Msaada wa Ajira

BOFREE

JF-Expert Member
Mar 1, 2012
985
1,297
Habari za majukumu,

Mimi ni kijana wa kiume miaka 26 nimemaliza Shahada ya Ualimu masomo Geography na Kiswahili ninaomba mwenye nafasi yoyote ya ajira aweze kunisaidia.

Mimi ni muaminifu na mchapakazi naweza kufundisha shule yoyote ile kuanzia shule ya msingi mpaka secondari napatikana mkoa wa Dar es Salaam kwa yoyote mwenye nafasi naomba tuwasiliane nimtumie mawasiliano ya simu.

Hali yangu si nzuri familia inanitegemea nimejaribu kupambana lakini hali ni mbaya
 
Anahitaji msaada na sio maswali. Mambo ya umri huku Africa achana nayo tu maana kuna viumbe huwa wanaishi umri mmoja kwa miaka miwili hadi mitatu na tunaishi nao huku mtaani vizuri tu.
😁😁😁😁 Basi mwenye connection amtaftie aisee naijua taabu aanayopitia tatizo jingine sekta binafsi ya mashule bado ipo damaged sana , mashule mengi mikopo tuu walimu hawalipwi unaishia kupewa posho 150000 kwa mwezi , na allowance ya tsh 20000 ukishika zamu za wiki
 
Mkuu umejoin JF mwaka 2012 daah ulikuwa na miaka mingap , mana enzi hzo ni wachache sana waliokuwa aware na JF, leo hii unadai una miaka 26 mbona kama unatushika
unaitajika msaada wako kiongozi hali ni mbaya sana
 
Duu pole sana kiongozi mimi ni mwalimu kama wewe nilimalza 2018nikaona ajira hakuna what decided ni kupambana tu ikitokea dili yoyote napita nayo....but kama kuna mtu anaeweza kumsaidia amsaidie maisha magumu
 
Mkuu umejoin JF mwaka 2012 daah ulikuwa na miaka mingap , mana enzi hzo ni wachache sana waliokuwa aware na JF, leo hii unadai una miaka 26 mbona kama unatushika
Jibu unalolihoji hili hapa mkuu
 
Kazi za ualimu imeshakua mtiti kuipata na sijui mwaka huu kama ajira zitatoka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom