Narudishaje files nilizofuta kwa bahati mbaya kwenye laptop?

Forgotten

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,346
10,220
Habari wana-JF, hapa nilipo sielewi nifanyaje maana nimepoteza data za 8 GB humo kulikuwa na files nyingi sana za muhimu ninachoshukuru documents nilizifanyia backup kivyake.

Laptop yangu ilikuwa imejaa sana na files zimekaa bila mpangilio sasa kwasababu nina laptop nyingine ambayo huwa siitumii sana nikaona nihamishie files zangu kule ili zikae nikifanya mpango wa kuziweka kwenye cloud storage pia.

Sasa nilichofanya nikaziweka kwenye ZIP file nika-copy kwenye flash sasa katika kuzihamisha kwenye laptop nyingine ile inatumia LUBUNTU OS ila kulikuwa kuna partition ya NTFS sasa ikawa kila nikiweka ikifika 47% haiendelei na kule kwenye Windows nilishafuta file nikiamini ntacopy files kwenye laptop nyingine. Basi nikaachana nayo ili nije nipige Windows OS kurahisisha kazi sasa baadae nikajisahau kwamba nilishafuta lile file kwenye main laptop nikafuta kila kitu kwenye flash sasa leo ndiyo nimekuja kushtuka nimeshapoteza files zote.

Nataka mnishauri ni software gani inaweza kusaidia kurejesha files, najua naweza ku-google tu au kupitia video kadhaa YouTube ila msaada wa hapa ni bora zaidi kulingana na experience za watu.
 
Zipo nyingi ila nyingi zinauzwa. Download recuva ila jitahidi usiweke faili lolote kwenye hiyo disc kabla hujamaliza ku recover.
 
EaseUS google then tafuta cracked kama una hela lipia dolari kadhaa

N.b usibackup kwenye faili ambalo mwanzo lilikuwa na data hizo you will permanently lost them
 
Back
Top Bottom