Msaada tafadhali wa vilainisha koo, nataka niwe na sauti nyororo

Lis

JF-Expert Member
Jun 2, 2012
471
346
Imenilazimu kuomba msaada wenu wa Hali na Mali, mnisaidie kunambia kitu kitakacholainisha koo langu ili niwe na sauti nyororo isiyo na Mikwaruzo.

Ofisi yangu imeniteua kusoma risala katika hafla flani hivi, hivyo mnambie ninywe nini ili niweze kulainisha koo langu?
 
Kunywa asali itasaidia. Ila huo mkwaruzo ni ea siku zote au kuna sababu...
 
'Huitaji' kuwa na sauti nyororo. Ongea tu na DJ wa hafla hiyo akuweke kwenye autotune. Sauti itayotoka hapo unachagua mwenyewe. Uongee kama Celine Dione, Shakira, Rihana au Beyonce, uchaguzi ni wako.
Teknolojia ni noma sana.
 
Imenilazimu kuomba msaada wenu wa Hali na Mali, mnisaidie kunambia kitu kitakacholainisha koo langu ili niwe na sauti nyororo isiyo na Mikwaruzo.

Ofisi yangu imeniteua kusoma risala katika hafla flani hivi, hivyo mnambie ninywe nini ili niweze kulainisha koo langu?

Hao waliokuteua waliangalia vigezo gani toka kwako?? Yaani pamoja na mikwaruzo kama gari bovu bado tu umepewa wewe hilo jukumu?? Una uhusiano gani na bosi wako kwani??.
 
Back
Top Bottom