Msaada tutani, nina gari yangu aina ya Noah sr40 je nije/niende mkoa gani nikafanyie kazi ya kubeba angalau abiria?

Mkuu jaribu kuipeleka kwenye minada maana kuanzia Manyara hadi Singida minada inaanza tarehe Moja hadi mwisho wa mwezi ivyo huwezi kukosa abiria hasa wafanya biashara maana saivi magari ya mizigo ayaluhusiwi kubeba wafanya biashara ivyo lazima mfanya biashara awe na gari la kumpeleka kwenye Mnada
 
Komaa Hapo hapo Dar
Msumi Muhimbili=5000×10=50,000
Ukirudi unapata kama hiyo.
Unapiga alfajiri na jioni.
Jumla 200,000
Ukitoa gharama zako......uongo.....hukosi......
 
Huko Nzega-Kahama hazisajiliwi tena kubeba abiria toka ile ajali iliyoua 18 pale Tinde 2016 ikihusisha Noah na Semi

Ila zipo nyingi zikibeba kwa namba za njano kwa hiyo ni mwendo wa kutoa kidogo kila ukisimamishwa na traffic.

Manual ama Auto siyo issue maana hata Probox na Alphard kwa sasa zinapiga route huko.
 
Nenda shule za mjini kama upo Dar, mfano wa Zanaki, Diamond na Upanga ufanye kazi ya kusanya wanafunzi (School bus) kulingana na eneo unaloishi. Kila kichwa 50,000 mpaka 60,000. Ukipata wanafunzi wako 10 una ajira ya maana.

Jioni baada ya kumaliza kurudisha wanafunzi unaenda kutega posta unakula vichwa vya Gongolamboto au Mbagala.

Hizo plan za hapo juu ni kama ni mkazi wa Dar.
 
Mkuu minada ya huko ni amsha amsha kweli yaani kuna biashara.? Na ni bidhaa zipi zinatoka sana kwenye hiyo minada?
Mkuu jaribu kuipeleka kwenye minada maana kuanzia Manyara hadi Singida minada inaanza tarehe Moja hadi mwisho wa mwezi ivyo huwezi kukosa abiria hasa wafanya biashara maana saivi magari ya mizigo ayaluhusiwi kubeba wafanya biashara ivyo lazima mfanya biashara awe na gari la kumpeleka kwenye Mnada
 
Nenda shule za mjini kama upo Dar, mfano wa Zanaki, Diamond na Upanga ufanye kazi ya kusanya wanafunzi (School bus) kulingana na eneo unaloishi. Kila kichwa 50,000 mpaka 60,000. Ukipata wanafunzi wako 10 una ajira ya maana.

Jioni baada ya kumaliza kurudisha wanafunzi unaenda kutega posta unakula vichwa vya Gongolamboto au Mbagala.

Hizo plan za hapo juu ni kama ni mkazi wa Dar.
Nashukuru sana, mkubwa.
 
Komaa Hapo hapo Dar
Msumi Muhimbili=5000×10=50,000
Ukirudi unapata kama hiyo.
Unapiga alfajiri na jioni.
Jumla 200,000
Ukitoa gharama zako......uongo.....hukosi......
Mkuu nipe details zilizoshiba hapa
 
Mkuu jaribu kuipeleka kwenye minada maana kuanzia Manyara hadi Singida minada inaanza tarehe Moja hadi mwisho wa mwezi ivyo huwezi kukosa abiria hasa wafanya biashara maana saivi magari ya mizigo ayaluhusiwi kubeba wafanya biashara ivyo lazima mfanya biashara awe na gari la kumpeleka kwenye Mnada
Imekaa vzuri
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom