Msaada wa biashara gani nifanye,please!!!

ufumawicha

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
504
209
Kama nilivyowahi kuwaelezeni,nimehamia Mbeya ambapo nimefanikiwa kupata kazi ya ulinzi,ambapo pamoja na kujibana ninaweza kujiwekea akiba tsh.120000/=.Naombeni ushauri nifanye biashara gani,kwa mtaji huo.Mke wangu ni mama wa nyumbani na amekuwa akinisisitiza sana nimfungulie japo kibiashara kidogo.NAOMBENI USHAURI PLEASE.
 
Kama ulipo ni kwako na pana nafasi ya banda, nakushauri ufuge kuku wa kienyeji. Kwa 120000 utapata kuku wasiopungua 8 ambao baada ya mwezi mmoja wataanza kutaga. Ukiokota mayai 8 daily, ukayauza kwa 450, utakuwa na uhakika wa at least 3000 kila siku. Hapo nimeassume una banda teyari.
 
Kwa kuanzia jaribu kumfungulia mkeo biashara.

Faida ya jambo hili ni :-
1. Mtu mwenye kufanya kazi au shughuli yoyote kwa kiasi kikubwa akili pia huwa "shape".
2. Huenda akawa na kipaji au mkono wa biashara kwa maana hiyo mafanikio yake ni mafanikio ya familia.
 
Ndugu Vingingula,asante sana kwa ushauri.Nimeamini hapa JF kuna watu wanaojali sana.Nilifikiria san kufuga,tatizo ni kuwa hapa nilipo NIMEPANGA CHUMBA NA SEBULE
 
Kwa kuanzia jaribu kumfungulia mkeo biashara.

Faida ya jambo hili ni :-
1. Mtu mwenye kufanya kazi au shughuli yoyote kwa kiasi kikubwa akili pia huwa "shape".
2. Huenda akawa na kipaji au mkono wa biashara kwa maana hiyo mafanikio yake ni mafanikio ya familia.
Kufungua biashara si tatizo.Tatizo ni biashara gani mtu afanye,ndiyo mtihani hapo.
 
Nipo Iyunga
Ok gud. Tafuta banda umfungulie shemeji mgahawa, au mpeleke shemeji veta akasomee ufundi kudarizi kisha akishahitimu mfungulie office awe anashona mashuka mnauza. Mtaji ukikua hayo mashuka mpeleke tunduma.
 
Back
Top Bottom