Msaada: Tofauti gan kati ya Computer science, computer engneering, na IT?

Finder

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2016
Posts
378
Reaction score
424
Kwa wajuvi wa mambo haya tusaidiaje utofauti wa hiz koz na ipi ni nzur zaidkatika ulimwengu huu wa technologia
 
Asanten
Ningependa kujua hasa kwa mfano mtu anayesomea computer science anasomea nn kwa undan zaid pia anayofautianaje na IT na computer engneering??
Kuna kijana kaniomba ushaur juu ya hizi koz ni ipi nzur kwa kuisomea?
Yeye anapenda sana mambo ya programming na developing apps and websites na kuwa mtaalamu wa mifumo ya ulinzi wa computer
 
Mwambie asome computer engineering ita mfaa kwa malengo yake
 
Mwambie asome computer engineering ita mfaa kwa malengo yake
Hii bongo miyeyusho. Usidanganyike na jina. Mm napendekeza walau asome CS. Engineering ya computer imeshahama siku nyingi sana iko kwenye mi AI na Robotics. Sasa kwa bongo land hii field iko nyum sana. Ila CS walau walau misingi yake iko pale pale.( science , principle , fundamental concepts, Laws nk) ziko pale pale. Kikubwa baada ya hapo ni yeye kujidevelop kwenye hizo field anazozitaka. Mfano hapo ametaja vitu vingi sana. Kiufupi a mastery kwenye labda apps dev kwa kuadv in programming. Ila CS itampa edge kuliko CE or IT.
 
Kama malengo yake ni haya "computer science" Naona ndo jibu sahihi
 
Computer Science (CS) ina matawi matatu ambayo ni:-

(i)Computer Engineering (CE) - hii inahusika na Computer hardware na Robots ambayo ina Artificial Intelligent (IA) hapa utasoma kuandika programu zinazoendana na hili eneo na pia utasoma umeme,

(ii)Software Engineering (SE) - huyu sasa ni programmer halisi ambaye yeye maisha yake yote ni coding(hapa pata kufaa kama unataka kuwa programmer) utakuwa na uwezo wa kutengeneza system na software katika hali ya kiwango cha juu maana masomo utakayo fundishwa kwa asilimia kubwa yanaendana na programming, na

(iii)Information System Management - hapa wanatolewa 'project manager, system analyst, system tester, n.k) waliobobea katika kuongoza, kusimamia, kujaribu na kufanya tafiti juu ya utengenezaji wa system na software projects.

Ukisoma CS utakuwa na uwanja mpana wa kusoma matawi yote hayo lakini hataweza kusoma kiundani labda ujiongeze kwa kusoma zaidi mwenyewe ili uweze kuwa na sehemu ambayo utamudu vyema. Nimalizie na

Information Technology (IT) - anayesoma hii kozi anakuwa advanced user wa system, software na mifumo ya mawasiliano ilizotengenezwa, anakuwa speed katika kutumia, kutambua makosa na hata kurekebisha hayo makosa, hapa kunafursa kubwa kwa mtu ambaye anautundu fulani katika kujifunza teknolojia na anaweza kujiendeleza. Na ndipo penye fursa zaidi hasa katika nchi zinazoendelea hata wanaosoma kozi hizo zingine mara nyingi wanaangukia hapa. Ndio maana mtu akisoma kozi ya computer anaitwa IT.

Information System Management na Information Technology zinampa fursa mtu ambaye hana uwezo mkubwa katika mathematics kusoma(Sio vyuo vyote vinatoa hiyo fursa kulingana na mtaala wao) lakini hizo kozi zilizobaki, there is no mercy for the mathematics unahitajika uwe konki kidogo wa math.

Hizo kozi zote zinawezesha mgawanyiko mzuri wa majukumu katika Information and Communications Technology (ICT) industry. Lengo likiwa ni kurahisisha matumizi computer na network systems kwa watumiaji wa kawaida. Hivyo kozi zote zina umuhimu mkubwa katika kuendeleza ICT.

Huo ndio uelewa wangu mdogo kuhusu hizo kozi lakini yapo mambo mengi zaidi ya hayo.
 
Correct👍👍👍
 
Umetafsiri vizuri sana ila ujawedha kumsaidia mdau. Mana pamoja na kujadili matawi yote. Hizo kozi zinatolewa tofauti tofauti kwa maaana kwamba haiwezekana kila moja ina mkazo wake kifani. Sasa swala hapa afanye kipi kitakachoweza kumsaidia kimalengo !?
 
Anasoma IT by professional
 
Kozi inayomfaa zaidi ni Software Engineering ingawa anaweza kusoma kozi nyingine lakini itahitajika ajiongeze kufikia malengo yake.
 
maswala ya programming mwambie Software Engineering ila kama ni security kuna CS(Computer Security)
 
Nimepata kitu hapa
Asanten kwa msaada wenu
 
uko vzr
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…