Msaada tafadhal kuhusu recovery partition / recovery disc????(dell laptop) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada tafadhal kuhusu recovery partition / recovery disc????(dell laptop)

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Skillseeker, Jun 16, 2012.

 1. Skillseeker

  Skillseeker JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Habari za kwenu wanaJF,

  Hivi karibuni nimenunua laptop mpya ya dell xps 15z ambayo ina space ya 750gb hdd, 8gb ram, 2.8Ghz, intel core i7, 64bits. Nimeikuta ikiwa na windows 7 home premium SP1.

  Kama mnavyojua hizi versions za windows zinatofautiana kabisa. Kwa matumizi ya kawaida zipo sawa ila kwa wale wanaofanya baadhi ya tasks watakubaliana na mimi kwamba kuna tasks ambazo unaweza kufanya kwenye professional but home ikakataa kutokana na limitations. Kwa upeo wangu nafahamu kuwa ultimate version ya windows ndo huwa imekamilika. hainaga matatizo.

  Lengo langu lilikuwa nikutoa windows7 home P SP1 niweke windows 7 ultimate 64bits. Kabla sijaizima laptop kulikuwa na partition moja (c: ). Wakat naanza process ya kuformat nilipofika sehemu inayoonyesha partitions nikakuta zipo 3,moja ni ile ya kawaida ya Disk 0 ambayo ilikuwa around 108MB, then kuna nyingine ilikuwa imeandikwa RECOVERY PARTITION ambayo ilikuwa ina 19.5GB(type: system partition) na ya tatu ilikuwa ndo hiyo partition ninayoiona mimi nikiwasha laptop ambayo type yake ni primary. Haya ndiyo maswali niliyokuwa najiuliza:
  1. Kwanini sikuweza kuiona hii partition ya 19.5GB??
  2. Najua umuhimu wa hii partition ni katika kurepair OS ili iweze kuwa kama ilivyokuja pale itakapokuwa corrupted. Sasa jinsi gani naweza kuiona hii partition?
  3. Jinsi gani naweza kutengeneza partition kama hii baada ya kuformat laptop ili niwe na recovery partition ya windows 7 ultimate?
  4. Naweza kutengeneza recovery disc badala ya recovery partition?
  5. Kwakuwa hii laptop inawarrant je kuiformat kabisa na kuanza kuifanyia configuration zangu mwenyewe inaweza ikafanya warrant yangu kutotambulika pale nikipata tatizo lolote ambalo litaitaji nitumie warrant yangu kulitatua?

  Naombeni mnisaidie niweze kupata majibu ya haya maswali matani ninayojiuliza. Nia yangu ni kuweza kuformat hii laptop na kuiwekea partition zangu mwenyewe zenye ukubwa ninaotaka ili niweze kutumia vizuri space niliyokuwa nayo lakini pia niweze kuwa na haki katika warrant yangu ambayo ni international.

  Nakushukuru wewe uliyechukua muda wako kusoma haya yote niliyoandika.

  Ntashukuru endapo utaweza kunishauri au kunipatia ufumbuzi wa haya yote niliyoyaongea au baadhi yake ambayo unaweza kuyatatua.
   
 2. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,577
  Likes Received: 846
  Trophy Points: 280
  nitakuwa maeneo haya nami nikisubiri jibu ya swali lako la tatu.
   
 3. N

  Nyasiro Verified User

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 20, 2012
  Messages: 1,286
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Usipate tabu sana kwa hiyo Recovery Partition kutoonekana kwenye Kwenye kompyuta. Mimi nadhani ni kwa sababu ina files za muhimu kwa ajili ya kurepair PC yako, pili nadhani huwezi kuiona kwa sababu unatumia Win 7 Home amabayo ina limited features ya matumizi ya kawaida ya nyumbani AU haina drive letter. Kama unataka kure-allocate disk space install software kama Partition Magic au nyingine ingawa Partition Magic huwa inamatatizo kwenye Win7. Hiyo 108MB sidhani kama inashida hata ukiformat laima itabkia sehemu fulani kulingana na size mpya.
  Ili kuiona hiyo partition jaribu ku-upgrade kwenda Professional au Ultimate au install disk management software kama Partition Magic.

  Jinsi ya kuitengeza: How to Create a Recovery Partition in Windows 7 - YouTube

  Kuhusu Warranty: Warranty haina uhusiano wa moja kwa moja na software including OS. Warranty inaharibika kama utafanya modification ya hardware kwa kuifungua PC na kuongeza RAM, HDD, n.k lakini kuformat hakumaanishi warranty imeharibika.

  Jinsi ya kuifanya ionekane ANGALIA HII: how to make dell recovery partition visible in my computer - YouTube
   
 4. leh

  leh JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 846
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kwanza, hio partition ya kwanza ya around 120mb inafanywa ni windows 7 (all versions) na inatumika ni windows kuweza kuboot kompyuta yako, ergo hutakiwi kuigusa au kama unataka, iformat uki install windows. sioni sababu ya kusumbuka nayo (its only 120mb na una gb za kutosha + hata ukiweza kuiformat na merge na partion nyingine, windows itaiweka tena). siku zote ignore hiyo partion
  pili, hiyo partition ya recovery inawekwa ni baadhi ya manufacturers kusaidia kurudishia windows na progams zilizokuwa installed. kama unafanya installation mpya, naonelea ni bora kuidelete na kuifanya part ya hdd yako. haina madhara yoyote na itakuwa useless ukidelete system ya zamani.
  tatu, umesema laptop yako ina 8gb. kama unafanya installation mpya ya windows, make sure its a 64bit edition. nasisitiza kwanini?? x86 au windows ya 32bit haisomi zaidi ya 4gb. hiyo ndo the biggest difference kati ya 32bit na 64bit. watu wengi hawalijui hili na wanatumia version yeyote. kama una kompyuta ambayo ina ram chini ya 4gb, always tumia 32bit coz 64bit ni nzito na itakuwa inatumia ram yako bure.
  tatu, recovery disk au partition si ya kurepair windows, ni ya kurudishia programs and settings on your computer after a new installation. haswa pre-installed programs ni manufacturer wa laptop yako. windows ikicorrupt, ina uwezo wa kujirepair, au shida ikiwa kubwa, inatumia cd uliyo install windows nayo. kuna programs za kutengeneza recovery disks, lakini mi sioni maana yake. kwanini nasema hili? coz nina system moja nayopendelea watu watumie. inaenda hivi: install windows and programs on partition 0 (usually C:/) and save everything else on other partitions (D,E,F..). hii itakusaidia incase upate shida yeyote na uhitaji kuweka windows upya. unadelete C:, unaweka windows, rudishia programs na komyuta yako inakuwa kama ya jana. therefore sionelei raha ya recovery disk
  and lastly, hakikisha kuwa warranty itabaki ukibadilisha OS. nasema hivi coz nilikuwa na rafiki wangu a.town laptop ilimzia baada ya 1 week. coz ilikuwa na guarantee, alivyoniletea, nikamshauri kwanza turudishe dukani wairekebishe wao. cha kushangaza, walisema warranty ni void baada ya kuweka windows mpya (ilikuwa imekuja na vista, akaweka 7). safest thing ni uwaulize ndo wasije wakabadilika if anything happens.
  mkuu, unmenunua bonge ya lappy, congrats
  **regards, leh :)
   
Loading...