Msaada wa aina ya gari ya kununua

GREAT VISIONAIRE

JF-Expert Member
Sep 28, 2012
365
453
Nina shida ndogo, nataka kupurchase gari, kati ya Range rover Discovery 4 ama Mercedes Benz E Class ya 2015, engine yake ni 4000cc.

Nimebajeti kutumia si zaidi ya laki moja kwa siku kwa ajili ya mafuta ya gari nitaloendesha. Shughuli zangu kusafiri ni mara chache, muda mwingi nakuwepo Dar.

Sasa ninaomba msaada kujua gari ipi itanifaa kwa bajeti yangu na foleni hii, ili kuendelea na vishughuli vyangu hapa mjini.
 
Nunua range rover autobiography..ni gari nzuri sana huwezi fananisha na hizo ulizotaja
 
Mkuu....
Nunua gari ya RANGE ROVER STARTECH, au CADILLAC ESCALLADE, au PRADO V8 ( 2017 ) MERCEDES BENZ G-CLASS, AUDI R8, BMW X7, hizo gari zinakufaa kwa shughuli zako bajeti ya mafuta ya hizo gari sio chini ya laki 3,

ila ni vizuri ukaweka oda uingereza na wataleta kwa mfumo wa leftie yaani usukani wa gari upo kushoto.

Mkuu....
Unaienjoy na safari zako.
 
Nina shida ndogo, nataka kupurchase gari, kati ya Range rover Discovery 4 ama Mercedes Benz E Class ya 2015, engine yake ni 4000cc.

Nimebajeti kutumia si zaidi ya laki moja kwa siku kwa ajili ya mafuta ya gari nitaloendesha. Shughuli zangu kusafiri ni mara chache, muda mwingi nakuwepo Dar.

Sasa ninaomba msaada kujua gari ipi itanifaa kwa bajeti yangu na foleni hii, ili kuendelea na vishughuli vyangu hapa mjini.
BMW X7
 
Unajua kama kuna faraja kuu ya mitandao basi ni ile hali kuweza kuishi maisha ya kifikra hata kama hunayo kweli. Pengine mdau yupo zake kwenye siti ya mwisho ya daladala la gongo la mboto, mfukoni ana buku ya kugeuzia kesho halafu anaomba ushauri wa gari ya kununua. Safi sana, baada yeyote kila jambo huanza na ndoto.
Ninachojua mimi mwenye nia hasa ya kununua gari kama hizo tayari keshamiliki gari kadhaa ikimaanisha ana uwezo mkubwa tu wa kuweza kupambanua akitakacho.
 
Mkuu....
Nunua gari ya RANGE ROVER STARTECH, au CADILLAC ESCALLADE, au PRADO V8 ( 2017 ) MERCEDES BENZ G-CLASS, AUDI R8, BMW X7, hizo gari zinakufaa kwa shughuli zako bajeti ya mafuta ya hizo gari sio chini ya laki 3,

ila ni vizuri ukaweka oda uingereza na wataleta kwa mfumo wa leftie yaani usukani wa gari upo kushoto.

Mkuu....
Unaienjoy na safari zako.
Aisee Uingereza wanaendesha Mkono wa kulia RHD na sio kushoto LHD.
 
Back
Top Bottom