Msaada wa Gari yangu Nissani teana 230 JM

hp4510

JF-Expert Member
Jan 16, 2012
6,451
6,325
Wakuu Habari za weekend

Gari yangu Aina ya Nissani teana 230jm inashida zifuatazo ambazo naomba ni share na wadau hapa mnipe mawazo

1. Check engine light iko on

2. Ukitembea umbali flan Gari inazima na kuwaka hapo ni ishu kweli kweli

3. Ikiwa Inatembea inakuwa kama inatetemeka

4. Kwenye Injini kwa chini Kuna moshi unatoka it's like oil au sijui ni kitu gani kinamwagika

Ombi langu wadau ni kupata msaada wa fundi mzuri au kama Kuna mtu alipata shika kama hii kwenye Gari yake basi anijulishe alifanyaje.

2020-10-03 12.40.30.png
 
Wakuu Habari za weekend

Gari yangu Aina ya Nissani teana 230jm inashida zifuatazo ambazo naomba ni share na wadau hapa mnipe mawazo

1. Check engine light iko on...
1. Tatizo la check engine light si la kubashiri, inaweza kuwaka kwa sababu nyingi sana...hapo kafanye diagnosis kwa wataalamu..

2. Hilo tatizo unaloona kitu kama moshi mbona ni rahisi sana kutatua....hicho ni kitu kinachoonekana peleka kwa fundi aangalie huenda ni exhaust inavuja moshi, au huenda ni oil inadondokea kwenye exhaust manifold....Hiyo leakage kama ni oil au moshi, fundi atamaliza tu..
 
Kuna waya za lead zinavujisha voltage , pia baadhi ya plug hazichomi mafuta ndiomana inapeleka mafuta mengi hayachwi vizuri peleka gari wakapime kwenye OBD SCANNER
 
Kuna waya za lead zinavujisha voltage , pia baadhi ya plug hazichomi mafuta ndiomana inapeleka mafuta mengi hayachwi vizuri peleka gari wakapime kwenye OBD SCANNER

Thank you so much
Unaweza kurecomend sehemu gani unaijua nipeleke wenye hiyo ODB SCANNER
 
Pasua kichwa hizo Gari.
Hivi gari ndiyo pasua kichwa au vivywa vyetu ndiyo vimepasuka?

Gari unainunua nzima hujifunzi kujua gari inatataka kutunzwaje, unaendesha gari bila kuifahsmu vizuri, kukiwa na tatizo dogo badala la kuuliza mafundi waliobobea wa gari hizo, wee unauliza watu wa jamii forum. Btother, miongoni mwa wanaokushauri humu wanaishi kwa wazazi wao bado.
 
Naungana na wewe mkuu,, watu wanakatishana tamaa sana na kiufupi hakuna gari mbovu
 
Back
Top Bottom