MUSIGAJI
JF-Expert Member
- Dec 26, 2014
- 2,187
- 2,462
Wanabodi habari nawasimu.
Kuna Jambo limetokea kwa dada fulani kwa kweli imenishangaza nikaona niilete hapa pengine ninaweza kupata mawazo na ushauri nikamfikishia au wahusika VODACOM wanawaza kushughulikia suala lake na kulitatua.
Huyu Dada anasimamia ofisi fulani inayoshughulika na huu uwakala wa MPESA, TIGOPESA n.k
Mwezi uliopita mwanzoni alikuja mtu akamwambia wako na kazi ya kujenga, sasa Kuna upungufu kidogo umejitokeza,Boss wao anaomba atume fedha kidogo kwenye simu yake ya voda (anayoitumia ya kawaida si ile ya uwakala) alafu atoe amkabidhi.
Akakubali huyo boss wao akatuma fedha, alituma mara mbili moja elfu 30 au 30+ na nyingine elfu 70 au 70+.
Baada ya kutumiwa akaitoa akamkabidhi yule bwana fundi.
Kumbe baada ya pale yule bwana aliyetuma (Boss wao) akapiga simu Voda, akasema ile 70 au 70+ ameituma kimakosa.
Sasa ilivyotumwa ndo aliitoa akamkabidhi bwana fundi,lakini alikuwa na fedha Kama laki tatu plus kwenye MPAWA.
Vodacom baada ya kupokea ile simu na wakaona alishaitoa basi wakafunga huduma ya MPESA. (Bila hata kumpigia kusikia kutoka kwake.)
Baada ya siku kadhaa akahitaji kutumia ile fedha iloyoko MPAWA akakuta kazuiliwa huduma,akapiga simu huduma kwa mteja ndo anaelezwa hivyo. Akaambiwa aende police kwanza,akaenda,kule akapewa RB then akaambiwa aende Voda wamfungulie akaunti.
Ameenda Voda,wanadai alipe kwanza ile fedha, kituko ni kwamba yule aliyetoa taarifa kuwa alituma fedha kimakosa,hata hapatikani kwenye ile simu,lakini Bado Voda wanasema aweke kwanza fedha kwenye akaunti yake (inaelekea walifunga huduma ya kutoa tu) ili hiyo fedha itumike kumlipa yule aliyedai ametuma kimakosa( japo hata simu yake haipatikani) alafu ndo afunguliwe huduma.
Alijaribu kwenda VODA makao makuu majibu yakawa yale yale. Binafsi bado nadhani walioshughulikia suala lake pale VODA tangu awali hawakuwa makini Kiieledi, Kwa mambo makuu mawili hivi.
Mosi, walipaswa kumpigia kusikia kutoka kwake punde baada ya kupokea malalamiko.
Pili, Baada ya yeye kigundua kuwa amefungiwa na akajoeleza kwao, walipaswa na wao walipomtafuta mlalamikaji bila kuopata simu yake kwa kitumia busara ya kawaida wangeona upande wa haki.
Wakuu, Je katika hali kama hii, huyu mdau ashauriwe Nini?