyo.waachane tu hakuna namna
Vipi swala la watoto?

Mme anasema atachukua watoto watalelewa na bibi yao huku mke anasema watoto watalelewa na yeye na hakuna mtu ataingia kwenye hiyo nyumba kulea watoto au kuishi.

Una mtazamo gani hapa ndugu
 
Hao mwanaume ana ushawishi kutoka nyumba ndogo na mwanamke hajali sbb kashadnganywa na x wake..tatizo ni la mwanaume kwa upande wangu sbb inaonekana alimruhusu huyo mwanamke kumpanda kichwani..mwanamke atakiwi apewe democrasia ndani ya nyumba..na ndio chanzo cha nyumba nyingi sana kuvunjika siku izi.nyumba inataka dicteta awe baba..tofauti na hapo nyumba itakua ya ovyo sana..baba anatakiwa awe anachange ndani ya dkk mbili tu..marekani ndio nchi ambayo inaongoza kwa democrasia baina ya wanandoa/kuhimiza democrasia na ndio nchi inayoongoza kwa devorse kuliko nchi yoyote duniani..mwisho wa siku hamna kitu mwanaume ndio atakae poteza sbb huwa baada ya kumis tunaumia sana moyo..mwishowe kifo.
 
Inasikitisha sana...

Kama wamefikia hapo... Na waachane tu, kila mmoja achukue ustarabu wake...

Cc: mahondaw
 
Huyo mama abaki na nyumba...alee watoto hapo...ipo siku nyumba ndogo itamfukuza..atarudi kwa mke wa ujana wake
 
Vipi swala la watoto?

Mme anasema atachukua watoto watalelewa na bibi yao huku mke anasema watoto watalelewa na yeye na hakuna mtu ataingia kwenye hiyo nyumba kulea watoto au kuishi.

Una mtazamo gani hapa ndugu
kama wamefikisha wote miaka saba.baba ndio anatakiwa awachukue .aondoke na wanae kisheria pia ndie anayeruhusiwa kama hawajafikisha basi watabaki na mama yao mpaka watakapotimiza na gharama za Watoto baba atatikiwa kuwagharamia
 
Una msaada mzuri sana Wa mawazo kwenye hili; mtoto wao kwanza ana miaka 11 na yupo darasa la tano na wa pili ana miaka minne yupo kindergarten
 
Ww mtoa mada ushapatanisha ndoa ngapi?? Au ndo unataka ujaribu hapo kisa ni ndugu yako ili upate uzoefu.....
Utakula za uso Mzee nani fanya yako ama wapeleke kanisani wakapatanishwe..
 
Msaada wa kiukweli - kweli hapo utatoka ndani ya hiyo nyumba mkuu. Huyo mwanaume ni kama kashashikwa na mwanamke wa nje anamuona mkewe hafai tena na sasa anaona zaidi negatives kuliko mazuri ya mkewe na pia huyo mama nae pengine sababu ya mazonge ya jamaa nae kapata pumziko nje basi tabu tupu!

Ulijaribu kumuuliza jamaa kama ni kweli hajampa mama kibamia kwa miezi 9? Kama ni kweli anategemea mama aendelee kuwa royal tu? Pamoja na kunyimwa haki yake na pia kusikia jamaa ana mwanamke nje na hadi kazaa nae?

Sasa mwambie jamaa yako kama yeye ni mwanaume wa kweli asiuze nyumba. Mwambie abebe begi amwachie mama na watoto nyumba, hivyo ndio wanaume wa kweli hufanyaga maana huwezi jua anaweza kuja kuugulia na kuzikiwa hapo uzeeni. By the way si ameshamjengea kimada nje, abebe begi akaishi kwenye nyumba yake mpya

Suala la kumpa kibamia kwa miazi 9 sikumuukiza direct wakati Wa mazungumzo; but mke wakati anaongea aliligusia na kuliongea kwa uchungu sana na ndipo Mme alipopaniki na kutaka kumpiga mke wake. Kwa hari yio nikajua kuna ukweli ndani yake

Bro, umeshauri vizuri sana na ntamweleza jamaa abebe begi lake aende
 
Mambo yao waachie wenyewe ndugu wao si ndio wameamua?? au wewe ndie uliwaambia wafunge ndoa?
 
Back
Top Bottom