msaada tafadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

msaada tafadhari

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Bizzly, Sep 1, 2010.

 1. B

  Bizzly Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  wana JF kuna jamaa yangu alikuwa anamsomesha mtoto yatima, maendeleo ya yule mtoto hayakuwa yakuridhisha hata kidogo darasani. akatakiwa kurudia kidato cha kwanza au kuhama, akahamishwa na kutafutiwa shule ingine lakini kule pia ndo akafanya vibaya zaidi. kwa kuwa huyo jamaa alikuwa ni mlezi tu akaamua kujitoa kwa maana ya kutomlipia ada na mpaka sasa haendi shule.

  Je, kuna sheria yoyote inayomlazimisha mlezi huyo kuendelea kupoteza hela yake kumlipia?

  Nini haki ya pande zote?

  naomba kuwasilisha kwa msaada wa mawazo
   
 2. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kama alijitolea kumsaidia kwa hiari yake mwenyewe, alipoona elimu ya sekondary imemshinda mtoto huyo, alitakiwa kufikiria njia nyingine ya kuendeleza maisha ya mtoto huyo ili aje aweze kujitegemea hapo baadae, ampeleke mtoto huyo ufundi ajifunze shughuli za mikono.
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Hata kama kuna sheria au hakuna sio ishu cha muhimu atumie ubinadamu ule ule alioutumia kuanza kumsomesha kwa kumtafutia elimu mbadala. Hasitafute visingizio vya kujitoa katika msaada aliojicommit. Ila nampongeza sana kwa ujasiri wake wa kujitolea kumsomesha huyo mtoto
   
Loading...