Msaada tafadhali: Jinsi ya kupunguza ukubwa wa makalio kwa mwanaume

The pexie

Member
Feb 24, 2020
35
42
Habari ya majukumu wana JF.

Mimi ni mwanaume Aged 23 ni mtanashati (handsome kiasi ) lakini Nina tatizo la kuwa na makalio makubwa sana jambo ambalo limekua likiniondolea ujasiri (confidence) mbele za watu na hata mbele za wanawake.

Nashindwa kuvaa nguo za kuchomekea kwa hofu ya mchomozo wa makalio. Pia T-shirt Nashindwa Kuvaa kabisa nikihofia kujicholesha na Mara Nyingi navaa begi kusudi nipate confidence ya kutembea,Most times nakuwaa natembea Jioni ama usiku at least nakua free kidgo
Honestly ni jambo ambalo Lina niumiza Sana kufikia hata kulia,

Nimewahi kukonda Sana kwa mazoezi(jeshini) lakini pamoja na hayo kufanya mazoezi sana na kupungua mwiil kwa kiasi kikubwa lakini makalio hayapungui kwa kiasi kikubwa kama mwili unavyopungua.

Ombi langu Kwenu kwa anayejua DAWA Au SOLUTION yoyote nzuri ya kupunguza makalio atakuwa kanipa msaada mkubwa kwangu na watanzania wengine wenye matatizo kama hayo ambao hawajui tiba.

Ahsanteni
 
Huo ni uumbaji wa Mungu usiukosoe, Jiamini jinsi ulivyo na tambua Mungu hakukosea kukuumba namna ulivyo, tatizo liko kwetu binadamu tunakosoa uumbaji wa Mungu. Kama umeona una mapungufu basi tambua kila binadamu ana mapungufu yake.
Aisee it's really hard to live that way Mkuu
It needs high level of commitment
Lakini Ahsante Sana Ndugu kwa kunipa moyo
 
daaaaaah.... nimewahi kuona watu kama wawili watatu waliokuwa na tatizo kama lako

wakajikondesha ila bado makalio yakabaki kuwa makubwa

mimi nahisi ni bora kukubaliana na hali as long as uanaume wako upo palepale basi sidhani kama kuna tatizo

chukulia hilo kama tofauti ya kimaumbile ya kawaida kama vile kuna mnene kuna mwembamba kuna wengine warefu na wengine ni wafupi

wengine wana uume mdogo wengine mkubwa wengine mwembamba wengine mnene

ukisema uanze kutafuta madawa ya kupunguza makalio naona utakutana na matapeli wengi na usifanikiwe

maybe surgery will do ila kwann ufike huko wakati ndio mungu akivyokuumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Surgery hapana Mkuu Never
You know I heard something that can Cure it. So I wrote this thread to Confirm that What I heard its a Solution and to get some New thought as well
Poa sio mbaya acha tusikilize na wengine wananjia ipi maybe utaconfirm hiyo njia kutoka kwa wadau wengine wakaja na solution nzr zaidi.
 
Firts step towards healing is acceptance.

Jifanyie assessment ww mwenyewe, vipi ukiangalia wazazi wako kuna mwenye shape ya haja, kati ya baba na mama nani ana tako la haja. Kama mmoja wapo yuko hivyo basi zitakuwa na genetics tuu umerithi.

Kama sio wazazi basi angalia koo za pande zote, baba na mama. Lazima kuna upande utakuwa na hiyo gene tuu. Hivyo hamna haja ya kuwa na anxiety na hali yako.

Kingine jiassess kama umekamilika, i mean kama una sifa za kuwa mwanaume rijali. Una uume standard, una dindisha, una matamanio na wanawake, pigo zako ni za kiume n.k.

Kama una hizo sifa zote basi hauna tatizo lolote la kijinsia. Kama ni tofauti na hapo basi hormone za kike zitakuwa zimezidi hivyo utahitaji uonane na wataalamu wa masuala ya jinsia ili kuweza kudetermine your true gender identity.

Unforgetable
 
Ni ngumu lakin jitahudi ukikubaliana na Hali nakwambia utashangaa mwenyewe
Aisee Mkuu Swala la kukubaliana na hiy Hali ni ngumu sana. Kuna Siku vitoto vya kike kama vitatu hivi navifaham nlikua napita vikawa Vinaniongelea nikaskia nilijiskia vibaya Sana Mkuu Mmoja alisema "huyu kaka ananenepa mpaka Makalio Moo Click,
 
Back
Top Bottom