Gemini Are Forever
JF-Expert Member
- Sep 10, 2019
- 1,457
- 2,435
Habarini!
Mbuzi wangu wamekuwa wakisumbuliwa na ugonjwa wa kuzunguka. Yaani huu ugonjwa mbuzi akiugua anashindwa hata kutembea (anabaki kuzunguka tu hapo hapo) na unaonekana huwa unaathiri upande fulani wa mbuzi.
Kwa mfano, akiathirika sana kiasi cha kushindwa kusimama, yaani akishalalia tu upande wa kushoto basi hawezi kulalia upande wa kulia hata kama unamgeuza.
Yaani ukimgeuzia huo upande mwingine utakuta anajigeuza haraka sana (inakuwa mithili ya ncha za sumaku ambazo haziendani).
Naomba msaada wa namna yoyote wa tiba, chanjo na jina la ugonjwa kitaalamu.