Wakuu Habari,
Nilikuwa nahitaji mwongozo wenu kwenye hili.
Tuna nyumba yetu Mbeya ambayo tumerithi toka kwa baba na mama baada ya kufariki. Tupo kama 6 hivi watoto. Kabla ya hapo kulikuwa na mashamba ya wastani kama hekari 5 Pamoja, garage na land rover ndogo. Vyote viliuzwa na baadhi ya ndugu tukiwa wadogo. Binafsi, nilitaka nianze kuvifuatilia, nikaona niachane navyo, nikasamehe na niendelee na yangu.
Nyumba tulikuwa tumepangisha, sasa kutokana na usumbufu wa mpangaji wa kutoa kodi, tumeafikiana na wadogo zangu tuiuze tu nyumba.
Maswali yangu:
Ni nani nimwone kwa ajili kufanyia valuation?
Sheria ikoje kuhusu mirathi, endapo marehemu hakuacha wosia. Naona baadhi ya ndugu wanasema Bibi na babu wanahusika katika urithi.
Nilikuwa namba na utaratibu wa kuuza nyumba ukoje? Labda mashaidi, sehemu gani unapitia? ili kuepuka kutapeliwa na mambo mengineyo.
Cha msingi kaeni kikao cha ukoo mteue msimamizi wa mirathi.
Aliyeteuliwa achukue miniti ya kikao hicho na barua ya mtendaji aende mahakama ya mwanzo kwenye eneo lenu kwa taratibu za kufungua mirathi na kupewa barua ya usimamizi.
Cha msingi kaeni kikao cha ukoo mteue msimamizi wa mirathi.
Aliyeteuliwa achukue miniti ya kikao hicho na barua ya mtendaji aende mahakama ya mwanzo kwenye eneo lenu kwa taratibu za kufungua mirathi na kupewa barua ya usimamizi.
Lakini kwa nini muuze?? Binafsi sijaona sababu eti mpangaji halipi kodi, binafsi siwezi kukubali kuuza nyumba waliotuachia wazazi anayetaka sehemu ya pesa tunamlipa chake kwa maandishi na ajue kajitoa mwenyewe....
si shauri muuze nyumba ya urithi, kama mnaweza watoeni wapangaji waliopo iboresheni nyumba tafuta wapangaji wapya , nyumba ikiwa nzuri na bora hata mpangaji atakuwa na nidhamu ya kulipa kodi.