Habarini za jioni ndugu na wanajamvi wenzangu, poleni na mihangaiko ya siku nzima. Natumaini salamu zangu mmezipokea.
Nimekuja kuomba msaada wa ushauri wa kitaaluma kwa anayefahamu kuhusu suala lifuatalo. Nina mdogo wangu amemaliza form 6 mwaka huu, namshukuru Mungu amefaulu vzuri na kapata Division One ya Point 9 kwenye combination ya HKL.
1.Hivyo basi naomba kupata msaada, kama kuna anafahamu ni kozi zipi za sanaa zinazopewa mkopo ??
2. Na alama zake hizo, kozi gani nzuri kwajili yake mdogo wetu.
Natanguliza shukrani wakuu [emoji4][emoji4]