Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

Msaada tafadhali, napitia wakati mgumu sana

Pole sana mkuu.

Sisi wanaume tumeumbwa kukutana na majanga ya hawa jamaa (ke) japokuwa wengine hawajawahi pitia.

Kwa kifupi tu unaumia sana maana ulimpenda ila yeye alikuwa anakutumia. So utakuwa na kipindi kigumu kwa muda tu na baadae utazoea. Achana nae kabisa coz tayari amerudiana na x wake walioishi kwa miaka 10 kama sikosei kwa upande mwengine ulikuwa unachepuka na mke wa mtu.

Jihesabu unaanza maisha mapya kama vile umetoka jela. "K" zipo nyingi sana na maisha ni kupambana. Usijione umefeli maisha ni kipindi cha mpito tu as longer as uko fiti. Chapa kazi tafuta hela.
 
Umepewa lifti unataka kupga na honi acha ubwazaza songa mbele bado kijana utapata wengine wengi t Kama hao
 
Mkuu Ni story. Ndefu nimeacha mengine nkajua ntayakuta kwenye maswli na ufafanuzi!! Mm kuaxhwa nimekubali mbali na huo msaad nliompa pia Kuna vingi tu nimemfanyia kwa huo muda mfupi nilikutana nae,! Kibaya aliniaminisha Hadi nkamtambulisha kwa wazazi na yeye akanitambulisha kwao kumbe alikua na lake moyoni!! Sijamkosea kitu na imekua gafla sana
Waambie wazee huyo demu alishakufa

Kama watakuuliza
How mtuu ndani ya mda mfupi unamtambulisha kwenu

Nb
Umri wako tafahdali kama huto jali
 
Ulivyoanza nikajua uko kwenye matatizo kweli kumbe utopolo tu. Tatizo unapenda kulelewa mkuu.
Achana naye, Jikaze, utazoea utasahau.
 
Sasa wewe mwanaume yuko nje anafanya fujo na wewe humo ndani unajificha na kuchungulia , yani ulionwa bwege kuliko kawaida, ata kama ni uoga sio hvyo, ata bitty tu umeshindwa, kweli wewe fara
 
Sasa wewe mwanaume yuko nje anafanya fujo na wewe humo ndani unajificha na kuchungulia , yani ulionwa bwege kuliko kawaida, ata kama ni uoga sio hvyo, ata bitty tu umeshindwa, kweli wewe fara
😀 😀 😀jamaa demu alimuona falaa snaaaa
 
Huyo we jitahidi tu kuachana nae. Huyo mwanaume alienae ipo siku tu atamletea tena visa na ndo hapo wewe utaibuka mshindi. Just relax
 
Single maza,mwanamke aliyekua kwenye uhusiano na mwanaume zaidi ya miaka 5,hapa na maana kwenye hyo miaka 5 walikua wanachakatana bas usije ukawaweka moyoni hzo type mbili za wanawake,ni rahisi kurudiwa na maex wao!!
 
Wazee nakuja kwenu nikiomba ushauri,

Kama kichwa cha habari kinavyosema japo mimi sio mtaalamu sana wa kuandika nitajitahidi kuandika machache na ya muhimu, mwaka 2018 nikiwa kwenye safari zangu za kibiashara nilikutana na mwanamke mmoja tukiwa tumekaa siti moja kwenye bus tulilokua tunasafiria pamoja!!

Tulipofika kwenye kizuizi sehemu flan gari ikasimamishwa kwa ukaguzi, kumbe yule mwanamke alikua na mzigo wa magamu(magendo) na akatelemshwa hapo beria.

By then tulikua tushapeana namba za simu na nikataka kujua kulikoni ndipo aliponisimulia mkasa wake na akaniomba nifikishe taarifa kwa ndugu ambaye alinipa namba yake na maelekezo yote!!!

Hata nilipomtafuta yule bwana hakua tayari kuonyesha ushirikiano na yule mdada akawa Hana namna ila kuomba msaada wangu Kama naweza kumsaidia, baada ya michakato yote kufanyika ikawa inahitajika laki 5 ambayo alikua amepungukiwa ili amalize tatizo lake.

Mimi nkaamua kumsaidia kiroho Safi na akatoka ndani , mwanzonii mwa 2020 nkapata kesi ya uhujumu uchumi iliyoniweka gerezani mwaka mmoja na miezi Saba, yule dada nlimpa taarifa siku nakamatwa(alishakua rafiki yangu lakini sio kimapenzi) katika mwanzo wa kesi yangu Hadi natoka gerezani nlikua nae bega kwa bega na hakuna siku hata moja alikosa Kuja kunisalimia nkiwa gerezani (NB gerezani wanasalimiwa siku za wikend tu)

Mungu akasaidia kesi ikaisha na nkatoka, yule dada akanikaribisha nyumbani kwake na katika muda huo wote nlikua sijawahi kufika nyumbani kwake!! Nkakuta anaishi mwenyewe na akaniambia Ana miaka 2 hayuko kwenye mahusiano na pale anapoishi Ni nyumbani
kwake hajapanga

Basi nkatumia nafasi Ile kumuomba awe mwenzangu na akakubali !! Tumekaa kwa upendo na furaha nkiwa naenda kwake kila napohitaji hata Kama Ni usiku wa manane namkuta Yuko peke yake!!

Lakini alishaniambia huko nyuma alikua kwenye mahusiano na mtu japo waliachana sababu ya changamoto za maisha ya hapa na pale Basi kidume nkashika usukani

Yule X wake anasema waliishi pamoja miaka 10 lakini hawakua kwenye ndoa , waliishikimada tu, na walikua wameachana miaka imepita 2 Sasa Hadi mm nakutana nae kimapenzi

Siku moja yule X akapiga simu , akamwambia nasikia una mwanaume hapo nyumbani, Sasa Leo nakunywa KVANT nakuja kukufanyia fujo hapo kwako!! Nkamwambia yule mwanamke huyu X wako Kuna kitu anakudai hapa au alikusaidia kujenga hii nyumba?? akaniambia hajawahi hata kuninunulia glass hapa ndani, vitu vyote Ni jasho langu, Basi nkamwambia Kama Ni hivyo hawezi Kuja Ni mikwara tu!!

Ilipofika saa 5 usiku yule bwana akaja, kumbe alimaanisha, akafanya fujo anapiga madirisha na milango ikawa fujo kubwa wakati huo sisi tuko ndani tumefunga mlango

Asubuhi nkamtaka akaripot police akasema hawezi kumuweka ndani maana Kuna mazuri alimfamyia wakiwa pamoja Ila atamuonya asirudie! Jioni yake akanipigia simu akaniambia nimepata ushauri kwa watu wazima wamesema hapa kwangu nisilete mwanaume, kwa hiyo kuanzia leo usije hapa labda Kama Ni kukutana tukutane juu kwa juu!!

Nkasema sawa sitakuja Wala usiwe na Shaka kuhusu Hilo!!! Nkamuuliza au ndo unamrudisha x wako akasema yule siwezi kurudiana nae maana aliyonifanyia Ni makubwa!! Ntakua na wewe tu Ila nyumbani ndio usije maana namuogopa akisikia Tena uko hapa atakuja kunifamyia kitendo kibaya maana namfahamu Ni mkorofi.

Basi mm nkaamua kukaa kimya Ila Mara kwa mara akawa ananichokonoa kwa msg na simu akitaka tuonane, na mm nkajaa maana niwe mkweli nlijikuta nampenda Sana huyu mwanamke!! Juzi nkampigia simu hakupokea na sio kawaida yake , meseji hajibu nkasema huyu labda atakua na mwanaume ndani !

Nkaenda kwake kufika dirishani nkakuta anaongea na Yule x wake kwa simu ananisengenya na kuniongelea vibaya!! Nkamwambia fungua mlango na kweli akafungua tukiwa ndani nkamuhoji Kama anataka kuendelea na mm au anarudi kwa x wake akasema ananitaka Mimi!!

Basi ukatokea ugomvi Kati yangu na yeye na asubuhi akaita watu wazima tukasuluhisha , jioni hii Nimempigia simu kapokea yule x wake Ila kaongea kistaraabu tukamaliza , baadae nlipopiga Tena akapokea mwanamke akasema bwana yangu ameenda kazini ,namsubiria aje tulale Mimi nlikua na wewe sababu ya shida tu!

Nikihesabu garama na muda ambao nimeuwekeza kwake afu Leo anakuja kunilipa jeuri nakosa Raha kabisa hapa najiuliza nimfamye Nini huyu mwanamke?? Na nitoke vipi kwenye hii Hali niliyonayo maana roho Inaumia Sana , nahisi nlikutana nae naweza kufanya tukio baya maana amenifanyia usaliti mkubwa Sana.

Nawasilisha wakuu naombeni ushauri wenu
Pole sana
 
Kama kuna watu wamesomea saikolojia humu msaidieni huyu jamaa, nati zimeanza kulegea kichwani. mpeni pia pole kwa kesi za uhujumu uchumi, huko gerezani alikutana na nini hadi kuwa wa namna hii?
Hahaha
 
Back
Top Bottom