Msaada uti+malaria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada uti+malaria

Discussion in 'JF Doctor' started by bandubandu, Apr 29, 2011.

 1. b

  bandubandu Member

  #1
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Ndg zangu naomba msaada,juzi nimepima malaria nikakutwa nayo 2,nikaanza matibabu ya cndano 5 za artem,pamoja na declopar kwa ajili ya maumivu maana mwili ulikuwa unamaumivu makali sana,jana nimerudi hospitali kuchoma cndano nikaomba kupima mkojo maana maumivu ya mwili yalikuwa makali sna,majibu yalionyesha nana UTI hivyo dk akaniandikia dose ya cpro yaani vdong 10 kwa muda wa cku 5 yaan 1*2 je hii ni sawa?jambo jingine je UTI inaweza sababisha maumivu ya tumbo hasa sehemu ya juu karibu na chembe moyo na tu
   
 2. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Pole bandubandu,

  Kama ulipima malaria kwa BS ikakutwa basi una malaria, endelea kutumia dawa za malaria (japo sijui kwa nini alikupa sindano, ilipaswa utibiwe kwa vidonge, labda kama unikuwa unatapika sana au muoga wa dawa za kumeza). Lakini vile vile ukigundulika na malaria haimaanishi huwezi kuwa/kupata UTI pia, kama ulipima mkojo na ikaonekana una UTI basi pia tumia dawa ulizopewa, Cipro (Ciprofloxacin) ni dawa sahihi na dozi ya kidonge 1*2 ni sahihi.

  UTI ni maambukiza ya njia ya mkojo, maambukizi yanaweza panda mpaka level ya mafigo na kusababisha maumivu ya tumbo. Lakini tumbo la chakula na tumbo la uzazi ni matumbo mawili tofauti. Sitegemei maumivu ya tumbo ya UTI yawe sehemu ya chembe. Maumivu ya tumbo sehemu za chembe mara nyingi huwa ni tumbo la chakula, sana sana mfuko wa chakula wenyewe.

  Dawa za familia ya NSAIDs (huna haja ya kuijua) ambapo Diclopar ni mojawapo husababisha Gastritis ambayo maumivu ya tumbo kwenye eneo la chembe. Hii ni kwa sababu hizo dawa zikitumiwa kwa wingi/muda mrefu husababisha kudhoofika kwa kuta za mfuko wa tumbo na hivyo acid inayomwagwa kwa kawaida tumboni kuumiza kuta za mfuko wa tumbo.

  Ushauri wangu: Endelea na dawa za malaria umalize dozi, Endelea na Cipro umalize dozi, ACHA KUTUMIA DICLOPAR...kama ni muhimu kutumia dawa ya maumivu basi tumia zisozo jamii ya NSAIDs.
   
 3. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  NB: Kama una ulcers, acha kutumia Diclopar na dawa nyingine za jamii ya NSAIDs, amabazo mara nyingi ni dawa za kutuliza maumivu.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  bandubandu,uti ikikushambulia kwa muda mrefu inaweza kupelekea infection kwenye figo (ambayo sio ya hatari kama itatibiwa na kuisha).inawezekana dr amehisi unaweza kusikia maumivu kiasi cha kutoelewa yanatokea wapi.ukimaliza dawa na maumivu yakaendelea,rudi kwa dr yuleyule ili akusaidie zaidi.otherwise hebu google uti uone unaweza kujiepusha nayo vipi kutokana na mazingira yanayokukabili na dalili za mwanzo.pole sana
   
 5. b

  bandubandu Member

  #5
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  mkuu heshima kwako,hakika nafurahi kupata ushauri mzuri na nitaufanyia kazi,pamoja daima tujenge taifa
   
 6. b

  bandubandu Member

  #6
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  mkuu nashukuru pia kwa mawazo mazuri na ushauri,ntaji
   
 7. b

  bandubandu Member

  #7
  Apr 29, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Mkuu Riwa samahani umenishauri nisitumie dawa za maumivu jamii ya NSAIDs,ombi naomba uniambie dawa mbadala kwa majina ninazoweza kuzitumia kwa ajili ya maumivu zisizokuwa jamii ya NSAIDs
   
 8. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Paracetamol,Ibuprofen,Meloxicam,Piroxicam,Tramadol etc.
   
Loading...