Msaada tafadhali

resonanceiduufu

Senior Member
Jul 29, 2016
112
62
Nina rafiki yangu Mwalimu, aliambiwa kwa mdomo na Kaimu Mkuu wa Chuo kwamba tarehe 04/11/019 anapaswa kwenda semina iliyopaswa kufanyika Morogoro tarehe hiyo, (aliambiwa kabla ya week 1 ili ajiandae) na akapigiwa simu na aliyepaswa kumpokea na kuongoza semina kwamba aje tarehe hiyo tajwa.

Semina ilipaswa kuanza taehe 04 mwezi huo tajwa juu ambayo ilikuwa jumatatu hivyo aliamua kuanza safar asubuhi kuelekea Moro, lakini akiwa anakaribia Dar es salaam, simu ilipigwa toka Morogoro na aliyepaswa kumpokea huko Morogoro kwamba semina imeahirishwa. Ikabidi rafiki yangu akubaliane na hali ila akaomba kurejeshewa pesa yake ya nauli, chakula na hotel (kwani asingeweza kurudi siku hiyo x2).

Rafiki yanu aliamua kumpigia simu na kumweleza madai yake yote Kaimu Mkuu wa Chuo na hivo kuomba msaada wa hizo gharama kwani asingeweza kugharamikia cost zilizojitokeza ghafla. Kaimu hakujibu chochote kuhusiana na kurejesha costs lakini aliishia kusema acha tuone tutafanyaje kwani naye ni kama hakujua kama imeahirishwa.

Rafiki yangu alilala Dar hotel siku hiyo huku akijua kuna msaada kesho kutoka kwenye Mamlaka atapata ili alipie chakula ya usiku na hotel, lakini hakupata msaada wowote kwani Kaimu Mkuu wa Chuo hakuwa anajibu tena sms.

Ilimlazimu kubaki Dar tena kwa siku nyingne ambayo ni jumatatu kwani hotel hawawezi kumruhusu aondoke bila kuwapa chao. Hivyo alikaa siku 5 (jumatau - ijumaa) akisubiria msaada kutoka kwa waliompangia safari bila mafanikio. Aliamua kukopa kwa ndugu jamaa na rakifi ili alipe na aruhusiwe kurudi kituo cha kazi endelee na majukumu japo ameshapata deni kubwa sana kwa waliomkopa.

Alipofika chuoni Jumatatu nyingine hakuulizwa alikuwa wapi wala hakuna aliyemuuliza nini kimekupata. Badala yake alitumiwa barua iliyoletwa na walimu wawili wakisindikizana ofisini kwake iliyosomeka "WARAKA WA NDANI. Unatakiwa kueleza sababu za kutokuwepo kituo cha kazi kwa muda wa siku 5" .

Alipaswa aijibu na aipeleke kwa Mkuu wa Chuo na barua hiyo iliandikwa na aliyekuwa Kaimu kipindi anaambiwa kwenda semina wakati Mkuu wa Chuo mwenyewe yuko ziara ya kikazi. Aliijibu barua na kukiri na kuomba kurudishiwa gharama zake ila mpaka sasa haijajibiwa.

Note: Kumekuwa na zoea la kuwafanyia wafanyakazi wengine hivyo, Na mwishowe inaishia tu kuwapa "Waraka wa Ndani" na kuwatishia na barua na maneno kama hayo kwamba utakatwa mshahara n.k

NAOMBENI MSAADA TAFADHALI
Je, kuna uwezekano wa kulishughulikia suala hili zaidi ya hivi tu kujibu barua na mwishowe iishe juu kwa juu, au anaweza kufanya nini ili akomeshe tatizo hili?

Nawasilisha!
 
Ngoja wajuzi waje.
 
Back
Top Bottom