Msaada: Sijawahi kupenda kutoka moyoni

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,076
1,975
Habari zenu waungwana,

Mimi ni mvulana kuna kitu kinanisumbua kuhusu upendo hususani katika mapenzi. Sikuwahi kumpenda mtu kwa dhati kutoka moyoni nimewahi kuwa katika uhusiano na wasichana kama watatu kwa nyakati tofauti lakini hakuna hata mmoja nilimpenda, japo najilazimisha na sijawahi kumpenda mtu bali ni kumtamani tu na nikimpata nikimaliza haja zangu natembea.

Ilifika wakati hata niliyewahi kuwa nae niliwahi kusoma meseji zake akichat na jamaa mwingine lakini sijaumia zaidi ya kuchukilia kawaida tu hata nikimsikia akiongea nae huwa nilikua namwambia endelea kuongea nae tu, aliwahi kuomba msamaha lakini nilijikuta sijali pia alishawahi kuniuliza HUJISIKII VIBAYA NIKIONGEA NA MWINGINE (huku akilia) nilimjibu "ndio".

Wao ndio walikuwa wananitafuta lakini mi sina mpango nao japo nilijilazimisha lakini hola. Nimewahi kuwa mwanachama wa CHAPUTA ila nilipoteza kadi (niliacha) pia napenda sana kuwa pekee bila kuwa na mtu na nafurahia mahusiano ya watu wengine japo inanitesa hii hali, naombeni msaada nini nifanye.

AHSANTENI
 
Theway ulivyo ndio jinsi ulivyo, na endapo utataka ufuate watu wanavyotaka wewe uwe, basi inamaana kwamba unataka kujikana na inakuwa maisha yako yamekushinda kuyaongoza sasa unawapa ruhusa watu wakubadilishe vile wanavyotaka wao... Anyway Sasa Tuambie unaomba msaada unataka uwe kama nani?
 
Nataka nipende na mimi pia natamani kuwa na mtu
 
Umesema ni mvulana bado una muda mwingi mbeleni tulia omba Mungu atakupa mkeo.
Vinginevyo ndo maumbile yako na hauko peke yako mdogo wangu sasa naamini kwamba Mungu katuumba wengi wa hivyo mi dadako wanaume wanateseka kama hao wasichana wako.
 
Ah kweli!!!!!!!????? Ushawahi kutendwa?
 
Ah kweli!!!!!!!????? Ushawahi kutendwa?
Siyo kutendwa ila sina muda wa kumpa mtu attention ya kutosha so hawanisomi wanaumia na kushindwa cha kufanya so niliye naye ameamua kuniacha kama nilivyo tu anavumilia. Muda mwingine najishtukia kama wewe hivi na kujiona huenda nina hatia lkn baade hali kama mwanzo. Hivyo naungana na STUNTER alivyosema hapo juu ni bora kujikubali ndiyo wewe ulivyo na ndiyo tafauti yako na mtu mwingine mkuu.
Ila kuna room ya kujirekebisha pia ila mi nimeshindwa kinachonisaidia ni hofu ya Mungu na aibu kwa wazazi na jamii tu.
 
Sasa kwa hili tunaweza kuishi na wake/waume?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom