Kusini pride
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 1,762
- 4,070
Nilimuachisha chuo, Mke wangu kagundua, ana Mimba mapacha watatu! Msaidie afungue biashara huko kwao!
Nahisi kuchanganyikiwa na sijui nifanye nini, kuna huyu binti niko naye kwenye mahusiano kwa miaka 5 au 6 sasa. Wakati nakutana na huyu binti alikuwa yuko chuo, na mimi nilikuwa nataka mtu wa kunisimamia biashara zangu, nilimuona nikaanzisha naye mahusiano, akawa anakuja dukani kwangu kipindi cha likizo, nilikuwa namlipa lakini baadae tukaingia kwenye mahusiano.
Alikuwa ananifanyia kazi vizuri ukizingatia nishafukuza wafanyakazi zaidi ya 10 hivyo nilimshawishi aache chuo ili asimamie biashara.
Ili kumuaminisha kuwa nitamuoa nilimtafutia TIN namba nikafungua na duka ambalo anatumia TIN yake lakini mzigo wote nilikuwa nikicontrol mimi hivyo nilijua hata tukigombana akitaka kuniacha nitatafuta fuso nipakie mzigo wangu wote na kumuacha na TIN namba yake kwani hata fremu ilikuwa ni nyumba yangu.
Aliniamini kweli, nimemshawishi mpaka akaacha chuo alikuwa anasomea udaktari alikuwa mwaka 3, hivyo tukawa tuko dukani.
Maisha yaliendelea na hakukuwa na shida, mwaka jana mke wangu alihisi kuwa nachepuka, na kwa ninavyomjua mke wangu nilijua atachunguza tu, hivyo harakaharaka nilimuambia binti kuwa anataka mtoto. Nilimuambia akaniambia nishakufanyia mambo mengi namna hii kwanini usinizalie, alinambia niende kwao kujitambulisha nikasema hamna shida, nilitafuta watu wawili tukaenda kujitambulisha ila nilimuambia siatoi mahari mpaka anizalie. Hata hatukuhangaika alibeba mimba na sasa hivi yuko kwao kujifungua.
Sababu ya kuja kwako ni hivi, mke wangu keshajua kuwa kuna mwanamke mwingine.
Anatishia talaka kashafungua na kesi mahakamani, mwanzo nilijua mke wangu hana ubavu wa kuniacha ila amekasirika baada ya kusikia yule binti nimefungulia duka ila kiuhalisia ni muuzaji tu. Hivyo amenambia kama nataka ndoa yangu basi binti asirudi dukani, kwa hali ilivyofikia najua mke wangu tukiachana ni hasara kwani kuna mali nyingi tumechuma naye pia ni sehemu ya biashara yangu.
Nimekubali kuachana na huyu binti na hatarudi tena dukani, shida ni kwamba tulishaangalia ana mapacha na si mapacha wawili bali ni watatu. Kwao wanajua keshamaliza chuo ila anahangaika kutafuta kazi, inamaanisha wanajua ni daktari tayari kwani sisi tuna miaka 5 na mimi nilianza naye akiwa chuo mwaka wa 3.
Nataka nimtumie mtaji kidogo ili akafanyie maisha huko kwao asirudi huku kwani hamna kitu