Msaada tafadhali: Jinsi ya kuondoa/kuzuiya matangazo ya biashara (Pop up Ads) kwenye simu

Mwenzetu

JF-Expert Member
Dec 16, 2010
550
193
Wadau nawasalimu wote,

Naomba msaada wa jinsi ya kuondoa au kuzuiya (ku dis-able pop up ads) kwenye simu. Ninatatizwa na kukuwaza sana na matangazo hasa yanayojitokeza kwenye simu wakati ninapokuwa na peruzi nyuzi humu jamvini.

Niseme ukweli mfano wa hili tangazo la TALA linanikera sana na sijui namna nitakavyoweza kuliondoa na mara nyingi limekuwa lina nililia bando zangu tuu.

Hivyo,naomba mwenye ujuzi wa namna ninanvyoweza ku block naomba anisaidie.

Wasalaam,

MWENZETU
 
Pole sana mkuu,

Hili limekua tatizo linalowasumbua wengi sana mpaka sasa hasa watumiaji wa simu za makampuni ya Tecno, Infinix na Huawei

Hatua ya haraka ya kufanya hivyo kwanza ni ku-Reset sim yako kisha uanze kuingiza app upya na setup zako.

Lakini hatua nyingine ni kwenda katika mfumo wako wa setting wa simu kisha tembelea apps, Ukifungua apps itafute app ambayo inadababisha pop up notification kisha restrict app kufanya hivyo.

Kama bado itaendelea, Bas hiyo simu itakusumbua sana hasa ukiwasha data.

Kujikinga na hii ni kuacha kudownload kila kitu, Au kusign in kila sehemu unayoona mitandaoni, Mara sijui mashindano, Mara kucheza games online haya yote ni hatari sana

Muda ni sasa, Tumia ulichonacho, Fanya unachoweza.
 
Asante sana kwa taarifa Mkuu,je nalipia kwa nani na ni kiasi gani? kwa jinsi ninanyokereka niko tayari kwa lolote.hebu nisaidie

MWENZETU
Huwezi mkuu dola moja sasa hivi ni 2300 bei zinatofautiana unalipa kwenye mtandao wa kijamii au search engine husika.
.
Mfano umeliona hilo la TALA instagram bonyeza kwa juu ya tangazo utaona dots tatu kisha li_block (hautoliona tena) ila ukitaka na mengine yoote utalipia ni hivyo hivyo na facebook.
.
Au waweza ku_download cracked apk za ku_block ads ukiwa kwenye websites
 
Back
Top Bottom