Msaada toka kwa Developers wenye experience kwenye Mobile Money Integration.

Muhamala

Senior Member
Oct 1, 2017
101
88
Nina project yangu inakaribia kufika hatua za mwisho kabisa ila kuna baadhi ya vitu ninapata shida jinsi ya kupata solution yake.

Na shida yenyewe ni kwa upande wa mobile money payment yani nataka mteja awe anauwezo wa kulipia kwa mobile money kwa mitandao mitatu yani Vocadom M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money. Yani nataka iwe mtu anapewa control number then anatumia ile control number kufanyia malipo kwenye menu ya mobile money mfano mzuri ni kwenye system ya Student's Loan Board ile inaitwa OLAS kwamba ili mwanafunzi alipie fees anapewa control number then ndio anaingia kwenye menu ya mobile money anaingiza namba ya kampuni then kiasi halafu anaingiza hiyo control number inakuwa tayari kashalipia. (Angalia picha chini)
Untitled_3_copy.jpg




Vile vile the same idea nadhani ndio hata hawa jamaa wa tatu mzuka na biko wanatumia same theory, kwa kuanzia nadhani ni lazima kwenda hizo kampuni za simu kufanya registration na vitu vingine vidogo vidogo ila mimi msaada ninaoomba hapa umejikita kujua whats behind hizo process zote na idea kwa ujumla ipoje.

Nina other option ninayoweza kutumia ila ubaya wake ni kwamba hiyo njia nyingine ina mlimit mtumiaji kutumia namba moja tu ambayo ataifanyia registration pindi anafungua akaunti kitu ambacho binafsi naona hakitaleta mantiki.

Nimeleta mada hapa nipate ushauri na nijue kwa kuanzia.
 
Kwenye hii kitu wacheki makampuni ya simu watakupa API ambayo utaintergrate kwenye system yako na mambo yatakuwa marahisi tu ,au nicheki 0687 535650 kwa maelezo zaidi sisi ndio wazoefu wa system developer
 
Kwenye hii kitu wacheki makampuni ya simu watakupa API ambayo utaintergrate kwenye system yako na mambo yatakuwa marahisi tu ,au nicheki 0687 535650 kwa maelezo zaidi sisi ndio wazoefu wa system developer

Ngoja niwacheki mkuu, Ahsante kwa ushauri.
 
kwa Tigo ingia web yao, API wameitupia uko

Tigo API yao nishaiona thanks chief, Voda nimejaribu wapigia wanipe link ila wanasema mpaka niende ofisini kwao na mimi nipo mkoani kwa sasa, bado Airtel nao siju wataleta story gani.
 
Back
Top Bottom