MSAADA!! Utaalamu wa vifaa vya solar.

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,330
2,000
Wadau ningependa kujulishwa namna bora ya kufunga vifaa vya solar kwa matumizi ya kawaida(Taa 1, Radio 1, Mashine 1 ya kunyolea nywele, Simu1).

Nina Solar Panel ya 40WATTS, Inverter ya 150WATTS, Solar Power control, Betri ndogo ya solar(ya maji) 20N.

System nzima ya Installation imefanyika na kuweza kuwasha vitu vyote hivyo but baada ya muda mfupi sana(sio zaidi ya dk10) mashine ya kunyolea nywele inashindwa kabisa kufanyakazi na betri level ya solar kuwa ya chini kabisa. Hii ni wakati wa mchana, na giza likiingia tu hiyo mashine ya kunyolea ndio haiwaki kabisa.

Nini cha kufanya ili mfumo wangu wa solar iweze kukidhi matumizi yangu.

Wadau ninaomba mawazo yenu ya kitaalamu, maana mahali nilipo hakuna Umeme wa TANESCO na Solar ndio njia mbadala kwangu kwani kuna jua la kutosha wakati wote wa Mwaka.
 
kajiti

Member
Oct 19, 2011
59
95
taa, redio na mashine vina watts ngap kila kimoja? battery ni mpya/nzima? kwa mtazamo wangu battery yafaa iwe ni kuanzia N50, taa, simu na radio zisiingie kwenye inveter (tafuta mtaalamu akusaidie kufanya hili)
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,330
2,000
taa, redio na mashine vina watts ngap kila kimoja? battery ni mpya/nzima? kwa mtazamo wangu battery yafaa iwe ni kuanzia N50, taa, simu na radio zisiingie kwenye inveter (tafuta mtaalamu akusaidie kufanya hili)
Asante sana kwa ushauri wako. Taa inatumia 1watt bahati mbaya sana Redio, Mashine ya kunyolea na TV havijaandikwa watts zake. Kifupi ni Redio ndogo na TV ndogo(14nchi).
Vifaa vyote vya solar ni vipya kabisa, ikiwemo hiyo betri.

Mahali nilipo mafundi wa umeme wapo ila kwenye issue za solar ni wageni kabisa.
Ukiondoa taa pekee(Hii ni DC hivyo haitumii inveter) vifaa vingine vyangu vya umeme viko kwenye mfumo wa AC hivyo ni lazima Inveter itumike.

Tatizo ni wakati nataka kutumia Mashine ya kunyolea au TV hapo umeme wa solar unafifia haraka sana. Hata kama nimezima vifaa vingine vyote bado inashindikana.
Ninahisi labda uwezo wa betri ni mdogo sana ama labda Solar Panel ni ndogo.
 
RR

JF-Expert Member
Mar 17, 2007
6,893

Hapa ishu sio udogo wa panel....ni uwezo mdogo wa betri yako....
Btw...tv, radio na vifaa vingine lazima vimeandikwa matumizi yake ya umeme...
 
mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
787
500
Pole mkuu. Panel ya 40w huendana na betri ya N40 ya unga (dry) ama N80 ya maji. Tunasema ratio ya 1:1 na 1:2. Kutokana na jua kutokuwaka "constantly" tunashauriwa watts chache za panel zizidi ili battery yako ijae hata kama kuna wingu.
Hata hivyo ili ufaidi tv, yakupasa panel yako walau iwe na 80W. Kwa betri uliyonayo utachukia solar.
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,330
2,000
Hapa ishu sio udogo wa panel....ni uwezo mdogo wa betri yako....
Btw...tv, radio na vifaa vingine lazima vimeandikwa matumizi yake ya umeme...
Asante sana kwa ushauri wako, Ngoja nichukue hatua sasa za Utekelezaji.
 
Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
6,330
2,000
Pole mkuu. Panel ya 40w huendana na betri ya N40 ya unga (dry) ama N80 ya maji. Tunasema ratio ya 1:1 na 1:2. Kutokana na jua kutokuwaka "constantly" tunashauriwa watts chache za panel zizidi ili battery yako ijae hata kama kuna wingu.
Hata hivyo ili ufaidi tv, yakupasa panel yako walau iwe na 80W. Kwa betri uliyonayo utachukia solar.
Asante sana kwa ushauri wako.
Sasa nimepata Mwangaza zaidi kuhusu umeme wa Solar.

Inavyoonekana Betry kavu(Dry) ni Bora zaidi kwa umeme wa Solar?

Swali rahisi kidogo, Hizo betri kavu(Dry) ni Universal kwa matumizi yoyote au kuna special za matumizi ya solar system tu?
Gharama za kuinunua zikoje kuanzia yenye N40, N60 na kuendelea?
 
next

JF-Expert Member
Nov 2, 2007
608
225

mkuu kwa matumizi ya solar inashauriwa utumie deep cycle batteries (deep discharge batteries) hizi zimetengenezwa kuweza kutumika hadi nusu ya nguvu yake (ingawa tunashauliwa kutumia robo tu ya nguvu yake na si zaid ili idumu zaidi) hivyo itakufanya ufanye shughuli zako kwa muda mrefu zaid ya hizi Betri za kawaida (chukulia Betri za gari) hizi Betri ninazozizungumzia zinauzwa bei kidogo. 80ah (sawa na N80) inauzwa around TZS 265,000 sijajua za uwezo wa N40 to 60 zinauzwa bei gani.

wewe upo wapi? hiyo system unaitumia kwa biashara ya saloon?
 
Asante Sana next kwa ushauri wako.
Mimi niko mikoa ya Kaskazini(Katikati ya Arusha na Kilimanjaro).
Hii system kwa sasa naitumia nyumbani ila naelekea kutaka kuitumia kibiashara(saloon na kucharge simu) maana italipa.
 
Last edited by a moderator:

engmtolera

Verified Member
Oct 21, 2010
5,150
1,250
Wadau ningependa kujulishwa namna bora ya kufunga vifaa vya solar kwa matumizi ya kawaida(Taa 1, Radio 1, Mashine 1 ya kunyolea nywele, Simu1).

Nina Solar Panel ya 40WATTS, Inverter ya 150WATTS, Solar Power control, Betri ndogo ya solar(ya maji) 20N.

System nzima ya Installation imefanyika na kuweza kuwasha vitu vyote hivyo but baada ya muda mfupi sana(sio zaidi ya dk10) mashine ya kunyolea nywele inashindwa kabisa kufanyakazi na betri level ya solar kuwa ya chini kabisa. Hii ni wakati wa mchana, na giza likiingia tu hiyo mashine ya kunyolea ndio haiwaki kabisa.

Nini cha kufanya ili mfumo wangu wa solar iweze kukidhi matumizi yangu.

Wadau ninaomba mawazo yenu ya kitaalamu, maana mahali nilipo hakuna Umeme wa TANESCO na Solar ndio njia mbadala kwangu kwani kuna jua la kutosha wakati wote wa Mwaka.

kikawaida,kabla hujanunua mfumo wa umeme jua ni lazima ufanye designing,na hii huzingatia sana mambo yafuatayo
1.ni aina gani ya vifaa unataka kutumia
2.vifaa hivyo power kiasi gani
3.je vifaa vyako utaviwasha kwa masaa mangapi
Baada ya kuelewa hayo,ndipo unakwenda sasa kudesign ukubwa wa solar panel utakayohitaji,ukubwa wa betri utakayohitaji,charger controler na kigeuza mkondo wa umeme

kwa harakaharaka tu,utagundua kuwa,ulinunua mfumo huo bila hata kufanya hayo niliyoyaeleza hapo juu na imesababisha kununua kihifadhi charge(betri) ndogo isiyo na uwezo wa kuvipa umeme vifaa vyako.

inaeleweka kuwa,initial investiment ya mfumo wa umeme jua ni gharama,lakini ukishafanikisha kuwekeza ktk mfumo huu faida yake ni kubwa sana.

Naomba nami nitie ushauri wangu ktk hili
mfumo ulionao wa watts 40 unatakiwa uwe na:-
1.Moduli ya jua watts 40
2.kihifadhi chaji[betri] chenye ukubwa wa N55Ah
3.Kidhibiti chaji[charge controler] chenye ukubwa wa 5A
4.Taaa zako zisizidi 10 na ziwe na ukubwa wa kuanzia 6watts-9watts
muda wa kutumia uwe ni masaa yasiyozidi 4 hadi 5 tu kama vifaa vyote vitatumika pamoja na kama utatumia taa peke yake kwa usiku tena za nje basi zinaweza kukesha na ziwe taa 2 hadi 3 tu,kama ni mashine ya kunyoa basi ni saa 1 hadi 2 tu na kama ni tv basi iwe ni saa 1 tu ama nusu saa
 
upo vyema engmtolera.
nimechek mashine yangu ya kunyolea ni 15watts, nikijaribu kufanya hesabu let say ya kutumia kwa masaa 12 kwa siku kwa vifaa vifuatavyo
15 watts mashine ya kunyolea moja
11 watts energy saver mbili
15 watts medium radio moja
tuachane na tv kwa sasa ili tupate system naafuu kabisa.
hapo jumla ya mahitaji yako ni 52 watts
okay tuikaribishie kwenye 60 watts. kwa 60 watts any inverter of 75 (60*1.25) watts and above can handle the load. Inverter inatakiwa izidi maximum load by at least 25%.
kumbuka maximum load ni muhimu kuipata ili uweze kujua.
mosi, inverter yako unaweza kufanya kazi bila kuzidiwa
pili. ukubwa wa battery bank utakayotakiwa kuwa nayo. hivyo Inverter yako ya 150 watts. inafaa kwa system yako. na kwakua ni system ndogo basi iwe ni 12volts system
kupata battery bank
12hrs*60w=720wh
720wh/12v=60ah
hivyo battery moja ya 80ah inatosha kbs
charging currency ni 10% ya battery capacity
so charger controler ya 8a
ukitata kupata solar panel ya kufaa mahitaji yetu apo juu
12v*8a=96watts
hivyo panel moja ya 100watts (au mbili za 50 watts au mbili za 60 watts zilizoungwa sambamba ( parallel)) zinafaa pia hasa ukizingatia nguvu ya jua kwa siku husika na (efficiency rate) kiasi cha ufanisi cha panel yako ya solar.
naomba mnisamehe kwa kuchanganya lugha.
 
mwangalizi

JF-Expert Member
Apr 24, 2012
787
500
Asante sana kwa ushauri wako.
Sasa nimepata Mwangaza zaidi kuhusu umeme wa Solar.

Inavyoonekana Betry kavu(Dry) ni Bora zaidi kwa umeme wa Solar?

Swali rahisi kidogo, Hizo betri kavu(Dry) ni Universal kwa matumizi yoyote au kuna special za matumizi ya solar system tu?
Gharama za kuinunua zikoje kuanzia yenye N40, N60 na kuendelea?

Kwa kweli nina muda sasa tangu ninunue za ukubwa huo! Kwa kutokujua nilianza na panel ya 30W; sitaki kukumbuka jinsi nilivyolaani solar.
Kwa sasa natumia panel ya 200W, betri dry ya N150 (wanauza around laki nne); tv 24hrs nikipenda, nachaji laptop, naprint kwa kutumia epson any time. Inverter ya 300W.
 
Mushi92

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,909
2,000
Kwa kweli nina muda sasa tangu ninunue za ukubwa huo! Kwa kutokujua nilianza na panel ya 30W; sitaki kukumbuka jinsi nilivyolaani solar.
Kwa sasa natumia panel ya 200W, betri dry ya N150 (wanauza around laki nne); tv 24hrs nikipenda, nachaji laptop, naprint kwa kutumia epson any time. Inverter ya 300W.
Mkuu una panel kampuni gani?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom