Msaada: Tigo hawataki kunirejeshea jumla ya Tshs 326,000/=

Msaada: Tigo hawataki kunirejeshea jumla ya Tshs 326,000/=

mwanadube

Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
79
Reaction score
21
Wanajanvi naombeni msaada tarehe 12/10/15 nilifanya malipo ya Dstv kupitia tigopesa muamala Bp.151012.1447.B348209164 yenye thamani ya tsh 146,000 lakini hayakuingia kwenye a/c yangu ya DSTV.

Tarehe 23/10/2015 nilikosea namba ya wakala nilitoa tsh 180,000 muamala CO.151023.1258.G671043053. Tangu tarehe 12/10/15 nimewapigi tigo huduma kwa Wateja zaidi ya mara 15 majibu yao ni subiri baada ya masaa 24 pesa yako itarejeshwa.

Nimeenda Tigo shop Mlimani, Uchumi, Ocean road na Buguruni majibu ni subiri baada ya masaa 24 .

Ndugu zangu, naombeni msaada ili pesa zangu zirudi kwani tangu tarehe 12/10/2015 biashara yangu ya kuonyesha mpira ligi kuu uingereza imesimama.

Nawasilisha..
 
Tigo hawathamini wateja wao hata kidogo.. Mimi nilifuatilia elfu 92 miezi miwili bila mafanikio..hawana Ishu hovyo sana
 
Wewe kama mimi tu wamekataa rudisha pesa yangu nimewapgia nara zaidi ya 20 naambiwa nisubiri 24 hours ikanibidi niende ofisini kwao pale kibo complex tegeta nikaambiwa utarudi within 48 hours now ni zaidi ya mwezi nimeachana nao
 
Wapeleke mahakamani mkuu mana Wamezidi, sasa kwanini wasikupe pesa yako
 
Kuwa Mvumilivu miw mpaka nikasahau nikashangaa napigiwa simu nikarudishiwa.wanachokifanya wana hold ile pesa kwa muda kuona kama yule uliemtumia atakuja kudai wakiona kimya wanakurudishia🐒
 
Kuwa Mvumilivu miw mpaka nikasahau nikashangaa napigiwa simu nikarudishiwa.wanachokifanya wana hold ile pesa kwa muda kuona kama yule uliemtumia atakuja kudai wakiona kimya wanakurudishia🐒

Kuihold siyo tatizo, kinacho chukiza ni unapoambiwa tatizo lako litashughulikiwa within 24hrs, ni bora wakakwambia subiri baada ya miezi mitatu then unajua nini cha kufanya.
 
Tigo hawajali wateja kabisa hata hiyo haiwezi kuwa agenda ya muda mrefu hapa. Tigo ni janga kama kimbunga tu
 
Kuwa mvumilivu kaka zitarudi tu kwani mie ilinitokea hiyo kuanzia tarehe 23.9 wamerudisha tarehe 17. 10 mwaka huu na nilitoa taarifa mara 5 na kwenda tgo shop so kuwa mvumilivu sema itarudi kipindi ambacho haukutarajia
 
Hawa jamaa wanamchezo mchafu Sana,ni wasumbfu mno kwenye miamala inapokosewa na hawajui pengine mtu alikuwa na shida gani na haraka kiasi gani, wanakera Sana, hapa kunaweza kukawa na wajanja ambao unapopata Tatizo km Hilo wanazuia hyo hela then ukishakata tamaa wanaipiga! Binafsi iliwahi kunitokea nkawachana live ndipo wakarudisha!
 
Kuwa mvumilivu kaka zitarudi tu kwani mie ilinitokea hiyo kuanzia tarehe 23.9 wamerudisha tarehe 17. 10 mwaka huu na nilitoa taarifa mara 5 na kwenda tgo shop so kuwa mvumilivu sema itarudi kipindi ambacho haukutarajia[/
QUOTE]

Nashkuru sana kwa kunipa matumaini
 
mimi walitaka kunidhurumu laki 230000
siliwafungia busta. ckutoka oficn kwao mpaka wanafunga nikawaambia mm ctoki nalala humuhumu. mbona waliitoa
 
mimi walitaka kunidhurumu laki 230000
siliwafungia busta. ckutoka oficn kwao mpaka wanafunga nikawaambia mm ctoki nalala humuhumu. mbona waliitoa
Khaa!! Hii safi sana. Sifa ya mwanaume ni kukomaa hasa. Siyo kulialia tu kwenye wakati hata mkataba wako na tigopesa sisi hatuujui. Namshauri mwanadube naye abebe maji na mikate aende kwenye ofisi zao aweke kambi hadi apewe chake :angry:
 
PM namba ya simu nikusaidie,ila kuna 10%,,kama uko tayari
 
Nawashukuru sana wadau kwa wote mliochangia,kwani mida ya saa saba mchana nimepigiwa simu toka tiGO wakiniomba msamaha kwa yote yaliyotokea na tayari muamara wa tsh 180,000 WAMENIREJESHEA bado ule wa 146,000 kwenda Dstv wameahidi kushughulikia Mara moja. Akhsanteni sana wana JF.
 
Nawashukuru kampuni ya Tigo kwa kuweza kurejesha kiasi cha tzs 326,000 kwenye a/c yangu.Nawashauri waboreshe kitengo cha Huduma kwa wateja kwani baadhi ya wafanyakazi hawatekelezi majukumu yao kwa sababu wanazozifahamu, either wanafanya kazi kwa mazoea au wamejisahau na kujiona bila wao kazi haziendi kitu ambacho kinasababisha malalamiko mengi toka kwa wateja yasiyokuwa na sababu
Nawatakia Kazi njema.BADIRIKENI tiGO KITENGO CHA HUDUMA KWA WATEJA.
 
Back
Top Bottom