Msaada: Utararatibu Kaymu

Msaada: Utararatibu Kaymu

brightoscar

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2013
Posts
369
Reaction score
544
Wanajamii nimenunua bidhaa kutoka Kaymu na nimelipa kupitia Tigo Pesa mpaka sasa hawajanipa nofication yoyote ya kuanza kuprocess order yangu na kunitumia.

Kwa kawaida inachukua muda gani wao kukupa progress after payment kwa wenye uzoefu?
 
kaymu sidhani kama wako serious!!! Wakiona order yake faster watakupigia simu baada ya kulipa ni more phone calls..
 
Wapo serious mkuu. Mzigo wako utapata tu. Sema weekend hawafanyi kazi.

Nikiwa na haraka na sina muda wa kwenda madukani huwa nawaambia waniletee pale ofisini. Nawapa hela baada ya kuridhika ndo nawapa hela.

Unaagiza kitu asubuhi saa 7 mchana kinakuwa kimeshafika.

Angalizo; usilipe kwanza hadi wakuletee mzigo cause unaweza kupata kitu usichotegemea. Kiatu wanasema ngozi kumbe sio ngozi
 
utapata mkuu usiwe na wasi wasi vuta subira... ila mkumbuke kaymu sio wanaouza direct ila maduka ndo yanauza kupitia kaymu.. mfano kama una duka lako unaweza kuuza kupitia kaymu... pia unaweza tembelea goodlookingtz store wako smart sana na bei zao ni rahisi
 
Mimi nimekoma kabisa siwezi tena kuhagaika na hawa jamaa! Mwishoni mwa mwaka jana nili order laptop na kisha nililipia kupitia utaratibu wao wa Tigopesa. Nimesubiri karibu mwezi ndiyo wananiambia order yangu imefutwa! Sikuwaelewa hata kidogo. Niliambiwa seller hana bidhaa hiyo tena. Wakaniambia nitafute laptop nyingine yenye thamani hiyo,nami nikafanya hivyo na kuongeza bidhaa nyingine kwa seller mwingine. Nako mambo ni yale yale! Safari hii nimeongea na watumishi kama watatu ambao kila mtu ni mbabaishaji tu. Nayo nikaambiwa order yangu imefutwa! Waliamua kunirudishia pesa zangu baada ya kwenda ofisini kwao. Walinirudishia pesa zangu kwa tigopesa ambapo nilipata hasara ya chargers wakati wa kuchukuwa taslimu. Ukweli ni wababaishaji na sijui matawi yao mengine katika nchi zingine yako kama hili la Tanzania!
 
Mkuu ofisi zao ziko maeneo gan hapa Dar?
 
Back
Top Bottom