Msaada tutani wakuu

Ze last Born

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,550
2,000
Habarini za asubuhi wakuu. Nisiwe mchoyo wa fadhila, natanguliza shukrani za dhati kwa muasisi wa platiform hii adhimu kabisa na namba moja nchini JF. Shukrani za dhati ziende pia kwa great thinkers wote wa JF kwa michango yao mbalimbali wanayoitoa .

Mimi ni kijana Mtanzania, umri 27yrs na nna Elimu yangu kubwa tu, kutoka Chuo kikubwa tu hapa nchini.

Niko safarini kuelekea KAHAMA ili nikapambane na maisha kikamilifu baada ya maisha ya Dar es Salaam kunishinda maana 99% ya hela niliyokuwa naipata iliishia kula tu na kulipa Kodi ya chumba basi,,yaani "Hand to mouth economy".

Nahitaji mtu ambae ni mwenyeji wa KAHAMA mjini ili anisaidie japo kuniongoza niwapo huko.

Sichagui kazi, katika jitihada za kutafuta pesa nimeamua kuvaa uso wa mbuzi na kutunza vyeti vyangu kabatini ili visinipumbaze akili.
Ntashukuru sana kwa wenyeji watakao jitokeza kunipa support.
 

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
29,754
2,000
Shuka kahama lala hapo asbh uliza gari za kwenda mwime watakuonesha... Kule Sasa kasome mchezo...Kama una kianzio kidg utafanya biashara maana maeneo huwa mnakatiwa kwa Bei rafiki ...kauze hata maji au juic za kopo ..uzuri machimboni maji ni maji. Iwe baridi au Moto yanaenda tu! Au Kam uko vyema kapike mbuzi na ugali kuanzia asbh. .! Ugali Dona na mhogo! Mbuzi ichemshe tu😋😋!hukosi 200-250k Kama Kuna nyomi
 

Ze last Born

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,550
2,000
Shuka kahama lala hapo asbh uliza gari za kwenda mwime watakuonesha... Kule Sasa kasome mchezo...Kama una kianzio kidg utafanya biashara maana maeneo huwa mnakatiwa kwa Bei rafiki ...kauze hata maji au juic za kopo ..uzuri machimboni maji ni maji. Iwe baridi au Moto yanaenda tu! Au Kam uko vyema kapike mbuzi na ugali kuanzia asbh. .! Ugali Dona na mhogo! Mbuzi ichemshe tu!hukosi 200-250k Kama Kuna nyomi
Shukrani sana mkuu kwa directives zako
 

Ze last Born

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,550
2,000
Ni salama zaidi kumpa kazi mtu unayemfahamu vema undani wake ili asije akafanya mambo ya hovyo huko kazini kisha akachafua reputation yako nzuri.
Wasiwasi ndo akili mkuu,, mie CV yangu iko vizuri tu ni mchapakazi na a very humble person...ni vile tu hujapata fursa ya kunifahamu.
All in all nakaribisha mtu yeyote mwenye nia njema ya kunikwamua hapa nilipo Sasa
 

Ze last Born

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
1,550
2,000
Shuka kahama lala hapo asbh uliza gari za kwenda mwime watakuonesha... Kule Sasa kasome mchezo...Kama una kianzio kidg utafanya biashara maana maeneo huwa mnakatiwa kwa Bei rafiki ...kauze hata maji au juic za kopo ..uzuri machimboni maji ni maji. Iwe baridi au Moto yanaenda tu! Au Kam uko vyema kapike mbuzi na ugali kuanzia asbh. .! Ugali Dona na mhogo! Mbuzi ichemshe tu!hukosi 200-250k Kama Kuna nyomi
I promise ntafika huko mwime dada #Manengelo na ntakupa mrejesho.
Kwasasa Sina cha kupoteza maana Sina mtoto, mke wala demu anayenipa pressure so I will struggle more reluctantly until I make a fortune out of it!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom