Msaada tafadhali

Big5

Member
Sep 25, 2014
34
14
Habari za leo ndugu wa jamii forum, naomba atakaye weza kunifafanulia hili na kunielekeza nini cha kufanya.
Mimi nilikuwa mwalimu wa leseni kwa jina lingine course hii ilikuwa inaitwa crush program. Nilibahatika kusoma degree ya uhasibu mwaka 2010-2013 baada ya kumaliza niliomba kubadilishwa kutoka kwenye kada ya elimu ila nilikataliwa kwani ajira yangu ilikuwa niya temporary, hivyo nikashauriwa nikasome post graduate ya ualimu hivyo basi mwaka 2015 nilianza kusoma post graduate na nikahitimu mwaka 2016. Baada ya kumaliza nilienda kwenye halmashauri ninayofanyia kazi kuomba kubadilishiwa muundo wa mshahara nikajibiwa hakuna kinachobadilishwa kwani system imezuiwa.
Cha kushangaza mwezi wa tisa mwaka huu sikupata mshahara kwenda kuuliza naambiwa nimetolewa kwani nilikuwa mwalimu wa leseni.
Naomba msaada atakaye weza kunielekeza vizuri nifanye nini ili nisipoteze ajira ya serikali kwani naipenda na familia inanitegemea.
 
Mkuu sipo katika kada ya Ualimu?Naomba Nifafanulie maana ya Uhalimu wa leseni..
 
Jaribu kwenda utumishi mkuu kama una nyaraka zote muhimu ukaongee nao uone mnatatua vipi hili suala
 
Siyo uhalimu ni ualimu, ni course ya muda mfupi kwa mafunzo ya ualimu.

Ndio wale walimu wa voda fasta ile program ya Lowasa akiwa PM?

Pole sana wenzako wajanja walishajiendeleza kuanzia na diploma toka enzi hizo sasa hivi wengine wana degree za ualimu na ni walimu rasmi.

Ila wakigoma kukurudisha tumia degree yako ya uhasibu kuomba kazi za uhasibu upya, awamu ya tano inatufundisha mengi sana.

Karibu sana mtaani mkuu.
 
Back
Top Bottom