Msaada sheria ya kuvunja mkataba wa nyumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaada sheria ya kuvunja mkataba wa nyumba

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by 1800, Aug 12, 2012.

 1. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wadau wale wenye utaalamu wa sheria naomba msaada wenu!mimi ni mpangaji ambae mkataba wangu uliisha tarehe 10 july,mkataba wa awali ulikua wa miezi sita kwa kodi ya 720,000 kwa maana ya 120,000 kwa mwezi,baada ya mkataba kuisha niliongea na mwenye nyumba akanipa mkataba wa miezi minne yaani mpaka november 2012,na mnamo tarehe 29 july nikampatia 400,000/= na ikawa imebaki 80,000 ambayo nilimuahidi kumlipa in three weeks time!cha ajabu juzi amenigeuzia kibao,anadai anataka kukata kodi ya mwezi mmoja alafu anirudishie pesa yangu iliyobaki kwa kua anataka kumuingiza mtu mwingine!je sheria inasemaje hapa wadau,na nikitaka msaada atakapotaka kuja kunitoa ndani ya nyumba nianzie wapi ili kumzuia
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mmmh!Kweli tusio na nyumba tunateseka sana,pole sana ndugu.
  Binafs sijui sheria ngota wanasheria waje watuelimishe.Ila naweza kusema kuwa mwenye nyumba ndio anaanza kuvunja mkataba je sheria inasemaje kwa upande mmoja kuvunja mkataba?je swala la notes lipo vip?haya ntaomba wanasheria watusaidie
  Ndugu mambo haya yanaboa sana,angalia sasa unaacha shughuli zako unaanza kufikilia mambo ya mwenye nyumba
   
 3. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante mkuu,jamaha unyanyanyasaji wanaotufanyia ni wa kuvuka viwango,ngoja tuone wajuvi wa sheria watanisaidiaje!maana niko njia panda
   
 4. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi sio mwana sheria lakini nina jicho lisilo la kisheria kung'amua kwamba mwenye nyumba wako hakutendei haki.

  1. Alitakiwa kukutaarifu kuwa hatakuongezea mkataba mwingine miezi 3 kabla ya mkataba wako kumalizika ili wewe hiyo miezi 3 usake nyumba nyingine.

  2. Anataka kukusanya kwani kama angeweza kusubiri mkataba wako uishe kwa kufuata condition ya miezi 3 ndio akuambie kuwa anaingiza mtu mwingine au hata kukuambia anasitisha kupangisha mpaka atakpo amua vinginevyo.

  3. Anachokufanyia ni kinyume maana hata wewe ndio ungekuwa mwenye nyumba na ungemfanyia wewe anachofanya kwenye malipo asingekubali.

  Ushauri.
  Kama mtaani kwako kuna chama cha wapangaji waone ka ushauri zaidi lakini pia si vibaya kumtaarifu balozi au mwenyekiti wako wa mtaa. Hii itakusaidia pindi atakapo kuchukua uamuzi wa kutoa vyombo kwa nguvu.

  Pole mpangaji mwenzangu. Nakushauri tuzidishe mapambano angalau tuwe na vibanda vyetu haka kama ni kama vya kuku.
   
 5. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu asante sana kwa ushauri wako!
   
 6. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Huo mkataba wa pili ulishasaini/ yaani wewe na Landlord wako? wote mlisign? kma ndio fungua shauri lako kwenye Baraza la ardhi na nyumba la kata( Ward Tribunal) baraza hili lina mamlaka ya kumzuia kukuondoa kwenye nyumba maana kwa kufaanya hivo atakua amevunja mkataba aliosign yeye mwenyewe bila kulazimishwa....
   
 7. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu wkataba wa pili bahati mbaya sijasign nae,kwa kua yeye anaishi Iringa na mimi Morogoro,aliniambia nimtumie hiyo amount kwa mpesa,nina msg tu ambazo alinitaka nitoe hela ya miezi minne,na msg ya Mpesa niliyomtumia,alihaidi mkataba angekuja nao yeye atakapokuja Morogoro!nina mkataba wa awali tu
   
 8. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Kitendo cha kukubali pesa ina maana ameshakubali na hiyo tunaita perfomance of contract, sasa anachotakiwa kufaya yeye ni mambo mawili tu kisheria, 1. aje msign mkataba na umalizie pesa kwa mda mliokubaliana au 2. wewe akurudishie pesa yako yote na wakati huo huo wewe unawweza kuomba compensation ya usumbufu...
   
 9. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu,kwa hiyo kwa kuanzia mimi niende wapi?baraza ardhi au?yeye anataka kumtumia balozi wa nyumba kumi ili kufanikisha eviction
   
 10. Jaslaws

  Jaslaws JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 5,151
  Likes Received: 2,195
  Trophy Points: 280
  sheria zetu hapa zinasemaje kuhusu acceptance kwa njia ya posta(ama acceptance kwa mtindo uliotajwa na mlalamikaji?)naomb ufafanuz kdgo hapa mkuu.
   
 11. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Wahi baraza la ardhi la kata
   
 12. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Asante sana mkuu!ngoja niwahi huko
   
Loading...