Msaada: Tatizo la kujaa internal storage ya simu

Ingia setting - app...force stop app zote ambazo hutumii ,futa caches data,unaweza kuwa games app zinakula sana space,futa zipakue unapotaka kucheza ukimaliza kucheza futa, video zote za kupakua zielekeze kwenye sd card.uwe una safisha RAM mara kwa mara,pia pakua RAM play store,inasaidia kiasi fulani kutuliza simu.
Kama unatumia facebook tumia ile facebook lite,ile facebook ya kawaida ni janga kwa simu yenye RAM ya 1gb na internal ya 16 gb
Kwa fb kweli natumia ya kawaida,, kuna tatizo naliona kwenye storage setting nimeelekeza videos kwenye SD card lakini cha ajabu zinaingia kwenye internal phone storage kitendo ambacho kimepelekea kufanya kuhamisha videos na documents kubwa na kuzihamishia kwenye SD card
Screenshot_20190703-090551.jpeg
 
Mkuu natamani kweli kurudi hapa kushukuru! BTW shukrani kwa hatua hii ya kwanza
 
Internal storage inajazwa na vitu unavotuma (picha na videos) kwa watu /groups za whatsapp. Vitu unavotuma huwa havifutiki kwenye storage hata kama utafuta kwenye gallery yako. Chakufanya ingia kwenye internal storage yako Kisha tafuta folder lenye jina whatsapp. Lifungue ndani Kuna folders nyingine. Fungua lenye jina media,lifungue utaona folders nyingine zenye picha, video, documents nk. Nk. Futa sent items zote kwenye kila folder nililo taja Kisha urudi kushukuru hapa .

HOPE I HAVE INFORMED YOU ENOUGH
Asante mkuu
 
Pia nenda kwenye folder nenda kwenye WhatsApp tafuta sent folder delete,tafuta status folder delete,audio sent folder delete kasimu katakua kepesi kama karatasi
 
Back
Top Bottom