molwe
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 425
- 456
Habari za jioni wanajukwaa! Nahitaji kujuzwa kuhusu sheria hii: Abiria anaekaa kiti cha nyuma baada ya siti za mbele ni lazima afunge mkanda?? Maana nimekutana na utata leo jioni, kuna trafiki alinisimamisha abiria wangu wa nyuma hakuwa amefunga mkanda, kwa jazba kachukua leseni na kadi kapeleka kwa bosi wake nikalipe faini, nikamweleza bosi kuwa abiria asiefunga mkanda yuko siti ya mbele, akasema sina kosa akanirudishia vitu vyangu nikaondoka.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app