Msaada unahitajika kuhusu email hii

Mbona mi naona kama anatakiwa kwenda kuchukua mpunga uliotumwa na UN kwenye DHL kumfidia hasara aliyopata kwenye biashara yake. Akifika ofisini atapewa maelekezo
Akachukue kadi dhl ambayo hata kwenye email hawajasema imetumwa kwenda wapi via dhl? Si kichekesho hicho
hata kwenye email hakuna sehemu walio muaddress kwa jina lake.
pili eti inabdi a cover gharama za ulinzi wa hiyo ela dila 169 yani wakutumia over bilion tatu washindwe kulipa hiyo laki tatu na ushee.
sisi wazoefu wa haya mambo tunasema ni wizi wa mchana kweupe utaliwa hizo usd 169.
Nashangaa kwanini watu wanaibiaa kizembe hivi haya mambo nimeanza yajua toka mwaka 2005 nikiwa form tu.
scammers hawa akimbie
 
Ninavyoona, email ameifanyia editing labda kuficha identity yake maana hata mawasiliano ya office ya DHL ameitoa.
Hiyo laki 3 + DHL wamekataa kuepuka kuzidisha muda wa kumlindia mzigo wake wakati yeye anakuwa ameshalipia(hawajui atachukua baada ya muda gani)
Ila unachosema kinawezekana pia kwa sababu wizi sasa hivi umepakwa asali.
 
Nalokwambia ni wizi tena uliodhahiri.
Mimi nshapokea emails na kuchat na mascammers wengi yani naweza kujua mtu ni scammer mara moja tu.
Nshapokea emails nyingi za wanaodai wakimbizi wako dakar senegal wazaz wao walikiwa wanafanya serikali ya gadafi wana maela mengi waliuawa wanatafta wayahamishie kwa mtu then utapewa mgao tena anajifanya binti anakutumia mapicha uoagawe.
Nishapomea email eti unatumiwa documents ujaze ukiambiwa kwamba kuna mama kafariki alikuwa na ela nyingi sana sasa hana ndugu katika kupekua nani arithi mali zake wakakuta jina na address yako kama mtu wake wa karibu..
Nshaookema emails kibao eti mtu yuko hoi anakuachia mali zake uzigawe kama charity ukiipokea leo kesho yake utashangaa unapokea email toka kwa mtu mwngime akidai ni lawyer wake na akikutaarifu kuwa huyo mtu kafariki usku ila process zitaendelea.
Na usiku huu nimetoka kuchat na scammer whatsapp ila mimi uwa naendelea nao nawachora tu mpaka mwisho nawapa matumaini as if wamenipata kumbe nawaenjoy.
Nishapokea email eti nimeshinda bahati nasibu ya nokia usd 1000000 wakati hata sina simu ya nokia mwaka 2011.
Nishapokea emails kuwa nimeshinda green card na bla bla kibao
So nakwambia kitu nachojua
 
UN gani haina hata spellcheck!
 


Nigerians hao wamenza tena mambo yao.....usifuatilie wala nini....wanataka kukuingiza tu mjini.
 
Aisee hao wanaojidai wakimbizi ndo wanasumbua sana kwenye box La email yangu mara wako dakar mara south Sudan yani full vituko
 
Aisee hao wanaojidai wakimbizi ndo wanasumbua sana kwenye box La email yangu mara wako dakar mara south Sudan yani full vituko
Soon utaskia baba au mimi nilikuwa waziri wa yahya jammeh
 
Hiyo dola 165 unatakiwa uitume kwa branch ya dhl benin cotonou ahahaa utapeli
 
Nakuomba uachane nao hao ni wezi watupu utarembwa kwa maneno mazuri sasa ukiingiza tamaa mbele ukatumia document zako za benki utaliwa pesa zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…