Msaada unahitajika haraka au ndoa inavunjika

mafia boy

JF-Expert Member
Jan 7, 2013
268
82
Aisee jamani naomba mnisaidie ...mie na mke wangu na mtoto wetu mmoja na huyu mke wangu tunapendana na kuahidiana mapenzi ya dhati cha ajabu.. Tunaweza tukawa tupo kwenye furaha mfulilizo...mpaka watu mtaani wanatumaind the way tunavyopendana... Sasa ikitokea tu kukorofishana kidogo wife ye hudai taraka.. Na siku nyengine hua anachukua cm yangu kwa siri halafu huanza kuchati na watu ambao anahisi yeye mie wapenzi wangu yaani akiona SMS hata imeandikwa""sawa wangu""..mitusi atakayopata huyo MTU si yanchi hii
Baya zaidi hua ananichunia sana akinuna atakaa hata siku 3 bila ya mawasiliano mazuri...hivi juzi kakuta nimetumiwa x kwenye group...na Mimi nikaifoward kwa MTU mwengine weeee....hadi wazazi wangu waliju kua naagalia x.. Sasa hii tabia nahisi ka inanichosha...mpaka naandika Uzi huu tayari ashadivert simu yangu...
Nahitaji jinsi ya kuiondoa hiyo divertion pia nahitaji nini cha kufanya ili amani itawale???
 
Hebu jaribu kumpiga hata taraka moja alfu uone kama alikuwa anabeep au lah
 
call divert kaitoe ipo kwenye call settings, aisee hiyo kesi nishakutana nayo demu alikua hivo hivo 200% usiku nimelala anaingia whatsapp kuchungulia text, akipiga mtu hadi ajue ni nani, mi nilikua sina tabia ya kukagua simu yake na kila akikagua akikuta traces zozote mwisho wake ni kupendekeza break up,
in short huyo manzi keshapata mtu pembeni sasa anatafuta uchochoro wa kukutoroka trust me. mpe likizo kama wiki mbili hivi bila mawasiliano yeyote ukweli utajulikana tu
 
Yaan jaby hizo ndio ishu zake...hivyo hivyo...halafu anachojivunia kua home kwa wazazi wangu wanamkubali aisee...Bimkubwa akisikia tu nimekorofishana nae hua haniulizi ananilaumu tuu....sasa nahisi nimpe likizo ndogo kwanza
 
Pole sana!
Mkeo ana wivu wa kijinga sana ambao una dalili za kuwa ukichaa. Kuchukua simu yako na kuwatukana watu asiowajua ni kukutia aibu na kukudharirisha, na kuna siku inaweza kukuletea kesi kubwa tu, rejea makosa ya mtandao.Kutuma clip ya x hadi kwa wazazi wako u ujinga uliopita kipimo, na nikusifu kwa uvumilivu wako!! Kama ana shangazi au dada zake wakubwa waombe wazungumze naye na kumuonya. na ukumbuke mara nyingi watu wa aina ya mkeo wana mambo yao ya siri hivyo muda wote hufikiri anayoyafanya na wewe unafanya, mchunguze pia!! akishindwa kujirekebisha mrudishe kwao kwa muda wakati ukitafakari!!
 
Ugomvi unasababishwa na smartphone, tumia nokia ya tochi, ukishindwa futa majina yote ya kike ktk simu yako, ukishindwa tafuta mtu wako mpange mission achati na my wife wako then na wewe unamstukiza kwa kuinyakua simu yake then unamfanyia ukorofi uliotukuka baada ya hapo atatulia.
 
Baadhi ya matukio yanafanana na wa kwangu,, ila kwa uzoefu kodogo nilionao naona ni wivu ulopitiliza, ila la kudai talaka atakua na chembe chembe za majuto ndani ya nafsi yake baada ya kumuoa na humpelekea mda mwingine kuwaza kuachana nawe ili akatimize matakwa ya moyo wake aliyokua nayo awali!…

Nishapambana na hilo la kutaka talaka naona nalishinda,,, mpuuze na mpe maneno makali na uonyeshe uko tayari kwa lolote atacool down
 
Huyo hakufai na atakuumiza zaidi mkuu,yeye hataki achunguzwe ila wewe anakuchunguza,Mtu mwenye wivu wengi wao si waminifu
 
Kaa utathmini tatizo lilipo myamalize ikishindikana, chungza pindi mlipoahidiana kuoana au ulipoamua kumuoa mazingira yalikwaje (upendo wa kulazimisha, upendo wa upande mmoja au upendo wa aina gani) usipopata jibu angalia ustarabu mwingine maana matusi kwenye ndoa, kejeli na makwazo huwa yanasababisha mengi na hata ulemavu kitu ambacho hukuwa nacho fikiria mara mbili, kama alikuwa rizki yako atatulia tu kama ulikuwa rizki yake utatulia si vinginevyo ni kuumizana. angalia magonjwa mengi kwa wanandoa ni presha, magonjwa ya moyo, vidonda vya tumbo, kuumizana mkiwa mnagombana... omba yasikufikie ni hatari sana
 
Ndio maana nilishapiga marufuku maswala ya simu yangu, Wewe nawe unamuendekza sana huyo Mkeo akidai talaka mpe.
Kuna muda inabd ujitofautishe kati ya kuwa Mvulana na Mwanaume Mkuu.
 
Nenda kanisani kama mkristo au msikitini kama Muislamu,waeleze viongozi wako wa dini wakusaidie,ila na wewe omba kwa Mungu wako ili akuepushie hayo majanga maana shetani naona tayari ameshabisha hodi kwenye ndoa yako..
 
Fikiri kabla ya kutenda ili usitende asiyoyapenda (fanya hasa yale uyafanyayo wakati mnapoishi kwa amani na furaha), naamini mtaishi kwa amani.
 
Back
Top Bottom