[Msaada] Sony Xperia L: Tatizo la Sauti

DJ Kassu

JF-Expert Member
May 3, 2012
382
282
Heshima kwenu wakuu. Nina tatizo kwenye simu yangu ninaomba msaada wenu. Ninatumia simu ya Sony Xperia L (C2105). Ni miezi minne sasa device hii inashindwa kutoa sauti kama ilivyokuwa mwanzoni. KWANZA; Nikipiga/nikipigiwa simu huwa inanilazimu kuweka Loudspeaker ndio niweze kupata perfect conversation. PILI; Audios na Videos hazitoi sauti mpaka pale ninapokuwa nimepiga simu na kufanya maongezi through a loudspeaker and eventually simu ikikata na Audio/Video nayo hupoteza sauti. TATU; Headset (Channel ya Earphone/Headphone) nayo haifanyi kazi, everything runs through a Loudspeaker tena wakati nikiwa on Call pekee. Vitu pekee ambavyo vimebaki vinafanya kazi normally kwenye upande wa sauti ni RINGTONE, ALARM & NOTIFICATION SOUNDS pekee. Tatizo lilianza siku ambayo nilikuwa najaribu kuconnect simu kwenye subwoofer ili nisikilize muziki kwa ujazo mkubwa (nimekuwa nikifanya hivyo mara kadhaa kabla ya tatizo kutokea). Still ninashindwa kuelewa kama tatizo lilikuwa Subwoofer au kuna tatizo lingine zaidi kwenye system ya Audio. Mwanzoni nilidhani Subwoofer imepiga shoti simu yangu lakini nakosa logic connection kabisa. Naomba msaada wenu wataalamu. Ninatanguliza shukrani zangu za dhati. Ahsante!
 
Hilo ni Tatizo la hardware, Nenda Kwa Fundi akabadishe mike
 
Back
Top Bottom