Msaada uwakala kusajili line za simu

Msaada uwakala kusajili line za simu

Kaliculus

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2019
Posts
271
Reaction score
248
Jambo wakuu. Nimechukulia usajili wa line za simu kama fursa kwa upande wangu, hivyo naomba mwenye ABC's kuhusu namna ya kuwa wakala wa kusajili line kwa finga- print anifahamishe yafuatayo:

1. Vifaa kwa ajili ya kuanza kazi ya usajili
na gharama yake

2. Namna ya kupata kibali cha uwakala na
gharama yake

3. Je, wakala wa kusajili line anapataje
faida ( Kamishen) ?

4. Mengineyo kama yapo.
Najua wapo watu humu wanafanya hiyo
kazi. Nawasilisha!!!!
 
Mm nafanya hyo kazi almast makampun yote ya simu

Cha kwanz inatakiwa uwe na smartphone ambayo utaweka app kwaajili ya kazi hii ni kwa mitandao ya halotel na ttcl maana airtel,voda na tigo kuna kifaa kimoja kinaitwa famoco ambacho ni simu iliyounganishwa moja kwa moja na kifaa cha finger print

Cha pili lazma uwe na namba ya nida hii ni lazma ili uweze kupewa kifaa kwaajili ya usajili wa fingerprint

Cha tatu unafika kampuni ya simu kila kampun kuna watu wanaitwa team leaders ambao kaz zao ni kuwasajili mawakala wapya (Mm mwenyewe ni team leader wa halotel moshi town)

Baada ya hapo lain yako kutokana na mtandao husila itawezeshwa kuwa code yaan lain maalum kwaajili ya uwakala na kulipwa malipo yako yote then utawekewa app kwenye simu au famoco na baada ya hapo utaelekezwa namna ya kusajili kwa kila mtandao

MALIPO
makampuni ya simu yanalipa mawakala wake kwa bonus na commision na hvi vyote vinategemea wateja wapya unaowasajili kila mwez

Kwa maelezo ya zaid % za commision utapata kwa team leader wakata anakuelekeza kaz


Ukiwa seliaz ni kaz nzur sana japo kwa sasa huu mfumo wa alama za vidole umepelekea wateja kungua kwa kias flan
 
Cha kwanz inatakiwa uwe na smartphone ambayo utaweka app kwaajili ya kazi hii ni kwa mitandao ya halotel na ttcl maana airtel,voda na tigo kuna kifaa kimoja kinaitwa famoco ambacho ni simu iliyounganishwa moja kwa moja na kifaa cha finger print
Mkubwa nasikia kwa sasa hata Voda,tigo & airtel sio lazima kuwa na Famoco

Halafu hako kafingerprint leader kanauzwa bei gani
 
Back
Top Bottom