Msaada tafadhali kwa Mwanangu Sharon | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada tafadhali kwa Mwanangu Sharon

Discussion in 'JF Doctor' started by Baba Sharon, Oct 29, 2011.

 1. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Tafadhali naomba mwenye ujuzi au uelewa wa hili anisaidie.........Mwanangu amekuwa na tatizo la kuanguka na kupoteza fahamu na limekuwa na tarehe maalum ni kati ya tarehe 15 na 27 au 26 na 28 ya kila mwezi.

  Kwa mfano tatizo hili lilimuanza terehe 27 ya mwezi wa Saba mwaka huu na limekuwa likiendelea hivyo mpaka jana alipoanguka tena. Mwezi wa nane alianguka mara mbili yani tarehe 16 na 28 mwezi huu hivyo hivyo. Sasa nashindwa kuelewa tatizo ni nini.......

  Alipelekwa hospitali baada ya kuanguka na alipimwa daktari akasema hana kitu chochote kinachomsumbua akampatia dawa za maumivu akarudishwa nyumbani.......

  Mwezi wa nane alipoanguka akapelekwa tena akaambiwa kuna uwezekano wa mtoto kuwa na degedege akapatiwa vidonge lakini cha kushangaza jana tena kaanguka na vidonge alitumia.

  Tafadhali naombeni msaada wenu kama kuna yeyote mwanae aliyekumbana na tatizo hili au hata la degedege.......Kwa kweli sina uzoefu mkubwa wa kulea watoto maana huyu ndiye wa kwanza.

  Na daktari anasema hili tatizo likiendelea litamletea mtoto kifafa naomba Mungu aipushie mbali hili.........

  Kuna nurse mmoja aliniambia labda kuna mtu alimwangalia mtoto na jicho baya sasa nachanganyikiwa maana uhusiano wa kuangaliwa mtoto vibaya na kuanguka kwake upo wapi na kuna ukweli wowote kuhusu hili?
   
 2. Mupirocin

  Mupirocin JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,596
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Anaumri gani, akianguka anapresent vipi na alipozaliwa alikuwa na shida yeyote na je kwa sasa anapoangaka anapata homa, akianguka anazinduka baada ya muda gani. Je baada ya kuzinduka anajikojolea au kutoa kinyesi. Hebu tueleze haya ili tukushauri cha kufanya.
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Pole sana ndugu, mwanao ana umri gani?...
   
 4. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Mtoto ana Miaka miwili na alipozaliwa hakuwa na shida yeyote mpaka July ya mwaka huu alipopata hilo tatizo.Mwezi July alipoanguka alizimia kwa kama dakika 25na ile jana haikuchukua muda mrefu hata dakika kumi hazikuisha akazinduka...........Huwa anapata homa anapozinduka na huwa hakojoi wala kutoa kinyesi..........Ntashukuru kwa msaada wako mkuu
   
 5. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Asante dada yangu..........ana miaka miwili na miezi mitatu
   
 6. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
   
 7. Baba Sharon

  Baba Sharon JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  Huenda ni kweli amepatikana Upepo Mbaya wa Shetani mchafu Mapepo wachafu waemkumba huyo mwanao pol sana Fanya hivi kama upo

  Dares-Salaam nenda maduka ya dawa yaliyopo hapo Kariakoo waulize Wauza hayo Madawa ya Kiarabu Wapemba hao Dawa inayoitwa (Nyungu ya Pwani) ni aina fulani ya Takataka zinazotoka nje ya Bahari ufukweni pamoja na Dawa zingine mchanganyiko watakupa na na waulize dawa inayoitwa Mavi ya Tembo, Mavi ya Punda, hayo Mavi ya Tembo na Mavi ya Punda utachanganya pamoja na kumfukiza huyo mtoto wako kwenye kaa la moto huku kajinfunika shuka nyeupe mpya kwa muda wa siku 7 asubuhi na jioni umfukize mtoto wako.
  Na Kuhusu hiyo Nyungu ya pwani Ukifika nayo nyumbani hiyo dawa ya
  nyungu ya pwani iweke katika chombo kikubwa kama Sufuria kubwa weka ndani yake maji ya kawaida uifunike kwa juu kisha weka katika moto mkali uichemshe kwa muda wa Masaa 2

  kamili kisha umwambie mama yake na mwanao avue nguo zote abaki na chupi na sidiria kama ni mwanamke kama ni mwanamme awe na chupi kifua wazi wajifunike hiyo shuka nyeupe mita 2 umfunulie hiyo dawa ili wapate kuvuta mvuke wake kwa muda wa dakika 10 ufanye hivyo kwa muda wa siku 7

  Asubuhi na usiku uanze siku ya jumapili inshallah matatizo ya kuanguka anguka yatapotea na huyo pepo mchafu aliye mkumba mtoto wako atakimbia mwilini mwake. Na jambo lingine utafute Dawa hizi za atumie kwa kula uchanganye na Asali kipimo chake ni nusu kilo

  Dawa zenyewe tafuta hizi hapa

  Kamun Aswadi,gramu 25 kamun abiyadhi gramu25, pilipi mtama gramu 25,karafuu gramu25,tangawizi kavu gramu25, iliki gramu25, Habati Soda gramu25, na Haltiti gramu gramu10 hizi Dawa zote uzitwange uchekeche upate unga wake uchanganye na Asali safi ya nyuki nusu kilo uwe unampa Mama yake hizi dawa ndio ale sio mtoto kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali asubuhi kabla ya kula kitu na mchana kijiko kimoja

  kikubwa cha kulia wali na usiku kijiko kimoja kikubwa cha kulia wali atumie hiyo dawa kwa muda wa siku 7 inshallah hayo matatizo yake mtoto wako ya kuanguka anguka yatakwenda zake kwa uwezo wake Mwenyeezi mungu . fanya hizo dawa zote ziende sambamba tafuta hizo dawa uanze kuzitumia siku ya jumapili inayokuja kisha kama ni wewe ni Muislam mpeleke mtoto wako kwa

  Sheikh akamuombee Dua la kama wewe ni Mkristo pia mpeleke kwa Padri au Mchungaji akamuombee dua baada ya kumaliza hizo dawa fanya hivyo nakutakia mafanikio mema. Fanya Dawa kisha unipe Feedback.

  source: P.h.D. Mzizimkavu
   
 9. o

  omholo Member

  #9
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana, matibabu yatategemea nini chanzo cha tatizo ni vema ukampeleka huyo mtoto kwa DK.bingwa wa watoto kabla tatizo halijawa sugu,lakini kuna mambo yanayoweza kuchangia kuanguka na kupoteza fahamu mf.kama kwenye ukoo kuna mtu alikuwa/ana kifafa anaweza kurithi,kama alipata magonjwa kama AIDs,meningitis,kuangukia kichwa na kupata shida kwenye ubongo,uvimbe kwenye ubongo,kupata shida wakati wa kuzaliwa hasa kwenye kichwa,mtoto kuwa na homa kali mara kwa mara bila kumpa dawa za kupunguza joto nk.
  kama kweli njia za kitaalamu zitashindikana peleka akaombewe kwa wachungaji kama ni pepo atatoka.
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole jamani mi sina msaada cjalea wala si dokta,ila nitaulizia kwa watu,poleni sana,mtoto ni kila kitu kwa mzazi
   
 11. twenty2

  twenty2 JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ninachokushauli kama kote umepita na imeshindikana basi rudi kanisani akaombewe ata kama ikiwezekana na nyinyi wazazi mkaombewe,basi ikishindikana na hilo shukulu mungu.
   
 12. Enny

  Enny JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Nenda pale Upanga Hospitali ya Family care kamuone Professor Matuja mtaalamu wa magonjwa hayo nina imani atakusaidia.
   
 13. twenty2

  twenty2 JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lazima usiwe na ushauri kwasababu ata avater yako inatisha
   
 14. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  ACHANA NA MAMBO YA KIHUNI NA MA IMANI. MAMBO YA KUJIFUNIKA SHUKA NA KUVUTA MOSHI. UMEJUAJE KAMA NI JINI AU MAPEPO?? TATIZO LENU NYIE WATU WA IMANI HAMNA HATA VIPIMO WALA UTAALAMU. HUJAMUONA HATA MTOTO UNAJIFANYA KUMWAGA UPUPU TU HAPA, ACHA KURUBUNI WATU...ETI TAKATAKA ZA BAHARI, MARA MAVI YA TEMBO....KU DADEKI TAMBAA KULE. SIWAPENDI SANA WATU HAWA..IMANI NI KAMA BANGE/MARIJUANA VILE. its my views

  well.
  naomba umpeleke huyo mtoto kwa dr. bingwa wa watoto atampa tiba maana wao wanakutana na hizo cases mara nyingi tu. mmojawapo wa madaktari bingwa ni DR MASAWE yupo hapo dar es salaam.
  usiwaze sana, fanya hima uhakikishe anaenda hospitali na si kuwasikiliza manesi bwana. komaa na tatizo mpaka litaisha na nzuri zaidi tatizo limeonekana akiwa mdogo ambapo akipewa dawa mapema atapona kabisa.
  pole sana
   
 15. twenty2

  twenty2 JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani ni pepo tu ndio linaombewa kwa wachungaji na usiamini kama ni pepo kuwa na imani ya kawaida duniani kuna majaribu mengi ya mungu,so sawa kaombewe lakini sio kwa kuamini kuwa ni pepo.
   
 16. twenty2

  twenty2 JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 296
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana kumbe ni mwenye umri mdogo hivyo,kwani ni mtoto wako wa kwanza?
   
 17. A

  Aine JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndg. Mpeleke mtoto kwa dr Massawe au kwa Dr Hameer pale kariakoo. Aidha mpeleke kwenye maombi Mungu atamsaidia achana na mambo ya kula mavi ni uchafu na kujilisha upepo soma Yer 32.27
   
Loading...