Msaada wa Gari ya Toyota Wish

jamii01

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
1,982
1,420
Wakuu nahitaji kununua family car japo nilikuwa nikitaka kuchukua kati ya Noah au Toyota wish.

Mwenye uelewa zaidi wa Toyota Wish naomba anijuze uimara,mafuta na spares nisije kupoteza pesa zangu kumbe gari zenyewe michosho.

Noah ni last option japo silipendelei sana..au kama unawazo ya gari zuri ambayo linafaa matumizi ya kifamily naomba unijuze..
 
Yupo jamaa anayo wish mwaka wa tatu hajawahi kuipeleka gereji kwa tatizo zaidi ya kubadili oil, na mishe zake dar arusha. Anasema mafuta pia inakula kidogo saana. Go for wish.
 
Aya magari mabaya sana bora Noah mzee
db400ef9687aa369184ae9a2d17622f8.jpg
 
Toyota wish ni 1.8 vvti engine ni gari bomba sana. Na ukinunua new model kuanzia 2005 ushuru wake ghali sana.

ISIS sio nzuri ukizingatia wamechanganya D4+vvti ina matatizo ya engine.

Wish ukinunua itabidi upandishe body kwa kuwa iko chini.

Wish gari mzee.

Niliendesha dar mwanza lita 80 tu nilitumia
 
Back
Top Bottom