Msaada tafadhali kuhusu benki nzuri, nataka kufungua akaunti

Mr Mikazo

JF-Expert Member
May 26, 2016
1,586
794
Nataka kufungua account bank. Nimejaribu kuulizia vigezo CRDB nimeambiwa ila nahitaji kujua mambo kadhaa kabla sijafungua account.

1. Kati ya CRDB na NMB, ipi ni bank nzuri? Namaanisha masharti nafuu, makato unapoweka na kutoa pesa.

2. Vigezo vya kufungua account NMB ni vipi?

Nitangulize shukran kwenu ndugu zangu
 
mie naona CRDB wako vizuri kuzidi NMB. Hao NMB hata huduma zao ovyo wakati mwingine, pia wana tatizo la vijana wao wanaojua IT kuiba pesa za wateja kwenye a/c zao. hiyo bank tuachie sie makwabwela lakini sikushauri kuingia humu! pia foleni zao ni balaa halafu huwa hawana huduma nzuri kwa wateja (wanafanyia mazoea) usishangae teller anaona foleni ndefu wamefungua dirisha saa 2.30 asubuhi, halafu saa 2.45 yaani baada ya robo saa tu tokea afungue anafunga dirisha eti ANAKWENDA KUNYWA CHAI!
 
ahsante kwa taarifa mkuu
 
Mkuu hakuna benki nzuri kwa vigezo vya makato! Benki zote ni wafanyabiashara na mabepari. Kuhusu kufungua akaunti, vigezo ni vile vile kwani sheria inayotumika ni moja kwa benki zote. La msingi angalia benki iliyojirani na wewe, ambayo haina foleni, yenye mtandao wa kutosha wa matawi na ATM kurahisisha uwekaji na utowaji wa hela na pengine yenye huduma nzuri kwa wateja. Kwa vigezo hivi CRDB na NMB hazitofautiani sana.
 
Waandishi wa habari katika kufuatiria habari huvigawa vyanzo vya habari. Kuna "primary na second source". Katika suala hili sisi ni second jaribu kuwaona primary ili ufanye uamuzi ulio sahihi.

Uzuri wa bank huendana na Malengo uliyonayo katika kufungua akaunti. Wewe una malengo gani na hiyo akaunti yako.
Ubora wa huduma za NMB upo juu ya CRDB sema wateja wengi wa huduma za kifedha sio wateja bora.
 
Back
Top Bottom